Wachaga wa Kirua Vunjo BANA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachaga wa Kirua Vunjo BANA

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by MPAMBANAJI.COM, Oct 24, 2011.

 1. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Hivi karibuni nipata kumsindikiza jamaa yangu hapa mjini huko kwao, kweli wachaga wengi wameendelea. Nikiwa huko nlipata kuona barabara inayosemekana kuwa inatengenezwa kwa kiwango cha lami hadi eneo liitwalo marangu mtoni. Kwa bahati mbaya naambiwa barabara hii imechukua muda sana bila ya kukamilika. Ilisemekana kuwa ingemalizika mwaka huu mwezi june kutokana na maelezo yao.

  Sasa kilichonishangaza kuna baadhi ya maeneo wamewekewa mbolea barabarani ambayo inasemekana ni moramu kwa ajili ya utengenezaji wa barabara. Lakini pia liniona wengi wakiangalia bila hata ya kuongea lolote. Ama kweli hawa wachaga wa KV hawana hata diwani au kiongozi wa kijiji anayeona hayo?

  Ilinishangaza sana kwani pia inasemekana kuna Mangi maarufu sana kwa wakati huo haonekani hata kwenye vitabu vya historia na wala jitihada zake inasemekana hazipo hata kwenye vitabu vya kihistoria ngazi ya kata na wilaya. Nyie wachaga wa KV mbona hampambanii maendeleo kwenye maeneo yenu.

  Hii inanipa wasiwasi kwani mchaga yeyote ukimwambia umetoka wapi basi atakuambia mie nimetoka MARANGU. Nawasihi mkomalie ile mbolea itolewe kule barabarani kwenu na muwekewe morum kulingana na vigezo vya barabara.
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  tatizo la tz ni kuwa wasomi wengi tumekimbilia dar na vijiji na miji midogo inaongozwa na wale waliokuwa wanashika mikia madarasani na wengi wao ni wale waliofeli mitihani ya darasa la nne. Usishangae uchagani kuyaona hayo, yako kila mahali
   
 3. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  mkuu nafikili ile barabara uliona ilivyo.kuna sehemu nyingi korofi kuna mabonde mengi sana na kona za hatari.ukiangalia ile barabara ina milima na mitelemko mikali.sio kweli kwamba ile barabara imewekwa mbolea.ukisema inachukua mda mrefu ntakubali.nadhani mwenyewe umeona jografia ya kutoka pale mwika hadi marangu mtoni.kwa upande wangu naona jamaa anajitahidi sema tu aongeze bidii.mi nampongeza sana yule alotengeneza kijipande cha barabara kutoka pale mwika hadi himo.ipo kiwango.mia
   
 4. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,532
  Trophy Points: 280
  kama sikosei hiyo moramu aliiweka mzee wa kiraracha wakati akiwa kaimu waziri mkuu
  baada ya kile cheo kwisha naye akafulia akashindwa kuikamilisha
  tuone kwa sasa anaweza akafanya hiyo kazi.
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kaendelezeni makwenu nyie.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,562
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Mpambanaji unayayasema ni kweli, KV ndilo eneo la mwisho kupata maendeleo Moshi yote. Wachaga wa huko hawako ambitious wala sio wapenda pesa. Ila pamoja na umasikini na uzubaifu wa Wachaga wa KV, eneo hili ndilo linaloongoza kwa kuexport marriegebility ladies, ukipata binti wa huko, wanatulia na hawana makuu, hata umvishe kaniki na kulalia maji wanaweza ili mradi Jumapili lazima aende kanisani hata kwa ndala.

  Ukienda kuposa KV, haalizwi motokari, kabati la picha, kabati la mbeho na ATM, kule unajichukulia kama umeokota na wanatulia nyumbani.

  Ukioa Marangu wanawake hao ni royal family, wateke, walaini na mitulinga hawawezi idara zote!.

  Ukioa Machame, nadhani sera zake zinaeleweka wazi lazima ujifunge mkanda na ghubu la kulazimishwa utajiri haliishi, na likiisha ujue ndio safari!.

  Mangi wa KV aliitwa Mashingia, enzi hizo za kale, kila kizuri ilikuwa ni kwa mangi kwanza akishachagua, masalia ndio wengine wapate!.

  Eneo hilo Kanisa Katoliki ndio limetamalaki, wana makanisa mawili, Uparo na kule juu Iwa. Mapadri ni kama miungu watu, hufolenisha kuwabariki hata wake za watu, na mume akisikia mkewe kaitwa kanisani, ni furaha tele kwa padri kuweka baraka!.

  Ukienda sherehe zao, wanaume wanakaa peke yao, na wanawake peke yao!, hiyo ndio KV!, huko lile somo halieleweki kabisa, wengi huanzishiwa migombani, ila thank God, wachaga wa KV sio gogo na gazeti hawasomi!.
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu pasco, hebu mtake radhi mheshimiwa James Mbatia, yeye ni wa pale Iwa,

  pasco kuna kirua vunjo mashariki pia ambayo hutumia njia ya uchira kuna kanisa la tatu linaitwa karumeli
   
 8. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  nadhani kama ndivyo basi hawa wachaga wa KV watengeneze mtandao wa kuhamasisha maendeleo ya huko kwao. kweli maoni yenu yanaendana na hali niliyoiona. Sasa Mbatia anamtazamo gani? hapa nakumbuka kuna majamaa wakati nasoma wakiambia wewe ni wa KV nn.walikua wanakasirika kweli kweli
   
 9. g

  glory zephania Member

  #9
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KV pombe imewazid hawa ndugu zetu..inabid wajirekebishe hawa watu..
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,277
  Likes Received: 5,637
  Trophy Points: 280
  Hee napita tu
  mie wa maranagu siruhusiwi kuchangia tusubiri wa kv
  wakina mosha assey mlay mko wapi aisee baabanguuu wameaaanza kuzalilishanaa embu njooni mjibu maswali jamani na kwa nini mmekimbilia wote darrrrr mmeawacha housegirl kijijini??
   
 11. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jamanii kwa kweli mimi ni mwenyeji wa KV kapisaaa.. sasa hayoo mnayosema kiasi yana ukweli kama hilo la miundo mbinu mibofu ya barabara kwa miaka mingi. kituo kikuuu cha usafiri kuelekea kirua magharibi ni kawawa na kirua mashariki ni uchira. haki ya munguu kote hukoo bado tunapanda pick up, trekta au lori la mchanga/tofali/mawe.

  kikubwa kinachokwamisha maendeleo KV ni wazawa wa kule haswa waliosoma na waliopo katika miji kama DSM kushindwa kukaa pamoja na kutafakari mustakabalii wa nyumbani. mimi kila xmass najitahidii kwenda nyumbanii na nimeanzaa kuwashawishii wensanguu tukae pamoja kujadili maendeleo ya hukuu kanyiii.

  Natoa wito kwa WAKV wote walioko hapa DSM tuanze mchakato kupitia chama cha maendeleo kirua kilichokufa kutokana na ubinafsi wa VIONGOZI kifufuliwe na Vijana wapenda maendeleo wakamate usukani tuhamasishe maendeleo kirua. Aisee nashukuu kama mitandao kama JF inajadili changamoto za KV.

  TUAMUE,TUNAWEZA JAMANIIII WAKV...
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,277
  Likes Received: 5,637
  Trophy Points: 280
  Kabla ya kukifufua tambua mianya iliochangia kukiua na kama uongozi hakikisha umepata ulioaminika ndio mkianzeishe na mlikuwa mnaenda mbali kwelikuliko wa marangu kabla ya wamarangu kuingiza wenye akili zao...
   
 13. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,532
  Trophy Points: 280
  ndo kusema kuwa nyie mko town na wake zenu wako huko shamba,
  kazi kwenu aise.
   
 14. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Nitakua tayari kuhudhuria hicho kikao na nitachangia kama an interested observer.Kama kweli we ni mwanaharakati itisha kikao kupitia vyombo vy a habari nami nitawasaidia mwazo.au kama vipi in a private sms ntakusaidieni kutengeneza mwongozo. KWELI basi waKV WAPO NYUMA sana kimaendeleo.Nazidi kukumbuka kweli eneo tulianza kuelekea huko linaitwa kawawa na kweli niliona pickup na malori hii ni shida na kazi kweli kweli. duuuu
   
 15. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  naomba uni pm huo mwongozo ili tuanzie hapo.

  Kuhusu kufufua chama nilikuwa natoa mwito kwa wana kv wote walioko hapa jf tutoe way forwad itakayoharakisha mchakato wa kujadili changamoto za maendleo kv na tuanze utekelezaji kwa kukutana mapema na kusonga mbele.

  Natumai chama kipo ila kimekufa kutokana na uongozi dhaifu ulioweka mbele ubinafsi.

  Wakirua tuache ego tujipambanue kama watu tunaoweza kutenda na tusiwe watu wa short term benefits and cheap popularity.

  Kwa data za haraka, kv ni moja ya maeneo makubwa zaidi kijiografia katika eneo la vunjo na lenye idadi kubwa ya watu, wasomi wapo pia japo wengi tuna ubinafsi zaidi.
   
 16. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  usihofu, lnipo tayari kabisa kushiriki katika kusaidia.ntakuja na mwongozo itakapofikia siku ya kikao ukifanikiwa kukiitisha.Nitafurahi nikisikia hawa viongozi wa kichama kama nao watakuwepo hususani huyo Mbatia na Mrema. I will be very interested to hear
   
 17. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Basi kikao kitaitishwaa karibuni na Mbatia na Mrema wataalikwaa japo sijui kama wanaweza kukaaa meza mojaa bado hata kwa majadilianoo..
   
 18. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,532
  Trophy Points: 280
  kwenye mambo ya home watakaa meza moja tu
   
 19. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  poa. kweli jitahidini tupo pamoja. Pia nawasili uwazi uwepo na mseti vipaumbele haswa miundominu,elimu na miradi midigomidogo katika eneo lile.Lakini mbana nasikia wapo wakatoliki maendeleo yapo juu sana.Kama mmja wa replies neona kuwa yapo makanisa matatu ya Katoliki na lutheran au misikiti vipi? kweli hapa pagumuQUOTE=Mamndenyi;2697242]kwenye mambo ya home watakaa meza moja tu
  [/QUOTE]
   
 20. Pendael24

  Pendael24 JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2015
  Joined: Feb 13, 2014
  Messages: 1,805
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  Chaajabu mpaka leo hii hio barabara bado haija kamilika,kwakweli kirua iko nyuma sana
   
Loading...