komasalonde
JF-Expert Member
- Sep 9, 2024
- 2,742
- 3,520
Hii dunia imethibitika kabisa kuwa Ina rasilimali za kutosha kuwawezesha watu wote duniani kula, kusoma, kutibiwa, kutalii, kujenga/kupanga na kufurahia maisha.
Bahati mbaya sana, ubinafsi, ubabe na uchoyo ama wa kisiasa au kuitawala umehodhisha rasilimali zote kwa vikundi au watu binafsi, huku waliobaki wakiteseka, wakiugua, wakishindwa kusoma, wakikosa matibabu na hata kufa.
Nchini Marekani, asilimia 10 tu ya idadi yao, humiliki asilimia 60% ya pesa zote za nchi. Na asilimia 90 ya watu waliobaki wanaambulia asilimia 40 ya mali zote.
Hapa Tanzania kwa mfano, jarida la African Wealth report la 2022 linasema kuwa watu karibu 2357 wanamiliki mali/pesa za thamani ya usd bil 5 plus. Yaani kati ya watu milioni 60 Tanzania,, watu 2,357 asilimia ndogo sana wanamiliki mali kubwa.
Kumiliki mali sio tatizo. Tatizo ni njama za watu hao wachache/kikundi kutumia chama, dola, nguvu za giza na hila ili kupora mali zote za nchi.
Wachache/kikundi hawa, ni makatili, wababe na roho ngumu kupora kila rasilimali bila kujali waliobaki wanaishi au wanakufa.
Bahati mbaya, wengi wanaobaki maskini hawana namna ya kutetea, kulinda na kudai ama mgawanyo wa rasilimali au kuwezeshwa kupata nao sehemu ya urithi wao halali wa nchi.