SoC02 Wabunifu wengi hawana vyeti ila wanavipaji ambavyo havithaminiwi ndani ya taifa lao. (05)

Stories of Change - 2022 Competition

Kingambe

Member
Sep 2, 2022
10
9
Ikiwa vocha imenunuliwa katika mtandao uleule na ikatumika ndani ya mtandao uleule faida yote na cash ile iliyolipwa wakati wa kununua ile vocha itakuwa ni haki ya mtandao ule iliyowekwa ile vocha. Pia endapo vocha imenunuliwa katika mtandao mwingine na kutumika katika mtandao mwingine.

Cash iliyolipwa wakati wa kununua vocha itakuwa ni ya mtandao iliyowekwa ila faida watagawana kati ya mtandao uliomuuzia mteja vocha na mtandao aliyoweka ile vocha na kuitumia. Katika mfumo kila mwezi kila mtandao utawapa cash mtandao mwingine kiasi ambacho kitaonekana katika mfumo (System)

Hii hakuwahi kuituma tena baada ya kuona hakuna ushirikiano kati yake na wamiliki wa mitandao ya simu na benki. Ulishawahi kuona unanunua kitu halafu anayekuuzia anakupa masharti baada ya kupokea pesa. Usipotumia kikaisha mpaka kesho nakuja mwenyewe kuchukua bidhaa yangu. Sasa iweje umuwekee mteja masharti wakati amekulipa pesa ?

Hiki ndicho wanachokifanya mitandao ya simu nchini na vifurushi vyao vwa siku, wiki hata mwezi. Haitendi haki hata kidogo, unakuta mteja anajiunga akiwa mjini kifurushi cha siku. wiki au mwezi, akipata dharula na kwenda kijijini ambako hata mtandao hakuna akakaa siku 1, wiki au mwezi wenye mtandao watakata kifurushi kile japo kosa au tatizo si la mteja bali ni wamiliki wa mtandao husika huduma zao si nzuri. Lakini anayehukumiwa ni mteja.

Bwana Kingambe aliibuni njia sahihi ya kumhesabia mteja muda wa kifurushi chake kwisha. Moja, muda wa kifurushi utahesabika pale ambapo mtandao unasoma vizuri. Hii inamaanisha hata kifurushi cha siku kinaweza kufika wiki, mwezi au mwaka. Pia cha wiki kinaweza kufika mwezi au mwaka na kifurushi cha mwezi kinaweza kufika mwaka na zaidi.

Hii inatokana na muda wa kifurushi kuhesabiwa pale ambapo laini husika ipo hewani na mtandao upo vizuri. Mfano, endapo mtandao utakuwa vizuri kwa kila siku dakika 5, itachukua siku 288 kifurushi kwisha muda wake. Endapo mteja atajiunga kifurushi na simu yake ikazima hata kama ni mwaka mzima, basi kifurushi chake atakikuta vilevile.

Pia hata kama mteja atasafiri kwenda sehemu ambayo mtandao haupo vizuri. Baada ya kukaa muda mrefu katika kijiji kile ambacho mtandao hakuna, siku yoyote atakapokwenda sehemu ambapo mtandao upo vizuri, bado kifurushi chake atakikuta vilevile. Mfumo huu utakuwa unatenda haki walau kidogo.

Lakini haki zaidi ni pale ambapo, mteja anapojiunga na kifurushi chochote basi asipangiwe muda wa kumaliza kifurushi chake. Atumie hadi atakapokimaliza. Ukiacha hilo bwana Kingambe, alikuwa anachukizwa sana na mitandao ya simu ya Tanzania.

Unakuta mteja hana haja na mambo ya kubeti au huduma mfano wa hizo, lakini anatumiwa sms kibao katika simu yake. Unajiuliza, ni kwanini mfumo uliwekwa hivi kusumbua wateja ? Bwana Kingambe alikuwa na wazo la kuweka programu ya sms ambayo kabla ya sms kuingia kutoka kampuni mbalimbali na za michezo ya kubashiri iingie sms ya taarifa kwa mteja. Mfano. Ndugu mteja, unapenda michezo ya kubashiri ?

Mteja akijibu ndio ndo sms za kubashiri zianze kuingia. Ila akikaa kimya bila kujibu chochote au akijibu hapana basi asitumiwe tena sms kama hizo. Unakuta unatumiwa sms za michezo mbalimbali kwa siku sms kibao.

Kama bwana Kingambe angepata fursa katika mitandao ya simu angetengeneza mfumo wa huduma ambazo zinaendana na mahitaji ya mteja. Mteja anapotaka kujiunga na huduma yoyote ataulizwa kiwango cha huduma anachotaka kisha ataambiwa gharama zake. Na mfumo huu pia uzingatie kifurushi ambacho hakina muda wa kwisha pia ni mitandao yote.

Mfano, mteja anataka dakika. Mteja ataingiza idadi ya dakika anazozitaka mfano dakika 100, kisha atatajiwa gharama mfano tshs 500/= (kila dakika 1 ni tshs 0.5) hivyo kila idadi ya dakika inazidishwa na tshs 0.5/= ila kunaweza pia kukawa na punguzo kutokana na wingi wa dakika ambazo mteja anatakakununua. Mfano kuanzia dakika 1000 hadi 2000 kila moja tsh 0.45.

Hii itamfanya mteja apate kifurushi anachokipenda katika sms, dakika na bando la internet. Bwana Kingambe pia, hakuridhishwa na utendaji wa mamlaka ya mawasiliano TCRA, kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwake na kulifanyia kazi suala aliloliripoti kwao. Hii ni kutokana application inayoitwa PIMAXNETA ambayo ni application ya utapeli.

Yenyewe ni application ambayo inatangazwa na wahusika kuwa inakuonesha sms ambazo mtu wako wa karibu anazowasiliana na watu wengine katika simu zao. Haipo katika play store ila ipo katika browser (opersmini). Wanakuonjesha kidogo baadhi ya sms zinazoingia katika ile namba. Ukitaka kuzisoma lazima ulipie tshs 40,000/= ili wakutumie namba ambazo utaingiza ili uweze kuzisoma zile sms, na baada ya kufanya malipo, hapo ndipo umeliwa.

Bwana Kingambe alishatapeliwa baada ya kukimbiwa na mkewe ambaye alimtoroka na watoto wake wawili. Utapeli huo ulifanikiwa kwa sababu rafiki yake wa karibu alishiriki kumthibitishia kama hata yeye aliitumia ile application hivyo akamuondoa wasiwasi bwana Kingambe akatapeliwa.

Baada ya kugundua kama ametapeliwa, bwana Kingambe ikabidi atoe taarifa kwa mamlaka husika. Kwanza makao makuu ya mtandao wa tapeli ambako aliambiwa awasiliane na mamlaka ya mawasiliano Tanzania. Aliwasiliana na TCRA na akaomba ile application ifungwe ili wengine wasitapeliwe kama alivyotapeliwa yeye. Ila mpaka sasa ile application bado ipo na wengine wengi wanaendelea kutapeliwa.

Sio hivyo tu, hata kwenye changamoto ya utapeli kwa kutumia simu wengi wametapeliwa na wanaendelea kutapeliwa kila siku. Kuna mfumo wa kutoa taarifa za utapeli. Ila cha ajabu kila siku watu wanatoa taarifa za utapeli na watu pia wanaendelea kutapeliwa.

Cha ajabu hakuna mrejesho ambao wananchi wanapewa kuhusu taarifa za utapeli wanazotoa kwa mamlaka husika. Mrejesho huo ni kama idadi ya taarifa za utapeli zilizopokelewa ndani ya huo mwezi. Pia hatua zilizochukuliwa na mamlaka kama vile kuzifungia namba zilizoripotiwa na wateja au watuhumiwa kukamatwa na kuchukuliwa hatua. Lakini mpaka leo watu wanaendelea kutoa taarifa na watu wanaendelea pia kutapeliwa na mamlaka zipo kimya.
 
Back
Top Bottom