SoC02 Wabunifu wengi hawana vyeti ila wana vipaji ambavyo havithaminiwi ndani ya taifa lao (01)

Stories of Change - 2022 Competition

Kingambe

Member
Sep 2, 2022
10
9
Baada ya kufeli chuo kikuu akiwa amebakisha mwaka mmoja, kwa kukosa ada, bwana Juma Ramadhani Kingambe akarudi nyumbani na hakuwa mtu mwenye kukata tamaa bali alikubaliana na kile kilichomkuta na kupambana ili maisha yaende.

Alirudi kwao Dar es Salaam akitokea Dodoma alipokuwa anasoma. Ila bwana Juma kabla hajafeli chuo kwa kukosa ada, alibuni bunifu mbalimbali ambazo aliamini angepata mafanikio ya bunifu zake hususani katika kukamilisha masomo yake.

Alianza na nywila zinazozunguka. Hizi ni nywira ambazo zinawaweka watumiaji wa simu na benki au katika mifumo mingine ya kutunza pesa sehemu salama zaidi, kuliko mfumo wa sasa wa nywira moja isiyobadilika.

Kutokana na umahiri wa bwana Juma katika hesabu, alizipata namba zenye tabia ya kujirudiarudia kila baada ya mara 42. Akaamua namba hizo azitumie katika mfumo wa nywira. Hii inamfanya mteja awe huru zaidi kwani haina haja ya kuificha nywira yake ya awali kwa sababu nywira hiyo baada ya kutumika mara moja basi haitatumika tena hadi mzunguko ukamilike mara 41.

Katika mfumo wa nywira inayozunguka kila mteja atakuwa na nywira 42 ambazo atakuwa anazitumia kila siku katika akaunti yake. Lengo kubwa la bwana Kingambe lilikuwa ni kuwaweka wateja sehemu salama zaidi pale ambapo ataibiwa simu au kadi yake ya ATM na mwizi akiwa anaifahamu nywira yake ya awali. Lakini kwa mfumo wa sasa, kama utaibiwa simu au au kadi yako ya ATM na mwizi anaifahamu nywira yako, umekwisha, unaibiwa.

Sio hayo tu, bali nywira inayozunguka ina namba zenye tarakimu kuanzia 3 hadi 4. Pia inabagua baadhi ya namba. Yaani kwa maneno rahisi si kila namba yenye tarakimu 3 au 4 ni nywira sahihi, bali kuna nyingine sio.

Hii itaendelea kumuweka mtumiaji wa huduma za kifedha kubaki salama na pesa zake. Pale mteja atakapoingiza nywira, mfumo utaichambua ile nywira katika tarakimu mojamoja (mamoja, makumi, mamia na maelfu). Endapo nywira itakayoingizwa itakuwa haiendani na nywira zetu, pia tarakimu zote 3 au 4 zikawa hazifanani na nywira yake sahihi, mteja atatakiwa kujaribu tena kuingia katika akaunti yake baada ya muda kidogo utakaopangiliwa katika mfumo (automatic system).

Mfano, kama nywira sahihi ni 2980 na mteja akaingiza 3641, huyu mteja atazuiliwa kuingia katika akaunti yake kwa muda baada tu ya jaribio moja. Ila endapo atakosea mpangilio wa tarakimu (mfano 1234 badala ya 3214) ataruhusiwa kuingia katika akaunti yake ndani ya muda uleule. Au atakayekosea tarakimu moja au mbili katika mfumo wa nywira (mfano 1234 badala ya 1257) pia ataruhusiwa kuingia katika akaunti yake muda uleule.

Aliandaa proposal mbalimbali na kuzituma katika benki na mitandao ya simu yote Tanzania. Wachache walimpa majibu ya kutia moyo na wengi walikaa kimya. Benki moja Tanzania ilimualika katika kuwasilisha mawazo yake.

Baada ya kumsikiliza kwa makini, walitoa hoja wakidai kwamba mawazo ni mazuri, ila mfumo huo kwa watumiaji utakuwa ni mgumu mno. Japo kwa upande wake bwana Kingambe, aliona ungekuwa ni mfumo mzuri sana kutumika na ungeweza kufanyiwa maboresho. Waliamua kumpa bwana Kingambe T-shirt ya benki yao kama pongezi ya ubunifu wake japo bwana Kingambe hakwenda kuichukua kwa sababu kwa upande wake T-shirt si lengo la ubunifu wake.

Kipindi ambacho bwana Kingambe amerejea nyumbani, hakuwa na kazi yoyote kwa sababu hana cheti cha taaluma. Kipindi hicho familia yake aliisafirisha kwenda Tanga (ukweni) huku yeye akibaki jijini kupambana.

Walitengeneza banda pamoja na wenzake na kuanza kufundisha masomo ya ziada (tuition) kwa sekondari, kidato cha kwanza hadi sita. Walipambana katika kufundisha na wakapata sifa sana katika kufundisha, ila wazazi wengi walikuwa hawalipi. Japo hana cheti cha chuo kikuu ila anashukuru kwa mwanafunzi wake wa masomo ya ziada (tuition) kutoka shule ya vipaji maalum Kibaha amekuwa wa kwanza kitaifa katika somo la Physics alilokuwa akimfundisha kuanzia pre-form one hadi anamaliza kidato cha nne.

Mwanafunzi huyo aliendelea kumuamini bwana Kingambe kwa kuendelea kufundishwa pre-form five na bwana Kingambe, somo la hesabu (advanced mathematics) Baada ya kuona wanafunzi wengi hawalipi, bwana Kingambe akaamua kwenda kwa mama yake kijiji cha Mwanadilatu kulima na kuchoma mkaa ili kuendelea kupata kipato.

Bado dhamira yake ya kuhakikisha wazo lake la nywira inayozunguka inatumika ili kulinda akaunti za wateja wote katika benki au mitandao ya simu.

Akaona apendekeze mifumo aina mbili ya nywira ambayo mtumiaji angechagua, atumie nywira ya namba zisizobadilikabadilika au nywira inayozunguka. Ila bado akapendekeza mfumo baguzi, ili si kila namba yenye tarakimu 3 au 4 iwe na vigezo vya kuwa nywira.

Pia, alipendekeza mfumo huohuo wa nywira inayozunguka ungewezakuwekwa kwa mtindo ambao mtumiaji aruhusu nywira yake kuzunguka na endapo hajaruhusu, basi nywira yake itaendelea kubaki ileile. Hii ni tofauti na ile ya kila unapoweka nywira mfumo unaibadilisha (automatic).

Baada ya kuweka maboresho hayo, akatuma tena proposal zake katika benki na mitandao ya simu mbalimbali nchini bila mafanikio.

Akaamua kuzigeuza zile namba ambazo ilibidi zitumike katika nywira inayozunguka na kuwa saini ya kimahesabu (mathematical signature), hii itawawezesha watu mbalimbali kuweka salama mali zao kutokana na wizi wa saini duniani.

Lakini kwa saini ya kimahesabu watu wenye kampuni mbalimbali wataendelea kubaki salama kwani hakuna anayeweza kuifahamu saini ya kimahesabu ya mtu. Katika mfumo utakaotengenezwa utatoa majibu ya aliyesaini kama ni mhusika au sio.

Huku akiendelea kuchoma mkaa na kulima kwaajili ya chakula, aliendelea kubuni mawazo mbalimbali kwani hakutaka kukata tamaa mapema akijua siku moja isiyokuwa na jina atafanikiwa.
 
Back
Top Bottom