SoC02 Wabunifu wengi hawana vyeti ila wanavipaji ambavyo havithaminiwi ndani ya taifa lao (06)

Stories of Change - 2022 Competition

Kingambe

Member
Sep 2, 2022
10
9
Utatuzi wao wa hili tatizo ni kuwatumia wananchi sms za kutoa taarifa za utapeli. Binafsi nimechoka kutuma hizo taarifa ambazo hazina mrejesho wowote.

Ila bwana Kingambe, anaubunifu wake ambao ni kiboko ya matapeli yaani badala ya wananchi kuogopa matapeli, kwa mfumo wa bwana Kingambe, matapeli ndio watawaogopa wananchi hatimaye utapeli utakwisha kabisa Tanzania.

Mfumo wa bwana Kingambe ni kuwepo kwa chaguo katika menu ya huduma ya kifedha baada ya kuingiza kodi, inayosema tuma pesa kwa tapeli. Huduma hii kabla ya kuanza kutumika, kwanza wananchi waelimishwe vya kutosha jinsi ya kuitumia huduma hii, kwa sababu huduma hii itakuwa na utendaji zaidi na uwajibikaji.

Mteja hatotakiwa kufanya huduma hii mpaka awe amejiridhisha kuhusu utapeli wa mtu aliyemtumia sms au kumpigia simu.

Kwa sababu isijekuwa mtu anafanya utani katika huduma hii kwani mtumiaji wa huduma hii anaweza akawajibishwa endapo ataifanyia utani huduma hii. Mteja anapopigiwa simu au amepokea sms kutoka kwa tapeli na akagundua kuwa huyu ni tapeli. Atatumia huduma ya kutuma pesa kwa tapeli.

Baada ya mteja kutuma pesa hiyo, mteja atatakiwa kutoa ushirikiano baadae kama shahidi namba moja. Pia kwa upande wa yule tapeli atapokea ile pesa na hatoweza kufanya huduma yoyote zaidi ya kwenda kwa wakala na kutoa.

Akitaka kutoa ile pesa kwa wakala, mara ya kwanza ajibiwe mtandao unasumbua jaribu tena baadae, ila kwa wakala apokee ujumbe kuwa huyo mwenye namba ........3153750 jina Juma Kingambe, anatuhumiwa kuwa ni tapeli tafadhali chukua hatua unazoziweza.

Kama serikali ikiamua kuanzisha kampeni maalumu ya teketeza utapeli wa kutumia simu Tanzania, wanaweza wakaweka utaratibu wa polisi jamii ndani ya kila mtaa. Mawakala wote wakahitajika kuwa na namba zao.

Kunapotokea mteja wa aina hiyo wakala apige simu kama vile anahitaji pesa kutoka kwa wakala mkuu.

Wakala mkuu huyo bandia ambaye ni polisi jamii, baada ya kupokea taarifa hiyo aje haraka na kumkamata mtuhumiwa. Na mfumo utatengenezwa kwa namna ambayo wakala ambaye atapokea ujumbe kutoka kwa huyo tapeli alipotaka kutoa pesa na asiufanyie kazi, basi atawajibishwa.

Bila kusahau, baada ya mteja kutoa taarifa na mtuhumiwa kukamatwa, mteja husika atatakiwa kutoa ushahidi endapo atahitajika.

Hatua nyingine baada ya kila tapeli kukamatwa na kuwajibishwa, mmiliki wa kitambulisho alichosajilia kama si yeye mwenye naye uangaliwe utaratibu wa nini cha kufanya dhidi yake. Bwana Kingambe anaamini kwa mfumo huo utapeli unatoweka mara moja. Kwa sasa bwana Kingambe hatumi tena bunifu zake kwenye mabenki au mitandao ya simu.

Atakachokifanya ni kushirikiana na mwekezaji yeyote atakayetokea mwaka wowote waanzishe mtandao wao ambao hautakuwa na changamoto kama zilivyo sasa katika mitandao yetu.

Baada ya hapo, bwana Kingambe ataendelea kufanya bunifu mbalimbali ila hatotuma tena katika mabenki au mitandao ya simu mpaka atokee muwekezaji, au mwenyewe atakapopata mtaji wa kuanzisha kampuni zake.

Bwana Kingambe akahamia katika ubunifu wa programu katika simu (android application). Programu hizo ni niulize mimi (ask me) kwaajili ya uratibu wa mambo ya utalii nchini ikiunganisha watalii, makampuni ya watalii, mahoteli makubwa, dereva wa taxi endapo watataka kutembea nje na utalii wao.

Hii itawasaidia watalii kuifahamu hoteli watakayofikia na kulipia huduma zote hukohuko walipo. Hii pia itasaidia kupunguza hatari ya wizi wa pesa kwa watalii hao kwa sababu matumizi makubwa watakuwa tayari wameyafanya hivyo cash watakayotembeanayo itakuwa ni kiasi kidogo mno.

Pia kwenye application hiyo, kutakuwa na matangazo ya hoteli bora ndani ya nchi husika, pia aina ya vivutio ndani ya nchi husika pamoja na gharama zake. Hii itasaidia pia katika kukusanya huduma tofautitofauti kwa pamoja badala ya kila kampuni kutumia website yake kitu ambacho kwa mteja inaweza kumpotezea muda kupata huduma aina tatu zinazotegemeana mfano, kuangalia vivutio na kuchagua nchi ya kwenda, pia hoteli ya kufikia pamoja na kampuni ya kupokea watalii ndani ya nchi husika.

Pia bwana Kingambe aliifikiria programu ya simu iitwayo safari njema (safe journey) application ambayo ingeisaidia dunia kuhusu usalama wa watoto na hata watu wazima wakati wa kusafiri kwa wale wanaosafiri lakini pia na hata usalama wa wale wanaoachwa nyumbani.

Katika programu hii lengu kuu likiwa ni usalama wa wananchi hasa watoto pia ni kukata tiketi mtandaoni. Katika programu hii kutakuwa na audio mbalimbali ambazo zitakuwa kama ushauri kwa mtumiaji kuhakikisha watu wanaendelea kubaki salama kila siku. Mfano ili kuifanya programu ifanye vizuri katika utendaji wake lazima kuna maswali mengi sana mtumiaji wa hiyo application ataulizwa.

Kutokana na maswali kuwa mengi sana katika application, maswali yatakuwa yanaulizwa awamu kwa awamu kila baada ya siku kadhaa mpaka maswali yatakapokwisha. Mfano wa maswali hayo ni kama. Jiko lako lipo ndani ya nyumba ya kulala au hapana ? Je, mnaishi watu wazima wangapi ndani ya nyumba ? Je, mnafuga mbwa? Je, un16na mfanyakazi wa ndani ? Je, unamiliki siraha ya moto ?

Je, unamiliki silaha za jadi kama mkuki, panga na mishale ? Je, unaishi karibu na pori hatarishi lenye nyoka, wanyama wakali au wadudu hatari ? Je, unaishi karibu na barabara kubwa na bodaboda na gari zinasumbua ? Je, kuna vijana wahuni karibu na nyumba yako ? Na maswali mengine mengi.

Lengo la hayo maswali ni kumkumbusha mtumiaji wa application hii dhidi ya ulinzi wa familia. Katika application kutakuwa na mode mbalimbali ambazo mtumiaji atatakiwa kuiambia application ili iweze kumkumbusha mambo muhimu. Mfano, mtu akitaka kutoka nyumbani atabonyeza kitufe cha natoka nyumbani, kisha application itamshauri baadhi ya vitu.

Mfano kama ana watoto itamuuliza, watoto unawaacha na nani ? Kutakuwa na chaguo la baba/mama au msichana wa kazi au ndugu mwingine au watoto wenzao. Pia kama ulikuwa umesema una mbwa wakali, au silaha utakumbushwa tahadhari juu ya hatari hizo unapoondoka.

Vilevile programu hiyo itawasaidia pia wasafiri, kusimamia safari zao kama vile kupima mwendokasi wa chombo cha moto wakati wa kusafiri.

Endapo mwendo kasi ni mkubwa yenyewe itakuwa inapiga alarm kuashiria mwendokasi unaotumika ndani ya chombo hiko cha moto si salama hata kidogo hivyo endapo atakuwa amelala ataamshwa na alarm ya simu.

Ila kama yupo macho atakuwa anashuhudia mwendo wa chombo chake cha moto. Pia kutakuwa na huduma ya nisindikize (escort me).

Hii ni huduma ambayo itakuwa inampa mtu fursa ya kutumiwa taarifa muhimu na abiria akiwa safarini wakati msindikizaji akiwa nyumbani.
 
Back
Top Bottom