SoC02 Wabunifu wengi hawana vyeti ila wanavipaji ambavyo havithaminiwi ndani ya taifa lao. (03)

Stories of Change - 2022 Competition

Kingambe

Member
Sep 2, 2022
10
9
Wazo hili lilimjia bwana Kingambe pale alipoona wizi mwingi unatokea pale ambapo, watu wa karibu wanapofahamu namba za siri za ndugu au rafiki zao. Mfumo huu pia, unaondoa hatari ya mwenye pesa ambayo hana matumizinayo kwa wakati huo, ahifadhi pesa zake katika vocha atakayopewa benki au katika ofisi za mitandao ya simu. Pesa yake itatunzwa katika akaunti yake kama condition na si pesa kama pesa.

Hii itaifanya akaunti yake kusoma salio la Tshs 0/= ili kumkatisha tamaa mwizi atakapoiba kadi ya ATM au laini ya simu. Hata akitaka kutoa pesa na akapatia namba ya siri, bado hatoweza kutoa chochote kwa sababu salio halitokuwepo ingawa salio limehifadhiwa katika condition ya hesabu. Ili ufanikiwe kutoa pesa, utalazimika kuingiza tarakimu 4 za vocha, kisha ufanye huduma ya kifedha unayoitaka.

Mara baada ya kumaliza kufanya huduma ile, mfumo utalibadilisha salio lako kuwa Tshs 0/= ambapo akaunti yako itakuwa wakati wote inasoma salio Tshs 0/= (zero balance) hata uwe na pesa kiasi gani. Pia watu wanaweza wakajiuliza, kwa vocha ya tarakimu 4 watu si watawaibia wenye mitandao ya simu au benki pesa ? Jibu ni hapana. Na si tarakimu nne tu, hata kwa tarakimu moja jambo hili linawezekana, isipokuwa kwa tarakimu 1 bado mteja atakuwa katika hatari ya kuibiwa kwa sababu tarakimu moja mtu kubahatisha ni rahisi sana.

Kila mteja katika akaunti yake, kutakuwa na variable "a" ambayo baada ya kutengenezwa akaunti yake kwa mara ya kwanza "a" atapewa thamani ya "0" . Hii ikimaanisha bado hajaongeza salio katika akaunti yake.

Atakapokwenda kwa wakala kuweka pesa ile variable "a" itabadilishwa na kuwekwa namba fulani zilizopo ndani ya ile vyocha na mfumo. Baada ya hapo mteja atakuwahuru kuongeza salio wakati wowote na kufanya huduma yoyote, mpaka pesa itakapokwisha, ile variable "a" itarudi kuwa 0. Ikumbukwe kuwa mteja yeyote ili aweze kufanya huduma yoyote ya kifedha, lazima aingize vocha sahihi na namba ya siri sahihi. Kimojawapo kinapokuwa si sahihi, kwa mara ya kwanza tu mteja anaweza akazuiwa kutumia ile akaunti kwa muda flani ambao utapangwa na kampuni ya fedha husika.

Kabla mitandao yote nchini kuwaza wazo la huduma ya mteja kujirudishia muamala mwenyewe tayari bwana Kingambe alikuwa amelifikiria hilo kwa makini na kwa ufanisi wa hali ya juu. Na ufanisi wake ni tofauti na ule ambao uliopo kwa sasa kwa mitandao yetu ya Tanzania.

Utakuta mteja anakosea kutuma pesa halafu, anajaribu kurudisha au kuzuia muamala mtandao hakuna. Ikitokea upande wa mtumiwaji sio mwaminifu pia mtandao upo vizuri anatoa pesa na huduma ya kurudisha au kuzuia muamala inakuwa haijamsaidia. Unapobuni huduma, hakikisha unafikiria mbali zaidi.

Mazingira ya mtandao (network) ni changamoto kubwa sana katika maeneo mengi nchini hasa vijijini. Pia, unapobuni huduma ni vyema kuangalia wale unaowatengenezea huduma hiyo itawasaidia vipi.

Mfano, kuna kampuni moja ya simu imeweka gharama ya kurudisha miamala. Hii inamnyima fursa mteja ambaye baada ya kutuma pesa na kukosea akaunti yake ikiwa haina pesa, mteja atashindwa kuzuia muamala huo. Ila kwa bwana Kingambe wazo lake halikuwa la kawaida. Alikuwa amewaza mambo mengi sana kumhusu mteja.

Alijua kama kuna changamoto nyingi kuhusu mtandao nchi nzima. Pia changamoto ya simu kuzima chaji. Akaona ni lazima kuwe na ucheleweshwaji wa makusudi katika mfumo pale mteja anapotaka kutoa pesa, kama muda wa kutoa (automatic delay) haujafika. Huu utakuwa ni utaratibu wa kila mtandao wa simu katika mfumo wao. Mteja anapopokea pesa atalazimika kusubiri dakika 10 au 20 ndio apate ruhusa ya kutoa.

Ila kila anapojaribu kutoa mfumo utamjibu majibu yaliyopangiliwa katika programu kama vile tafadhali subiri, ombi lako linafanyiwa kazi na kadhalika. Ila kwa mteja ambaye katika akaunti yake hakuna pesa aliyotumiwa ndani ya dakika ishirini zilizopita, huyu ataweza kutoa pesa bila kucheleweshwa na programu. Au kwa mteja atakayetoa pesa kiwango ambacho hakitaijumuisha ile pesa iliyotumwa kwa muda ule atafanikiwa kutoa muda uleule.

Mfano, endapo mteja atapokea kiasi cha Tshs 100,000/= na akaunti yake ilikuwa na Tshs 200,000/= kabla ya kupokea ile laki moja, na kufanya jumla ya kiasi cha Tshs 300,000/=. Mteja atakapotoa kiwango chochote kuanzia Tshs 1,000/= hadi Tshs 200,000/= huku gharama ya makato ikujumlishwa humohumo atafanikiwa kutoa muda uleule. Ila endapo atajaribu kutoa zaidi ya Tshs 200,000/= hatofanikiwa kutoa hadi baada ya dakika 10 au 20.

Lengo kuu la kufanya hivyo ni kumpa fursa mtumaji aweze kurejesha muamala au kusitisha muamala kipindi ambacho mpokeaji bado hajaitoa ile pesa. Vilevile katika muda huo wa kucheleweshwa mtoaji na programu kuna sms ambazo atatumiwa mtumaji ili kujiridhisha kama aliyemtumia ni mtu sahihi au la. Kama si mtu sahihi aweze kuirudisha pesa yake kabla haijatolewa.

Pia changamoto nyingine ni kwamba, kwa mfumo wa sasa, baada ya masaa 24 huwezi tena kurudisha au kuzuia muamala wakati ni jambo ambalo si sahihi kwa sababu, yawezekana ndani ya masaa 24 yule mteja aliyetumiwa akawa bado hajaitoa ile pesa. Moja kutokana na uaminifu wake. Mbili kutokana na changamoto za mtandao sms ya kupokea pesa kutoingia katika simu. Tatu, simu kutokuwa hewani kabisa.

Kwa mfumo ambao aliupendekeza bwana Kingambe, mteja aweze kurudisha pesa pesa yake aliyoituma kwa makosa muda wowote. Pia hatakama pesa imetolewa basi yule mteja aliyeitoa ile pesa, katika mfumo kwenye akaunti yake awekewe deni, ili atakapoingiza pesa siku yoyote na mwaka wowote endapo usajiri wa laini hiyo haujabadilishwa basi pesa aliyoiba ikatwe na kurudishwa kwa mwenyewe.

Baada ya mfumo wake kuzingatia mambo kama hayo ya msingi, akatuma proposal zake kwenye mitandao yote Tanzania ila hakupata majibu yoyote na badala yake, mitandao ya simu ikaja na huduma hiyo kwa namna ambayo bwana Kingambe anaona bado ni changamoto kwa wateja.
 
Back
Top Bottom