SoC02 Wabunifu wengi hawana vyeti ila wana vipaji ambavyo havithaminiwi ndani ya taifa lao. (04)

Stories of Change - 2022 Competition

Kingambe

Member
Sep 2, 2022
10
9
Bado hakuchoka, bwana Kingambe aliendelea kupambana katika kutafuta maisha. Hakusahau kuhusu mambo ya ubunifu.

Akaja na jambo la ajabu zaidi la vocha zenye tarakimu 4. Hili aliliwaza baada ya kuona tarakimu za vocha ni nyingi sana kwa mteja, pia ni rahisi sana kukosea. Katika mfumo wa vocha zenye tarakimu 4 ni lazima mfumo huu uendane sambamba na ulinzi wa vocha hizo ili mteja asije akafanikiwa kuingiza vocha bila kununua.

Bwana Kingambe alilijua hili ndio maana akaanzisha huduma hii ikiwa inamtegemea muuzaji wa zile vocha aweze kuingiza namba ya simu ya mnunuzi wa ile vocha. Baada ya kuingiza namba ya simu ya mnunuzi pia atatakiwa kuingiza namba zenye tarakimu nne kisha baada ya hapo, atamkabidhi vocha mteja wake.

Vocha ile itatumika kwenye namba ile tu, mtu mwingine ambaye hajanunua vocha akiingiza itakataa kuingia. Pia hii itasaidia wateja kuhifadhi muda wa maongezi katika akaunti zao ili usitumiwe na watu wengine hovyo, kwani ataiweka ile vocha pale tu atakapotaka kuutumia. Kama hana matumizi na muda wa maongezi basi hatoweka vocha ile.

Hii pia itasaidia kutatua ile changamoto ya salio la mtu kutumika katika huduma mbalimbali ambazo mteja hajajiunganazo kama ilivyo sasa. Utakuta mteja ameweka salio, baada ya muda salio linapungua. Akipiga simu huduma kwa wateja anaambiwa kuna huduma amejiunga wakati katika kumbukumbu za mteja hajawahi kujiunga na huduma yoyote.

Ukiacha ubunifu huo, bwana Kingambe akaja na ubunifu wa kupunguza namba katika namba za akaunti za benki kuanzia tarakimu 1 hadi tarakimu 6 na herufi 2. Mwanzoni mwa namba za akaunti herufi moja na mwishoni moja.

Mfano, A000000A ni namba za akaunti mojawapo ya benki yenye tarakimu 6. Pia A0A ni akaunti mojawapo pia yenye tarakimu moja. Hizo ni namba za akaunti mbili tofauti. Kwa akaunti za namna hiyo zinafikia idadi ya akaunti tofautitofauti 115,555,544.

Kati ya akaunti hizo, idadi ya akaunti zenye tarakimu 1 ni 104. Akauniti zenye tarakimu mbili ni 10400. Akaunti zenye tarakimu tatu ni 104000. Akaunti zenye tarakimu nne ni 1,040,000. Akaunti zenye tarakimu tano ni 10,400,000. Akaunti zenye tarakimu sita ni milioni 104. Katika mfumo huu akaunti A0A ni tofauti na akaunti A00A.

Hii ikimaanisha idadi ya tarakimu katika akaunti pia inatofautisha akaunti moja na nyingine. Hizi akaunti ni msaada mkubwa kwa wateja wa benki na wale wahudumu wa benki muda wa wateja kuweka pesa zao. Kwa mteja ni rahisi kuandika namba chache, pia kwa teller inamsaidia pia kuokoa muda wa wateja kusubiri kuhudumiwa katika foleni.

Ikiwa inachukua sekunde 1 kwa mteja kuandika kila namba katika akaunti yake, kwa akaunti za sasa zenye tarakimu 15 mteja atatumia sekunde 15 katika kuiandika akaunti hiyo, vivyohivyo kwa teller naye atatumia sekunde 15. Hii inakadiria kwa makadirio ya chini mteja mmoja atahudumiwa ndani ya sekunde 30.

Lakini kwa akaunti yenye tarakimu moja, mteja atatumia sekunde 3 na teller sekunde 3 jumla sekunde 6. Ndani ya sekunde 30 zilezile watahudumiwa wateja 5 zaidi ya mfumo wa akaunti za sasa. Faida ya akaunti zilizopunguzwa ni kutumiwa na taasisi mbalimbali ambazo watu wengi wanalipia huduma katika taasisi hiyo kupitia benki.

Mfano wa taasisi hizo ni kama mashule, vyuo na taasisi mbalimbali ikiwemo taasisi binfsi na za serikali. Hii itasaidia watu wakati wa kulipia huduma benki. Kumbuka urefu wa akaunti za wateja utabaki uleule isipokuwa, urefu ule utaendelea kubaki ndani ya programu, ila kwa mteja hana haja ya kupewa akaunti yenye namba nyingi.

Mteja atapewa namba za akaunti chache kama utambulisho wake katika programu, ila programu itafanyakazi ya kuitafuta akaunti ndefu baada ya kuingiza akaunti fupi. Mfumo huu, hautabadili chochote katika mfumo uliopo zaidi ya kuongeza akaunti hizi fupi.

Mteja atakuwa na namba za akaunti 2 zikitumiwa na mteja mmoja, akaunti ndefu na fupi. Yoyote akitumia ni sawa. Sio hivyo tu, bwana Kingambe akaandaa pia namba za simu zilizopunguzwa kutoka tarakimu 10 hadi tarakimu 1 hadi 6.

Jumla ya namba za simu 1,000,000 namba za simu zilizopunguzwa. Hizi zitatumika wakati wa kuweka pesa na kutoa pesa. Lengo ni kurahisisha kazi kati ya mteja na wakala wakati wa kuweka pesa.

Pia hii itasaidia kuficha namba halisi ya mteja kwa wakala ambao si waaminifu. Kwa sababu namba yake halisi haitaonekana katika sms ya muamala wowote zaidi ya jina na ile namba iliyopunguzwa.

Hii itazuia mawakala kuzitumia namba za watu hovyo kama vile kuwapigia wake za watu na kuharibu ndoa za watu, pia kutumika katika utapeli. Pia namba hizo hutoweza kuzipigia wala kuzitumia sms. Zenyewe ni kwaajili ya kuwekea pesa tu.

Akaandaa tena proposal na kuituma katika benki zote na mitandao yote ya simu Tanzania bila kujibiwa chochote.

Bwana Kingambe bado hakuchoka. Aliamua kuandaa mfumo ambao utamsaidia kila mteja kutoa pesa kwa wakala yeyote. Kwa mfumo huu, ni lazima kila mteja awe na laini zaidi ya moja ili aweze kutoa pesa kwa wakala.

Pili mteja atatakiwa kununua vocha ambayo itakuwa inauzwa katika maduka ya mitandao. Vocha ile, itakuwa na namba ambazo wahudumu katika maduka ya mitandao wataziingiza katika mfumo. Baada ya kufanya hivyo mteja atapewa ile vocha.

Na pale atakapotaka kutoa pesa anaenda kwanza kwa wakala. Kama ni wakala wa mtandao fulani ataingiza ile vocha katika laini ya mtandao ule na kutoa pesa. Katika mfumo kutakuwa na mahesabu ya programu ili kufahamu vocha ile imenunuliwa kutoka mtandao gani na imetumika ndani ya mtandao gani.
 
Back
Top Bottom