SoC02 Wabunifu wengi hawana vyeti ila wana vipaji ambavyo havithaminiwi ndani ya taifa lao - (02)

Stories of Change - 2022 Competition

Kingambe

Member
Sep 2, 2022
10
9
Kuna bunifu mbalimbali ambazo aliziandaa kabla hata ya kufeli chuo. Hizi zilikuwa ni programu katika kompyuta ambazo aliziandaa katika programu iitwayo MATLAB. Programu hizo ni daftari la mahudhurio (school attendance), sign win (weka saini ushinde), programu ya kufanya maswali ya hesabu ya mafumbo hatua kwa hatua (mathematics words problem solver) kwaajili ya kuwasaidia wanafunzi kujifunza hesabu hata mwalimu asipokuwepo na vitabu vya sayansi ndani ya programu (programed science books).

Daftari la mahudhurio, ni mfumo ambao ungeweza kurahisisha mawasiliano kati ya mzazi na mwalimu. Mfumo ambao ungeweza kuwapa taarifa wazazi, wote wenye simu kubwa (smart phones) na viswaswadu (button phones) Kuhusu mahudhurio ya watoto wao. Hii ingewasaidia wazazi kupata taarifa za awali kuhusu mahudhurio ya watoto wao popote walipo nchini (kwa wenye simu ndogo), ila wenye smart phones popote duniani waweze kupata taarifa. Si hayo tu ni mambo mengi ambayo yangewezakufanyika ndani ya mfumo wa daftari la mahudhurio.

Pia katika mfumo wa saini ushinde (sign win), huu ulikuwa ni mfumo wa wafanyakazi wote duniani katika kusaini waingiapo kazini na muda wa kuondoka. Sio hivyo tu, kila siku mfanyakazi atakayesaini mapema zaidi ya wengine apewe zawadi kama pongezi ya kuwahi kazini.

Hii ni mifumo ambayo bwana Kingambe alikuwa akiibuni huku akiendelea kulima na kuchoma mkaa. Ingawa wapo wengi waliopitia changamoto kama zake wakaamua kujinyonga, ila yeye aliendelea kumuomba MWENYEZIMUNGU aendelee kumsimamia japo hakuwa na msaada wowote kutoka kwa yeyote bado hakukata tamaa.

Alikuwa na programu yake katika kompyuta, ya kufanya maswali ya hesabu ya mafumbo hatua kwa hatua. Kipindi bado yupo chuoni alitumia muda mwingi katika kuiandaa hii programu. Mwanzoni aliamua kuifanya hii programu imsaidie mwanafunzi katika maswali ya mafumbo ya umri peke yake. Programu ilifanikiwa kufanya maswali ya mafumbo hatua kwa hatua huku mwanafunzi akiwa anapewa maelezo ya kutosha kuhusu ufafanuzi wa swali.

Programu hii ni tofauti na kikokotoo (calculator) ambayo yenyewe inafanya matendo ya moja kwa moja ya kuzidisha, kutoa, kugawanya na kujumlisha. Ila programu ya bwana Kingambe yenyewe inapokea maelezo yote ya swali kisha inafanya michakato ya kufahamu swali linataka nini, kisha inaanza kutoa majibu huku ikitoa maelekezo ya kwanini imefanya hivyo hilo swali na si vingine. Baadae akaona ni vizuri kuandaa kitabu kizima cha hesabu kuanzia shule za msingi hadi kidato cha nne. Vyenyewe vikiwa ni vitabu vya programu vyenye kufuata mtaala lakini vyenyewe tofauti na vitabu vya sasa.

Vitabu hivi vitampatia mwanafunzi notes ila katika kila mada kutakuwa na programu ambayo itamsaidia kufanya swali lolote litakalomshinda. Hii ndio tofauti kubwa kati ya vitabu vya kawaida vya hesabu. Pia anamawazo pia ya kutengeneza vitabu vya kemia, baiolojia na fizikia kwa namna hiyohiyo.

Kwa kutumia programu ya MATLAB pekee, haikuwa rahisi kutengeneza programu hizo za vitabu. Ila bwana Kingambe akaamua kuiweka kiporo na kuendelea na programu nyingine. Alikuja na wazo la kupunguza idadi ya namba katika tokeni za luku na vocha kwaajili ya kuongeza pesa katika akaunti za wateja wa simu au benki.

Punguzo la namba katika tokeni za luku, ni wazo aliloliwaza bwana Kingambe ili kumrahisishia mteja wakati wa kuweka umeme katika luku yake. Kwa wazo lake, idadi ya tokeni za luku iwe ni namba moja tu inatosha.

Unaweza ukajiuliza maswali mengi. Moja, je, hii inawezekanaje ? Mbili, watumiaji wa luku si wanaweza wakaiba umeme bila kufanya malipo kwa sababu mteja anaweza akabahatisha namba, kwa sababu namba zenye tarakimu moja ni kumi tu. 0, 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8 na 9. Jibu ni hapana. Mteja hawezi kuiba umeme kwani huduma ya luku ni prepaid (malipo kwanza kabla ya matumizi).

Kitakachofanyika, kwa wale waliosoma mambo ya proramming, kutakuwa na variable katika kila akaunti ya mteja wa umeme, variable ambayo, wakati mteja anatengenezewa akaunti hiyo ile variable itawekwa thamani ya sifuri ikimaanisha mteja hajanunua umeme bado, kimahesabu ya programu (int a=0) na atakaponunua umeme ile variable itakuwa 1 kwa kanuni ya kimahesabu ya programu (a=a+1).

Baada ya mteja kununua luku, zile idadi ya namba za tokeni, zitahifadhiwa ndani ya programu kwani mteja haina haja ya kumtumia namba nyingi akahangaikanazo kuziingiza katika luku yake, wakati programu zipo za kurahisisha kazi. Hapa mteja anapoingiza tarakimu yoyote 0 hadi 9 mfumo utaangalia thamani ya "a" kwanza kabla ya kuruhusu zile tarakimu za luku kufanya kazi na umeme kuingia.

Moja, kama thamani ya "a" ni 0 katika programu ((if a==0) {cout<<"haujanunua luku, tafadhali nenda kanunue luku na ujaribu tena baadae"<<endl;}) mteja hatoweza kufanikiwa kuingiza umeme kama hajanunua umeme.

Mbili, kama thamani ya "a" ni 1, baada ya mteja kuingiza tarakimu yoyote kuanzia 1 hadi 9, programu itaruhusu zile tarakimu za luku kufanya kazi. Pia ni lazima thamani ya "a" katika programu ibadilike (a=a-1) ili kuirudisha kwenye "0" ikimaanisha mteja hajanunua umeme bado, na endapo mteja atataka kuingiza tena umeme hatoweza kwa sababu thamani ya "a" imerudi kuwa sifuri, hivyo atalazimika kununua umeme ili thamani ya "a" ibadilishwe kuwa 1 na programu yenyewe.

Alitengeneza programu katika programu ya kompyuta ya MATLABU na akaendanayo TANESCO lakini hakupata ushirikiano wowote na kuamua kuachana na hilo na kuhamia katika vocha za kuongeza pesa katika akaunti za simu na akaunti za benki, kama vocha za kawaida za kuongeza muda wa maongezi.
 
Serikali inahitaji kutoa sapoti na power kwa wabunifu wa ndani.
Refer to this thread

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom