Mie nipo hapa Dodoma,
Tangu waheshimiwa Wabunge waanze kuja Dodoma kwa kikao cha Bunge la Bajeti, kumekuwepo na ongezeko kubwa la mashangingi hasa nyakati za jioni kuja hapa chuo kikuu cha Dodoma na kuwachukua watoto na kuondoka nao. Wabunge wanawatuma madereva tu, wao hawaonekani!
Je hii ndo kazi ambayo wametumwa na wapiga kura wao? Na je kwanini wanawaharibia maisha watoto wa watu wakati wao wameoa na kuwa na familia zao? Kama wanahusudu sana Ngono kwanini wasije na wake zao?
Nawakilisha wadau!!!
Hali halisi ya maish ya jiji la Dodoma na uwepo wa mikutano ya wabunge dodoma kwa mang'amuzi yangu imepelekea wengi hasa dada zetu kugeuza hali hiyo kama kitega uchumi kutokana na hali halisi ya maisha ya Dodoma kiuchumi yalivyo. Yameongelewa miaka mingi tu na sasa ni mabadiliko ya mtandao wa zama hizo kwenda zama za leo.
Siku za nyuma kabla ya vyuo vikuu kuanzishwa Dodoma, machangudo walikuwa na pato la hakika kipindi cha mikusanyiko ya wabunge. Bunge linapoanza malaya walifurikia Dodoma na bunge linapositishwa malaya walirudi kwenye himaya zenye wateja wao kwenye miji yenye wapita njia na wenye pesa wengi. Siyo siri wabunge wengi wamepukutika na kubaki tu historia yao kutokana na huba walilotekwa na machangudoa bila kujua malipo kwa hao ilikuwa ni kununua sanda na kuacha wajane na watoto yatima.
Baada ya semina elekezi juu ya elimu ya ukimwi makazini, maofisini nk, na uanzishwaji wa vyuo vikuu nchini, Dodoma ikapata kipa umbele kupanua wigo wa elimu kwa kuwa na vyuo vinavyozunguka himaya ya makao makuu ya serikiali Dodoma. Vyuo hivyo sasa vimegeuzwa bustani ya waheshimiwa wabunge wasio na haya ya kujali heshima ya familia zao, future za wanafunzi wa vyuo vikuu vivilivyo kando ya "ALEOPAGO" (
aleopago ni neno la kiyunani likimaanisha kilima walipokuwa wanakutana wanafalsafa kama Sokrates kujadili falsafa) ya wabunge Dodoma. Ni dhahiri hali ya maisha kuwa ngumu kwa wanafunzi, na mitandao kadhaa inayotumiwa siku hizi ikiwemo mitandao ya internet ni njia rahisi ya kuwanasa wanavyuo wa Dodoma. Jana na Leo hali hiyo imemtokea mbunge wa Marekani aliyezoea kufanya oral sex na mwanachuo wa miaka 21 mtandaoni kulipuliwa na ameomba radhi wananchi na serikali, leo iko hadharani. Hayo yanaweza watokea Waheshimiwa wabunge Dodoma. Baya zaidi mambo hayo yanavyofanyika kwa usiri huwezi kuwa na hakika kama wanajihakikishiaje usalama kiafya.
Niliwahi kusimamishwa mara fulani Dodoma majira ya saa 12 jioni dada kadhaa wanaranda barabarani na kusubiri kuchukuliwa na magari, nilifikiri mwanafunzi katoka chuo anaomba msaada kuwahi home, rafiki yangu mwenyeji wa dodoma kaning'ata sikio kwamba ni mtafutaji, waheshimiwa huwapitia hapa, na wanafikiri we ni mmoja wa waheshimiwa. Hakika hatari kwa watoto, na mbaya kuwaharibia future yao, maana sasa badala ya kutulia kwa ajili ya mitihani ya kufunga mwaka wako na harakati za kuwatuliza waheshimiwa walioko kwenye bunge la bajeti. Waheshimiwa wasiooa na kuolewa tafadhalini tafuteni soulmate wenu for good, msije mwambukiza madudu ndugu yangu.