Wabunge wetu na mabinti wa vyuo!

Sinai

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
288
47
Mie nipo hapa Dodoma,

Tangu waheshimiwa Wabunge waanze kuja Dodoma kwa kikao cha Bunge la Bajeti, kumekuwepo na ongezeko kubwa la mashangingi hasa nyakati za jioni kuja hapa chuo kikuu cha Dodoma na kuwachukua watoto na kuondoka nao. Wabunge wanawatuma madereva tu, wao hawaonekani!

Je hii ndo kazi ambayo wametumwa na wapiga kura wao? Na je kwanini wanawaharibia maisha watoto wa watu wakati wao wameoa na kuwa na familia zao? Kama wanahusudu sana Ngono kwanini wasije na wake zao?

Nawakilisha wadau!!!
 
Kaka una ushahidi? unajua hizi tuhuma ni nzito, au ni ile kauli ya JK kwamba jamaa wapunguze ngono.

Kama ni kweli ndio sababu posho zao hazitoshi, Wakiambiwa wapunguze wanakuwa wakali kama mbogo.
 
Hao mabinti wanapewa fedha kidogo za mikopo ambayo ni kama Tsh.5,000 kwa siku kwa ajili ya chakula na malazi na wabunge wamekataa kuwapigania waongezewe mikopo. Wabunge wao wanapewa fedha nyingi zaidi Tsh.100,000 kwa siku na wabunge nao hawataki posho zao zipunguzwe.

Kwa hiyo kinachofanyika ni kuwa wanafunzi wanajiongezea posho zao za siku kwa njia hiyo na wabunge wanajipunguzia posho zao za siku kwa njia hiyo. Hapo panaeleweka?
 
Mie nipo hapa Dodoma,

Tangu waheshimiwa Wabunge waanze kuja Dodoma kwa kikao cha Bunge la Bajeti, kumekuwepo na ongezeko kubwa la mashangingi hasa nyakati za jioni kuja hapa chuo kikuu cha Dodoma na kuwachukua watoto na kuondoka nao. Wabunge wanawatuma madereva tu, wao hawaonekani!

Je hii ndo kazi ambayo wametumwa na wapiga kura wao? Na je kwanini wanawaharibia maisha watoto wa watu wakati wao wameoa na kuwa na familia zao? Kama wanahusudu sana Ngono kwanini wasije na wake zao?

Nawakilisha wadau!!!
Mkuu huenda hao madereva wanajichukulia wenyewe.
Lakini kama wabunge wamesahau majukumu yao wakaanza kuwashughulikia hao mabinti nadhani muheshimiwa JK anapaswa awape semina elekezi.
 
Hao mabinti wanapewa fedha kidogo za mikopo ambayo ni kama Tsh.5,000 kwa siku kwa ajili ya chakula na malazi na wabunge wamekataa kuwapigania waongezewe mikopo. Wabunge wao wanapewa fedha nyingi zaidi Tsh.100,000 kwa siku na wabunge nao hawataki posho zao zipunguzwe.

Kwa hiyo kinachofanyika ni kuwa wanafunzi wanajiongezea posho zao za siku kwa njia hiyo na wabunge wanajipunguzia posho zao za siku kwa njia hiyo. Hapo panaeleweka?

Ni kweli...Lakini kwa mtindo unaoendelea Dodoma tujiandae kuzika vijana wa kiume wasio na hatia!!! kwani hao Mabinti watajaolewa na Wakaka ambao hawajui maisha walioyapitia huko nyuma... Kina dada hao wajirekebishe...
 
KAZI NA DAWA
Wanatoa huduma nje ya bunge.
na hao wabunge wa kike vipi? wao hawataki wanafunzi wa kiume?
 
Enzi nasoma UDSM, kuna Waziri Mwandamizi alikua anakuja mwenyewe pale Hall 7...nadhani yule dada alihamia Mabibo Hostel au alikua na kimwana mwingine tena, coz kuna siku waziri huyo alibananishwa na Auxiliary Police wa pale usiku kwa kuzidisha muda wa kukaa na gari yake ndani wakati ni mgeni...
 
kweli bwana hawajamaaa wana madalali wao kabisa hali ni mbaya na saizi ndio mwisho wa semester watoto wanadhalilishwa kwa sababu hawana pesa za kujikimu,ni vyuo vyote dom
 
Mie nipo hapa Dodoma,

Tangu waheshimiwa Wabunge waanze kuja Dodoma kwa kikao cha Bunge la Bajeti, kumekuwepo na ongezeko kubwa la mashangingi hasa nyakati za jioni kuja hapa chuo kikuu cha Dodoma na kuwachukua watoto na kuondoka nao. Wabunge wanawatuma madereva tu, wao hawaonekani!

Je hii ndo kazi ambayo wametumwa na wapiga kura wao? Na je kwanini wanawaharibia maisha watoto wa watu wakati wao wameoa na kuwa na familia zao? Kama wanahusudu sana Ngono kwanini wasije na wake zao?

Nawakilisha wadau!!!

Ndio maana Mhe Hamad Rashid wa CUF anang'ania wabunge kuwa na madereva hata kama Kanuni za Ajira na Fedha za Serikali hazitambui kama wabunge mi moja ya watumishi wa Serikali wenye stahili hiyo. Ofisi ya Bunge inamiliki idadi kubwa ya mabsi kwa ajili ya kuwasafirisha wabunge kutoka ofisi za bunge na vituo vilivyopangwa lakini kila mmoja anang'ang'ania kupiga moto gari kuja nalo Dodoma kwa ajili ya shughuli kama hizo.
 
Na baada ya hapo wataanza kudai posho ya mafuta wakisingizia kwamba wanaenda kafanya kazi za kijamii. Itabidi uchunguzi ufanyike atakaye naswa aachishwe kazi kwa manufaa ya wananchi.
 
Hao mabinti wako zaidi ya miaka 18 na wanayo haki ya kufurahia maisha watakavyo. Hiyo ndio aina ya maisha waliyoichagua kwa sasa. Kuwa wanafunzi kusiwanyime haki yao ya msingi. kwangu sion tatizo kwa mabinti isipokuwa kwa wabunge ambao wameoa na wanaendeleza ufuska wao
 
Hao wana vyuo wenyewe ndio wenye viranga. Wangetulia saa ngapi wabunge wangewapata; wameshindwa kujua majukumu yao wametanguliza tamaa. Kwani wamelazimishwa???????????? Ispokuwa ni viherehere vyao tu vya kujipendekeza kwa tamaa zao!!!!!!!!!!!!!!!!
 
madada zetu nao wamekuwa rahisi sana!

Lakini hawa si tunawachukulia kwamba ni watu wazima kwa kuwa kwa mfumo wa elimu ya Tanzania watakuwa wameshafikisha miaka 18 na zaidi hivyo wanaweza kujiamulia mambo yao wenyewe? Mi nafikili itakuwa siyo kiherehere chao bali ni utashi. Mwenye masikio na asikie yale yasemwayo na wajoli wa BWANA.
 
Umaskini na ujinga ndiyo unawadhalilisha watoto wa kike. Wabunge nao msiwalaumu wana ganzi kama binadamu wengine, sasa wakikutana na hao watoto wenye njaa ndiyo inapokuwa kizungumkuti.

Pole zao hao watoto, Mungu awatie nguvu maana sasa hivi makaburi yanajaa kila siku. Kila msiba wangetaja chanzo cha kifo basi tungeweka watu tungejifunza sana, aliyekuwa kwa HIV watasingizia kisukari, shinikizo la damu, wengine wanadiriki kusema eti ni vidonda vya tumbo wakati watu tuliomuona akiwa hospitali anaumwa HIV.

Glory be to GOD.
 
Sio viongozi wetu ndio wamekua wazinzi mno???

lakini kumbuka anaetoa huo Uzinzi ni mdada.........wadada wa siku hizi bana sio kama kipindi kile huwezi hangaika nae saaana just one day hata kama hamjawahi kutana nae UNAKULA MZIGO..... Hii ni mbaya sana dada anaangalia tu usafili na mfukoni kuna nini lakini hajui mwilini kuna wadudu gani
 
Back
Top Bottom