mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,664
- 18,040
Kuna wabunge wanatoa mawazo ya hila hadi wanakera!! Ni unafiki mkubwa sana!! Lengo lao ni kutaka kuwapitisha watu wao kwenye ajira ya utumishi wa umma kwa mlango wa nyuma wa "kujitolea". Hii itatesa sana wale watakaoingia kichwa kichwa kujitolea wakati wako nje ya kundi hili la wateule!! Watajitolea miaka nenda rudi na ajira wasipate!! Kuna vijana wengi sana walijitolea hadi wakanyoosha mikono!!
Hawa wabunge tunawataka na wao wajitolee kwenye bunge hili la bajeti!! Wasipate posho wala mshahara!! Zile walizokwisha chukua zihesabike mkopo na wazirejeshe!! Waonyeshe huu uzalendo hadi mwisho wa mwaka, halafu ndio watufundishe utamu wa kujitolea!!
Hawana hata aibu, hebu watuambie huyo anayejitolea atakula nini?, atavaa nini? atatibiwa vipi? hadi siku atakapopata ajira!! Halafu hatuzungumzii kujitolea kwa mwezi mmoja au miwili bali mwaka au miaka!! Hii ni kutumia shida ya mtu kumfanya mtumwa!! HATUTAKI!! Jitoleeni kwanza nyie wabunge na mawaziri kwa mwaka mmoja!!