Wabunge wa CHADEMA waitikisa Singida Mjini

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
Wakuu salaam.

Baada ya kumaliza Kikao Cha Kamati Kuu Mjini Igunga Kazi za ujenzi wa chama zinaendelea.

Wakati Dr Slaa akishambulia Katesh Kamanda Lema,Chiku Abwao na Mimi mwenyewe tutakuwa na mkutano wa hadhara katika viwanja vya stendi ya zamani kuanzia saa 8 mchana. Kabla ya mkutano huu tumebahatika kutembelea na kujionea wenyewe jinsi kina mama na watoto wanavyopata tabu kupata maji.

Tumekutana na msururu wa ndoo, madumu wanawake na watoto wanasubiri maji katika eneo la Mwenge Sekondari.

Miaka 50 tangu Uhuru watu mpaka Leo wanatumia zaidi ya masaa 12 kwa Siku kusubiri maji. Mji wa Singida unahitaji special attention kuhusiana na suala la maji.

Kutoka Bwawa la Singida mjini Singida

Regia Mtema

================
PICHA:

wanataka-mabadiliko.jpg

regialema.jpg

walimu-malalamiko.jpg

watu-singida.jpg

lema-singida.jpg
 
Twangeni kotekote walisema vyama vya msimu kumbe wao sasa ndio wanageuka chama cha msimu.
 
Washeni moto bila kuchoka. Wao wanasubiri kuvuana magamba. Please let us know where are you heading after there. Mbona kamanda wa sheria Lissu hayupo?
 
Mkuu Regia bila shaka ikifika jioni utatupa ripoti ya pima joto inasemaje? Tutataka kujua mwitikio wa watu wa Singida. Je wanajuta kupoteza kura zao mwaka 2010 na kuwapa nafasi wakwapuaji na wasanii kuendelea kuimalizia nchi yetu kabisa na hata kufikia hatua ya kukomba hata ile asali kidogo iliyokuwa imebaki kwenye mizinga ya rasilimali za nchi yetu.

Amsheni fahamu za waliolala wajue hata hilo tatizo la maji ni laana ya kuweka madarakani wezi na wanyonyaji
 
mkuu Regia jana uliahidi kutuwekea fotos imekuwaje??naomba mtimize mnayoahidi
 
Waamsheni wanasingida siku moja nilifikia pale hostel za katoliki kulikuwa na mkutano wa wanamagamba walikuwa na mkutano wao jimbo la singida mjini walikuwa wanafurahia Dewji kuwagawia kila mtu sh. 10,000/- kama nauli na waliandaliwa chakula cha mchana hapo.

Singida mkoa maskini wamefungwa na magamba na kudanganywa kwamba mkichagua chadema mmekwisha.
 
Kazi njema makamanda tunawatakia kila la kheri. Singida bado iko nyuma sana inahitaji uamsho wa kueleweka.
 
Wananchi wa Singida na Dodoma wameishazoea shida, wanaona kama kukosa maji ni haki yao...

Ila nina uhakika 2015 watashangaza magamba, baada ya kuona matunda ya kuwa na kamanda kama Lissu anayeipeperusha vema bendera ya mkoa wao...

Tofauti kati ya Lissu na Nyarandu ni kubwa mno, kama mbingu na dunia vile bt kabla ya kumpata Lissu walikuwa hawayajui hayo...
 
Vizuri kupaza sauti juu ya changamoto na matatizo yanayoikumba jamii kila mnapopata nafasi ya kutembelea wananchi katika maeneo tofauti nchini.

Ushauri wangu; Msiishie kusema shida zao tu bali mtoe na suluhu ya hayo matatizo yao katika njia ambayo itaeleweka hasa kwa mwananchi wa kawaida ili atakae wabeza, wananchi watakua wameelewa ufumbuzi wa matatizo yao uko wapi.

Kwa njia hii mikutano yenu itakua na tija na faraja kwa wananchi mnaowatembelea na mtapata ushirikiano wa kutosha.

Msijikite katika kutoa lawama tu kwa watendaji wa serikali bali kuonyesha njia sahihi itakayo leta ukombozi.

Tumechoshwa na habari za ufisadi na ubadhilifu katika serikali na inavyoelekea hakuna njia ya kuwabana wahusika pindi wanapotajwa ingawa tunafarijika kwa wachache ambao hatua zimechukuliwa ingawa si za kuridhisha sana maana suala la tume nalo limekua kama sehemu ya kufichia hayo madhambi.

Ni maoni yangu tu hayo machache.
 
Makamanda bado tunaomba mwende na Tabora kwenye jimbo la Said Nkumba, Sikonge, huko mavuno yanawasubili kwa hamu, mwisho tunawatakia kila jema katika kuleta ukombozi kwa wana Singida, yawezekana mkakutana na vikwazo lakini kazi yenu ni moja tu, kuwakomboa watu, mengine yatakuja yenyewe.
 
Wakuu,
Leo makamanda wa CHADEMA wanahutubia umati wa wananchi wa Singida mjini. Namuona kamanda Godbles Lema kwa mbali pale,taarifa nilizopata ni kwamba makamanda wengine wanakuja. Picha na taarifa zingine nitawajuza
 
Mabadiliko hayatoki kwa Mungu...watanzania tuna akili sana na tumejaaliwa kujua mema na mabaya..sasa maadam ya miaka 50 yote mabaya tumeyaona ni wajibu wetu kuchukua hatua muafaka sasa na tuwe na mategemeo Mapya yasiyo na ufisadi..

CCM hakuna wa kuaminika hata mmoja..tukisema tusome Albadiri kwa walioibia Taifa NINA UHAKIKA HAKUNA HATA MMOJA ATAKAYETOKA..kidooooooogo magufuli..ILA NAYE KAGANDANA NA MAGAMBA...

Nina hasira mimi mtoto wa watu..naweza tafuna Fisadi.
 
Serikali ya CCM imechoka na imeshindwa kuongoza nchi, kwani wao bado wapo katika kufikiria 10% badala ya kuleta maendeleo katika jamii ya watanzania, kwani hayo yanayoendelea ni mateso kwa watanzania.

Tanzania sio maskini wa hivyo bali ni wa kutengenezwa na kundi la watu wengi kutoka katika chama cha magamba, wenye tamaa ya utajiri na kupinga kila aina ya maendeleo kwa watanzania walio wengi ambao ni maskini. Waelimisheni wananchi kwa maovu yote yanayofanywa na CCM na nini faida ya kupiga kura ya Urais na ubunge kwa chama cha CDM katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Naamini CDM ikiwa chama tawala kero zote hizo zitafanyiwa kazi kwani hakuna kinachoshindikana kwa miaka mitano mnaweza kupiga maendeleo yaliyokuwa yafanywe kwa miaka ishirini. Bila 10% au ufisadi kazi kiuzalendo kuridhika kwa kile unachokipata Tanzania yetu itakuwa hamna mtu anayelia njaa. Vita zaidi zaidi katika katiba mpya iharakishwe kabla uchaguzi kwani hicho ni kikwazo kikubwa cha kuunyima ushindi upinzani.

Na muhimu zaidi wapinzani muondoe tofauti zenu kabla uchaguzi wa mwaka 2015 ili muweze kupiga kura moja ya Urais Nccr na Cuf wasitoe mgombea wa urais nguvu zote zielekezwe kwa mgombea wa CDM na hapo tutaweza anzeni sasa kwani mwende na wakati kabla 2015 mapatano yawepo.

2015 sio mbali kwani nia ni kulikomboa Taifa letu lililoangamia.
 
Napenda kukumbusha Ritz kitu kimoja. Kilichompata Hosni Mubaarak na wanaye angalia kisije kikajirudia hapa TZ, lets wait brother. Hakuna haijuae kesho.
 
Regia umenichesha sana, hiyo ya Bwawa la singida ipo kwenye sera za Chadema au wewe umejisemea tu?

Mbona Dar haijachukuwa maji kutoka Bahari ya Indian maana ni mengi sana lakini bado kuna uhaba wa maji sana jijini Dar es Salaam?

Ebu muulize Mnadhimu wako kuhusu hao maji kabla ya kuyaongelea maana ni mwenyeji wa huko, maana husije ukadhani mambo ni marahisi wakati hujakabidhiwa alafu ukikabidhiwa unaanza kulia na kutoa machoa, kama Nyerere alivyosema anawaonea huruma wanaogombania kukimbia Ikulu wakidhani pana raha!

CCM ina Mpango mzuri sana wa maji ambao upo katika utekereza katika mji wa Singida na tatizo la maji linaweza kuja kuwa Historia baada ya huo mradi unaoendelea sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom