Wabunge ndio maadui Wakwanza wa Maendeleo yetu na wanatunyonya

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,467
23,756
Watanzania. Naomba kwa heshima na Taadhima. Leo hii tufahamu wanaotukwamisha katika maendeleo ni akina nani. Hatuwezi shinda vita vya Umaskini ikiwa Hatujafahamu Maadui zetu ni akina nani.

Tunapaswa pia tufahamu wanaopigana wakiwa upande wetu bega kwa bega ni akina nani. Wanaweza kuwepo watu wa namna hiyo lakini si Wabunge.

Sikiliza haya yanayohusi Wabunge. Halafu tupaze sauti zetu kuwataka waache kutunyonya. Waache kuumiza Watanzania Maskini.

Tuanze na kupunguza mishahara yao iwe nusu, kisha tuwaambie walipe kodi na PSSSF, na wakimaliza muda wao wasubirie miaka miwili kupewa kiinua mgongo.

Wasiruhusiwe kukopa kutoka mifuko ya PENSION.

Yangu mimi ni hayo tu.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Umesema cha maana sana hakika wabunge ni miongoni mwa wanyonyaji wakubwa. Isitoshe viti maaluum havina ulazima wala haisaidii kitu vifutwe. Tumejenga tabaka la watu fulani kazi yao kuzungukia nafasi hizo kwa njia ya kutoa rushwa.
 
Ni kweli kwamba Wabunge wetu ni WANYONYAJI wakubwa. Ni KUPE. Marupurupu wanajipangia wenyewe. CONFLICT OF INTEREST!

Talk is cheap. UZALENDO, UZALENDO kumbe ni WIZI, WIZI na uporaji wa mali ya uma.

Kwa vile hakuna upinzani, watajichotea watakavyo. Kwa katiba iliyopo ni mtindo wa kunyonywa bila huruma, na huku wakifunika kombe kwa kutaja sana neno UZALENDO.

Waheshimiwa hawa ni MABWANYENYE yaliyokubuhu.
 
Adui mkubwa ni Ccm hakuna kingine. Bila ccm labda leo hii kama nchi tungefika mbali sana.
CCM?! Unasahau akina mdee, akina bulayo, akina kitila, lijua likali, etc.

Hao wote ni wale wale. Achana na habari za vyama, simama na raia wenzako, chama chako ni uraia, katiba ni ile ya taifa. Weka vyama kando.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Tuanze na kupunguza mishahara yao iwe nusu, kisha tuwaambie walipe kodi na PSSSF, na wakimaliza muda wao wasubirie miaka miwili kupewa kiinua mgongo.

Wasiruhusiwe kukopa kutoka mifuko ya PENSION.

Yangu mimi ni hayo tu.

Everyday is Saturday............................... :cool:
Nakuunga mkono. Wabunge ndio maadui zetu.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Watanzania. Naomba kwa heshima na Taadhima. Leo hii tufahamu wanaotukwamisha katika maendeleo ni akina nani. Hatuwezi shinda vita vya Umaskini ikiwa Hatujafahamu Maadui zetu ni akina nani.

Tunapaswa pia tufahamu wanaopigana wakiwa upande wetu bega kwa bega ni akina nani. Wanaweza kuwepo watu wa namna hiyo lakini si Wabunge.

Sikiliza haya yanayohusi Wabunge. Halafu tupaze sauti zetu kuwataka waache kutunyonya. Waache kuumiza Watanzania Maskini.

View attachment 1817808
Hii attachment yako hata haikubali kufunguka. Hebu itume ila usiitume kama attachment. Tuma link au file....

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom