Mambo kumi ya kuzingatia kwenye Blog yako kabla ua kuanza rasmi

Kainetics

Senior Member
Jun 20, 2022
116
170
Kainetics Mambo Kumi Kablq HujaanzaBlogging.jpg


Hello, natumai mu wazima. Kwenye kujaribu kuiongelea Blogging kwa kina, kutokana na maombi ya baadhi ya wadau, nimeona mwanzo kabisa uwe na Basics, na hapa ntaongelea mambo ambayo utahakikisha umeyaweka sawa kabla hujaendelea na swala zima la Blogging.

Mengi ya haya mambo yatakua sio mageni, maana nina uhakika ntakua niliyaongelea kwenye ile Blogging 101, japo ntakazia. Hivyo, kam una blog na uko serious nayo kuona kuwa inakuletea matokeo mazuri , hakikisha umeyazingatia yafuatayo;

🏷 UPEKEE MZIMA WA BLOG [1]

Hakikisha Blog yako inamuonekano unaoridhisha, kwako wewe kama mmiliki na unaendana na mada ya kile utakachokuwa unaongelea. Kwenye muonekano kuna mambo matatu ya msingi; Matumizi ya Rangi, Branding na Aina ya Uandishi.

Yapo maelfu ya blogs huko ambazo zitakua zinaongelea kitu kile kile utakachokua ukikiongelea wewe hivyo kujitofautisha ni vizuri, na mhimu. Ndio maana unapaswa tafuta upekee kadri uwezavyo. Nikisema muonekano, naongelea blog nzima inavyofanana ukiitembelea kupitia simu ya mkononi au laptop yako.

Haipaswi kuwa na mambo mengi, iwe minimal, isiyo na tu maneno tudogo mno au mi maneno mikubwa. Likija swala zima la rangi, unapaswa kuwa na rangi zinazo kudefine wewe ili huko mbeleni ukianza kukua kama blog na brand, uwe unaweza tofautishwa na wengine.

Bloggers wengi wanao anza utakuta wanatumia templates zile zile, kana kwamba unaweza tembelea blog tano tofauti na mwisho wa siku ukahisi ulikua kwenye blog moja. Hio sio nzuri.

Ukifumba macho ukafikiria neno; MillardAyo, lazima rangi nyekundu na nyeupe zitakujia kichwani. Itakua hivyo hivyo ukifikiria neno BBC. Ukifikilia DW, itakujia rangi ya Blue. Na ingekua ufikirie Kainetics, rangi ya kijani itakujia kichwani.
Hivyo ni mhimu kujiuliza, ukifumba macho ukafikiria blog yako, rangi gani inakujia kichwani? Kama haipo rangi specific basi kuna tatizo mahali. Na kama ni nyeusi na nyeupe. Pia kuna tatizo mahali. Kuwa na rangi maalumu zinazo kudefine wewe.

Kabla sijatoka hapo hapo kwenye rangi, sio kisa nimesema uwe na rangi inayokudefine , basi uchague rangi yoyote ile, kuna rangi zinaendana na kitu fulani na kuna rangi zinagoma kabisa. Huwezi kuwa na blog unako ongelea mambo ya conputer na simu, ukaanza tumia rangi nyekundu. Hio ni rangi ya mahusiano na afya 🤣

Hizi ni baadhi ya Rangi na Ninche Zinazoendana

🎯 BLUE - Technology, Gaming, Music , Investment, Toys, Travel, Tourism, Business News, Job Vacancies, Betting, Forex na Product Reviews

🎯 GREEN - Personal Finance, Insurance, Savings & Loans, Making Money, Financial Freedom, Entreprenuership, Agriculture na Small Business Ideas/Projects.

🎯 RED/PINK - Health, Relationships, Counselling, Film Reviews, Entertainment, Breaking News, Family Advice, etc

🎯 ORANGE - Corporate News, Buying & Selling, Gym & Fitness, Weight Loss, Coupons, Offers , Giveaways, etc Hii ni rangi ya biashara ya kuuza na kununua.

🎯 YELLOW - Life Hacks, DIY, How-to Guides, Detailed Tutorials, Na Blog zozote zile ambako unafundisha skill maalumu, mfano, Graphics Design, Kuimba, Kupika, nk. N rangi ya kujifunzia.

Likija swala la Branding, ni kuhakikisha blog yako ina nembo inayokutambulisha, ambayo sio rahisi kusahau, nk. Nadhani nembo ya Kainetics unaifahamu, picha ya kwenye profile ya hii channel...na utaikuta karibia kwenye kila banner nazo tengeneza za post zote za humu.

Hii inasaidia kuzipa content zako upekee, kuonesha umetenga muda kuhakikisha una deliver ktu chako mwenyewe. Hivyo hakikisha blog yako ina nembo yako mwenyewe, yaani logo, Favicon na pia Banner zote za Blogpost utakazotumia, ziwe na ka nembo kako pia. Ni ka kitu kadogo, kenye nguvu in the long run.

Lastly, ni kwenye aina ya uandishi. Blog nyingi tunazoanzisha kwa madhumuni ya kutuingizia pesa, lazima zitakua za Kingereza maana main source ya uhakika ni Google Adsense. Shida, inakuja kwenye uandishi wenyewe, maneno yanaandikwa lakini hayana hisia zozote zile. Yaani yapo tu.

We tembelea blog 5 zinazomilikiwa na watanzania, za Kingereza. Unaweza dhani zimeandikwa na mtu mmoja . Ambae hajali hata anachokiandika. Hata za Kiswahili pia, mambo ni yale yale. Na hata channels za Youtube, utakuta wana copy format nzima ya content zao kana kwamba huwezi watofautisha. Jambo ambalo sio poa.

Tafuta sauti yako mwenyewe kwenye uandishi, kitu kinachofanya mtu anae soma content zako kujua anaeandika n nani, na kujijengea picha yake mwenyewe we ni mtu wa aina gani. Yaani choice ya maneno, salamu yako ilivyokaa, na unavyohitimisha blog post zako.

Mfano; kama ulikua hujui, unaweza define style yangu ya uandishi kua situmii Kiswahili rasmi, au sanifu. Maana naona kinaboa 🤓 pia Bullet Points utakuta nyingi nyingi, na Paragraphs n fupi fupi kukurahishia usomaji. Wewe uandishi wako uko defined vipi?

🏷 WRITING SCHEDULE [2]

Baada ya kujihakikishia kuwa Blog yako iko na upekee unaojitosheleza, kinachofuata ni kuamua aina ya Blogger ambae utakua. Zipo namna mbili ambazo unaweza amua kuwa kama Blogger na zote mwisho wa siku zinaweza ingiza pesa, japo kwa viwango tofauti.

Aina ya kwanza, ni ile unataka kumiliki Blog ambayo imekamilika kwa kila kitu(yaani iwe ina post zilizokwisha andikwa tayari) kazi yako iwe kuweka matangazo kuna kuongeza Traffic. Hii ni nzuri kama unafundisha kit fulani na ushaandika yote kuhusu hicho kitu ko hakuna haja ya kuandika mambo mapya.
Ukiwa Blogger wa aina hii na kama hizo post zako ziliandikwa vizuri na unapata traffic wa kutosha, let's say unique visits 2,500 kwa week, uhakika wa walau $450 kila mwisho wa mwezi upo.

Aina ya pili, ni kuwa Blogger anaeongeza content kwenye Blog yake mdogo mdogo. Hii ni nzuri kama Blog yako iko kwenye Ninche inayohitaji uandike mara kwa mara. Mfano kama una Blog ya Tech Reviews, lazima itakubidi uandike kila simu mpya, pc au OS mpya ikitoka. Maandishi yako yakiwa authentic na yenye mtiririko mzuri, basi utaanza jipatia watu watakao kuwa wanarudi mara kwa mara kusoma ndo maana utahitaji Writing Schedule.

Hii simply, ni ratiba unako panga siku gani utakua ukiandika content mpya, na kwenye Category gani. Siku gani utakua ukijibu comments, na siku gani utakua ukifanya SEO, au kufanya research ya content mpya.

Mfano wa Writing Schedule ni kama hivi;

SIKU | UTAKACHOFANYA
J/Tatu | ANDIKA BLOG POST MBILI
J/Nne | PUMZIKA
J/Tano | JIBU COMMENTS
Alhami | ANDIKA BLOG POST MBILI
Ijumaa | ANDAA CONTENT ZA NXT WEEK
J/Mosi | PUMZIKA
J/Pili | PUMZIKA

Kwa Schedule ya ivyo, utakua na post 4, zilizoandaliwa vizuri, kila week. Siku moja ya ku engage na readers wako na siku 3 za kupumzia au kufanya mambo mengine.

Ukiifanya hii kwa week 3 , inageuka mazoea, na visitors wako wanazoea siku gani wategemee content mpya. Umuhimu wa kitu kam, hio, inakufanya uwe commited, inakupa Recurring visitors na kuboost RPM ukishaanzakuwa na matangazo.

Hapa ndo unapomzidi Blogger ambae haandiki content mpya, maana ukiwa na unique visits kama zake, izo izo 2,500 kwa week let's say kwenye Niche ya Personal Finance, tegemea walau $750/mwezi average .

🏷 CTA's na AUTOMATED SUBSCRIPTION [3]

Kwenye mambo ya muhimu ambayo hayazingatiwi na karibia 90% ya Bloggers nliokutana nao ni hizo CTA's na Automated Subscription kwenye blog yako, kabla hata hujaanza rasimi kublog.

Hizi zinakusaidia wewe kutowapoteza visitors wako, wapya, na kuwapa urahisi wa kuaccess content zako, kwa kufanya wawe wanapokea email mpya au Notification kila ukiweka blogpost mpya kwenye Blog yako.

Kama hufahamu CTA'S ni nini, hizi zinaitwa Call To Action Prompts. Zinaweza kuwa Buttons, Forms, Pop Ups, nk. Mfano ukitembelea blog yangu ya Kainetics.one kwa mara ya kwanza kabisa. Itatokea pop up, ninapokwambia unadike jina lako na namba ya simu nikuunge kwenye Group langu la WhatsApp.

Hio inahakikisha kuwa msomaji mpya hapotei na huko kwenye group la WhatsApp huwa nashare tips mbali mbal, na kuwaacha wao kwa wao wadiscuss. Likijaa, naunda lingine na kufanya kitu kile kile. Now yapo magroup manne yenye watu walioserious na kile wanachofanya na kutaka kujua zaidi.

Kama utakua una blog ya Kingereza na una target watu wa nje, automatically huwezi unda pop ups zinazoomba namba zao za simu, bali email zao ili wawe updated kila ukipost kitu kipya. Hiki sio kitu cha lazima kufanya ila inasaidia kuboost CPC yako, Crawler Bots za Google zikiona Cordination ya traffic yako na Blog. Moja ya sababu kwanini Blog ya WordPress ni bora kuliko izo za Blogger.

Hivyo basi, hakikisha una hata ki form, au ki Pop Up kinacho collect email za users wako pendwa nawe in return unaweza wapea giveaway, kama course ya bure, au kitabu, nk. Uzuri ni kwamba unaweza automate process nzima. So, kama uliku na CPC ya let's say $0.25, ukfanikiwa collect leads 500, utakuta CPC imepanda yenyewe kwenda walau $0.95. Ni mhimu.

🏷 SOCIAL MEDIA ACCOUNTS [4]

Hii siendi iongelea kiundani hata 🤓 kama una Blog inaitwa LeroyTech.com , hakikisha una account Instagram inayoitwa LeroyTech, iwepo pia page ya Twitter, Facebook , Pinterest na Messenger.

Ziwe na logo sawa, description sawa na zote ziwe a link ya Blog yako. Kama una blog ya WordPress, tafuta Plugin yenye Automated Sharing, kuwa kila ukipost makala mpya kwenye Blog yako iwe inazituma directly kwenye social media accounts na Pages zako.

Simple ivyo, ila ni muhimu.

Readers zako wakitaka kukusemesha au kukuuliza kitu chochote wanakuwa wanafahamu pa kukutafuta, kukufuatilia nk. Karibia 70% ya watanzania gawasomi Blog ya MillardAyo ila wanamfuatilia Instagram na Youtube, na hio kwa nafasi yake inajitosheleza. Hivyo hakikisha izo Pages zipo.

Bonus
-----

Kua na email ya bishara ambayo pia unaweza andikiwa ujumbe directly, na hao readers zako. Mfano, info@jinalablog.com au hello@jinalablog.com au hata jinalako@jinalablog.com

🏷 ROYALTY FREE IMAGES [5]

Watu wengi huwa na blogs zilizo monetized na wanaamka siku moja wankuta wamepigwa Ban bila maelezo yoyote yanayoeleweka. Moja ya kisababishi kikubwa, ni Picha unazotumia kwenye Blog yako. Kama matani vile.

Kwenye hizi mambo za mtandaoni, aidha ukutane na audio, video au picha, fahamu tu kwa haraka haraka kuwa itakua na Copyright au Hakimiliki. Na wengi huwa tunazipuuza hizi, unaandika post yako, unaenda Google unasearch picha una dosnload unabandika kwe ye post, umemaliza. Kumbe umeharibu.

Na walivyowakorofi, wanakuacha kwanza mpaka uanze kuingiza hela, ndipo wanakuja appeal kuwa unatumia content za wtu wengine bila kubali au kuzinunua. Zipo aina tatu za Copyright ambazo unapaswa kuwa na idea nazo likija swala zima la Digital Contents;

1. Free For Personal/Non- Commercial Use- Hii inamaanisha video/audio/picha/maandiko husika unaweza yatumia uwezavyo ukiwa uafahamu hautoingiza hela kwa namna yoyte ile kwenye matumizi yako. Ukiingiza hela umevunja matumizi hivyo unakua kwenye makosa

2. Creative Commons/CC - Hii ni ile utakuta unaruhusiwa kufanya chochote unachotaka na content husik. Yaani hata uiuze, iuingizie hela, uiite yako, nk. Unakua hauko kwenye makosa.

3. Free For Commercial Use- Hapa ndo utakuta unaruhusiwa kuitumia kazi husika hata kama itakuingizia hela, lakini sio sahihi kuuita ya kwako. Hizi sana sana ndo utakuta ni lazima uzinunue.


Picha nyingi ambazo ziko Online ni aina hio ya kwanza na ndo rahisi kuonekana zikiwa za kwanza ukigoogle. Ukitumia izo kuwa na uhakika kuwa itafika muda fulani na account yako ya Adsense itafungwa tu kama uliwahi kuwa na matangazo.

Kukwepa hilo kasumba lolote, utahitaji kuwa na picha zinazotambulika kama Royalty Free Images. Yaani ni picha zenye Quality kubwa ambazo mmiliki wake anaruhusu kuzitumia utakavyo kikubwa umpe Credit. Hizi ndo picha unazopaswa tumia kwenye Blog yako.

Zipo sehemu kuu mbili ambako unaweza pata picha za namna hii,

Pexels.com na Unsplash.com . Ingia humo, search picha yoyote ile utakayotaka, utaikuta. Utadownload. Maisha yataendelea. Acha kugoogle na kudownload picha kizembe za kutumia kwenye blog yako.

🏷 CONTACT US PAGE (6)

Kabla hujaanza rasmi hio kitu nzima ya Blogging, hakikisha blog yako inayo contact page ambako readers wako wanaweza kuwasiliana na wewe, iwe wanataka fanya biashara pamoja, kuuliza swali au kuwasilisha kero zao.

Pia hii itaonesha kuna asilimia kadha wa kadhaa za kuwa legit , kama muandishi (au kama unaandika kama kampuni/brand)

Ukianza andika content za kingereza nyingi nyingi utakuta inatokea muda utaanza copy idea za titles na maandishi kwa bloggers wengine. Kwa hao wazungu, akihisi umecipy kazi zake, atakuandikia naomba uondoe post fulani uliyoandika maana sio yako. Ukitii na kutoa, utakua huna issue ya kuhofia, lakini ikibaki, unaweza pigwa strike from nowhere na kukuta una poteza monetization.

Mbali na mambo ya Monetization, fursa ni nyingi, na kama unapenda skiliza feedback ya readers wako, basi kuwa na hii page ni mhimu. Isiwe na mambo mengi, yaani form ambapo mtu ataandika jina lake, Subject ya Ujumbe, na ujumbe wenyewe.

Mambo mengine optional unayoweza kuongeza ni Barua pepe yako, social media links namba ya simu na hata adress.

Ila mhimu ni iwepo hii page na iwe kwenye primary menu ya blog.

🏷 ABOUT US PAGE (7)

Kama ilivyo page ya mawasiliano, page nyingine ya mhimu ambayo lazima iwe kwenye blog yako ni page unakoelezea wewe ni nani, unaandika kuhusu nini, kwanini unaandika mambo unayoandika na most importantly, unamlenga nani? Na viewers wako wategemee nini cha ziada kutoka kwako?

Hayo yote yanamwagwa kwenye About Us page. Hii ndio page ambayo ukiwa creatuive pia, unaweza itumis kutengeneza Authority ya jina la blog yako kama Keyword(kwa kulitaja mara kibao kadri utakvyoweza, walau hata mara 15)

Mfano; blog yangu inaitwa Kainetics. Ivyo kwenye About Page unaweza tegemea kukutana sentence kama hizi;....

...Karibu Kainetics!
...Kainetics Ni Nini?
...Kwanini Kainetics na sio 'Kinetics'
...Madhumuni ya Kuanzisha hii Blog ya Kainetics
...Huduma Unazoweza pata toka Team Kainetics...Hizo mambo zote na paraghraoh zitakazoandikwa kujibu hilo swali, zinalipa neno 'Kainetics' credibility kama Keyword kana kwamba ukitokea kulisearch, utakutana na Blog yangu ikiwa imeshirikia nambari moja.

Hio ndo most Basic SEO practice unayoweza fanya, yenye matokeo ya haraka na chanya.

🏷 PRIVACY POLICY, DISCLAIMER & TERMS AND CONDITIONS (8)

Hizi kwa jina lingine unaweza ziita Legal Dumps. Kwa msomaji wa kawaida kama mimi na wewe, ni mambo ambayo hatuna muda nayo, maana sidhani kama kuna mtu anasomaga izo Policies au Terms, nk. Zipo, uta agree na kuendelea na safari, hivyo unaweza jiuliza, kama hakuna anaezipaga muda kwanini mimi nijihangaishe nazo kuziweka?

Una kila sababu kwanini unapaswa fanya ivyo.

1. Disclaimer huwa ipo kumwambia user kuwa kwenye blog yako anaweza kutana na affiliate links ambazo in one way or the other, akizigusa na kufanya purchase, utaingiza kamisheni.
Kitu ambacho kwa nchi zilizoendelea ni cha mhimu, maana watu hawapendi onekana kama walichakachuliwa au uliandika post husika ilimradi upate kamisheni na hujali ulichosema.

Hivyo ni mhiku kuwa na Disclaimer...inayoelezea uwepo wa izo affiliate links au matangazo kwenye blog yako, hauusiani na credibility ya kile unachoandika.

2. Privacy Policy, kwenye privacy policy, unapaswa kua very specific kwenye kuelezea data gani za visitors wako unazicollect na pia unazifanyia nini.

Sana sana, hapa huwepo mambo kama Cookies, IP, Email na Device Info. Wengi wanaogopa data zao kuuzwa , hivyo unapaswa clarify kua data zote unazocollect kwenye blov yako, zinabaki kwako na hakuna Third Party Entity inayohusika.

90% hatusomagi izi Policies, ila fan fact makampuni yote yatakayoweka Matangazo kwenye Blog yako lazima yatapitia Policy zako kuona kama zinabana au zimelegea mno. So, kama unaenda weka Ads za Adsense, Adsterra au InfoLinks...lazima Privacy Policy iwe intact.

Lastly ni T&C. Hizi nadhani zipo, ukiwa unaweka app mpya kwenye simu, aidha uwe unaweka software kwa pc, na hataukitembelea blog/Ecommerce store yoyote ile. Ila ukweli unabaki pale pale 95% hatusomagi izi mambo, na hazina faida kwa wengi isipokua scenario moja mtu akitaka kukuletea mauza uza, kama una offer services zozote zile.

Term's & Conditions zenyewe zipo kuelezea misingi inayoendesha blog yako, scenario gani zikiwepo zitaleta matokeo gani na kwanini.

Mfano, nina tengeneza blogs kwa wanaozihitaji. Anaweza kuwepo mtu akanilipa hela nimtengenezee blog, na nikamtengenezea kwendana na kiasi alichotoa. Inaweza tokea siku moja akachanganyikiwa, umemkabidhi akakuambia nimehailisha naomba nirudishie hela yangu 😁😁 hapo ndipo Terms & Conditions zinaingia.

Kama hukuwa specific nini kitaonesha kazi imekamilika, au ni kwa scenario gani mteja anakua sahihi kurudishiwa hela, basi inamaanisha itabidi umpe tu hela yake, au unageuka kuwa tapeli. Hata kama ulikua kwenye usahihi.

Kama unauza vitu online, mtu anunue T-Shirt Nyekundu, kwa bahati mbaya umtumie ya blue, kama kwenye Terms na Conditions zako hukuspecify nini kinatokea kwenye scenario kama hio, akitaka umrudishie hela yake na tshirt ya blue abaki nayo. Anakua hayuko kwenye makosa. Hii ndo maana unapaswa tenga muda wa kutosha kuhakikisha Terms zako ziko fair , zinakulinda wewe na zinamlinda mteja wako.

Nadhani hio ndo sababu nyingi haya ma platform mengi ya kitapeli yana uwezo wa kukwepa kesi nyingi mahakamani, pale yanapo dhulumu wateja wake, maana kipundi unasignup uliweka ki tick kuwa unakubali Terms & Condition zao.

So siku nyingine tengaga muda uzisome kabla hujakurupuka. Na kwenye tovuti yako, ni mhimu ziwepo kama una offer huduma ya aina yeyote ile.


Kuziunda hizi unaweza tumia Generator kibao tu Online. Ni kuGoogle, "Privacy Policy Generator, Refund Policy Generator au T&C Generator, etc" and you'll be good to go.

Usizipuuze hizi.

🏷 ANALYTICS (9)

Hii sitoiongelea sana maana inahitaji kuongelewa kivyake vyake kwa kuwa Topic yake ni kubwa. Kama una biashara au tovuti yoyote ile, na ungependa kuiona inakua, lazima uwe na data za kutosha kujua wapi unapo feli na wapi unapatia.

Huo ndo umuhimu wa kuwa na Data Analytics. Kujua mambo kama Traffic unayopokea kwa siku, views ni ngapi, Post gani zinatazamwa zaidi, wasimaji wako wanatoka google au kwenye social media, wengi ni wa nchi gani, na wanatumia vifaa gani ku access site yako. Jinsia na mambo kama hizo.

Kabla hujaanza kufanya Blogging, hakikisha ume set mfumo mzuri wa kucollect data kama hizo. Mimi ni mtumiaji wa WordPress, na kwa WordPress kupitia Google Site Kit, unaweza unga Google Analytics na Search Console ambazo zita kufeed kila aina ya data utakayokuwa ukitafuta.


Zipo Plugins kama JetPack na MonsterInsights ambazo zitakupea data nzuri tu na za kutosha. So stick to them.

🏷 CONTENT LOCK (10)

Hii ndio kitu ya mwisho na ya mhimu, japo sio ya lazima. Hii pia itakusaidia sana kama uko kwenye ninche inayohitaji uandike content kwa kina, na baada ya kufanya research ya kutosha.

Hakuna jambo linatia hasira kwa mwandishi yeyote yule, kama kuharibu masaa 10+ kuandaa content zilizotulia then from nowhere mtu aje acopy na kupaste kwake.

Ndio maana ni vizuri kuwa na hii Content Lock Plugin. Zipo za bure na za kulipia (sijajua kwa Blogger kama unaweza fanya hii kitu, lakini kwa WordPress ni uhakika)

Kama utakua na blog ya Kiswahili, ni rahisi hizi mambo za kuibiana maandiko kukutana nazo, so kulock content zako kana kwamba mtu hawezi ku copy , nk. Itakusaidia. Yapo mengine mengi lakini kwa leo niishie hapo.

Itimisho

Ukijipa muda wa kutosha kuhakikisha mwanzo wa hio Blog yako ume cover hizo aspect zote za msingi, basi safari yako ya kuandika itakua imerahisishwa kwa ukubwa wake maana utajikita kuandika, na kufanya SEO. Bila hofu ya mambo madogo madogo kama hayo(yanayoweza geuka makubwa yakiamua)

Kama una maswali , nyongeza au maoni karibu. Pia mtasamehe kwa sehemu yoyote utakapikutana na typing error. Ntapitia baadae na kujaribu kuedit.

Nawasilisha,
Kainetics
 

Kainetics

Senior Member
Jun 20, 2022
116
170
[Nje ya Topic]

Ukihitaji kuundiwa Blog Professional ambako karibia yote ya hayo nliyoandika yamekua covered, waweza ni PM. Itakua na ;
✍ Paid Domain of your choice
✍ Hosting Miezi 2- Utaendeleza Lipa Mwenyewe After Those Two Months
✍ Premium Theme
✍ Logo na Basic SEO
✍ Na nkikukabidhi ukifika muda wako wa kuunga Adsense assistance hio natoa bure.
 

mtu chake

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
28,030
58,028
[Nje ya Topic]

Ukihitaji kuundiwa Blog Professional ambako karibia yote ya hayo nliyoandika yamekua covered, waweza ni PM. Itakua na ;
✍ Paid Domain of your choice
✍ Hosting Miezi 2- Utaendeleza Lipa Mwenyewe After Those Two Months
✍ Premium Theme
✍ Logo na Basic SEO
✍ Na nkikukabidhi ukifika muda wako wa kuunga Adsense assistance hio natoa bure.
mawasiliano hujaweka
 

mkulu senkondo

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
1,650
3,005
[Nje ya Topic]

Ukihitaji kuundiwa Blog Professional ambako karibia yote ya hayo nliyoandika yamekua covered, waweza ni PM. Itakua na ;
Paid Domain of your choice
Hosting Miezi 2- Utaendeleza Lipa Mwenyewe After Those Two Months
Premium Theme
Logo na Basic SEO
Na nkikukabidhi ukifika muda wako wa kuunga Adsense assistance hio natoa bure.
Mkuu hapo inagharimu kiasi gani, I mean total cost mpaka blog yangu isimame?
 

Kainetics

Senior Member
Jun 20, 2022
116
170
Mkuu hapo inagharimu kiasi gani, I mean total cost mpaka blog yangu isimame?
Total costs zinategemea na bajeti yako kwanza, pia na features utakazo taka ziwe ndani ya Blog yako.

Kwa Basics za lazima,
Ipo Domain (Hizi zina range from $2/mwaka hadi $9/mwaka kwa domain za .com, .net, etc ivo ni wewe kuchagua unataka domain za aina gani)

Hosting (Hii ni walau $3.95/mwezi. Wewe ndo utachagua utaanza na kulipia miezi mingapi ya Hosting)

Baada ya izo ndipo inakuja gharama ya kuundiwa blog, ambayo ina depend na features unazohitaji ziwemo kwenye blog na mambo extra utakayotaka nifanye:

So ukiondoa gharama za Hosting + Domain, unaweza ongeza gharama zangu binafsi from 115k hadi 655k (hio itadepend na mambo unayotaka ndani ya blog. Though ideal pricing ipo kwenye 235k kwa blog yenye kila kitu unachohitaji kuanza rasmi/professionally)

Waeza nicheck PM
 

mkulu senkondo

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
1,650
3,005
Total costs zinategemea na bajeti yako kwanza, pia na features utakazo taka ziwe ndani ya Blog yako.

Kwa Basics za lazima,
Ipo Domain (Hizi zina range from $2/mwaka hadi $9/mwaka kwa domain za .com, .net, etc ivo ni wewe kuchagua unataka domain za aina gani)

Hosting (Hii ni walau $3.95/mwezi. Wewe ndo utachagua utaanza na kulipia miezi mingapi ya Hosting)

Baada ya izo ndipo inakuja gharama ya kuundiwa blog, ambayo ina depend na features unazohitaji ziwemo kwenye blog na mambo extra utakayotaka nifanye:

So ukiondoa gharama za Hosting + Domain, unaweza ongeza gharama zangu binafsi from 115k hadi 655k (hio itadepend na mambo unayotaka ndani ya blog. Though ideal pricing ipo kwenye 235k kwa blog yenye kila kitu unachohitaji kuanza rasmi/professionally)

Waeza nicheck PM
Nimekuelewa ndugu yangu. Nitajipanga then I will contact you.
 

ElimuKwanza Tz

Senior Member
Jun 5, 2021
187
225
Safi Happ kwenye picha ndipo pakikuwa pananiumiza kichwa vibaya.

Swali 01
langu mfano Niche nayotaka ifanya sio ya kuandika kilasiku mfano ukiandika Post 100 almost Kama umeshaandika kilakitu kwenye hiyo Niche na Blog Ni jambo endelevu miaka na miaka mbele je ninaweza andika post hizi zinzofika 100 nkawa siandiki tena na pesa nikawa naingiza.

Swali 02
Source yangu ya picha ikiwa unsplash je itakuwa na ulazimw wawapa credit kwenye post zangu.

Pia vipi kutumia picha za shutterstock
 

Kainetics

Senior Member
Jun 20, 2022
116
170
Safi Happ kwenye picha ndipo pakikuwa pananiumiza kichwa vibaya.

Swali 01
langu mfano Niche nayotaka ifanya sio ya kuandika kilasiku mfano ukiandika Post 100 almost Kama umeshaandika kilakitu kwenye hiyo Niche na Blog Ni jambo endelevu miaka na miaka mbele je ninaweza andika post hizi zinzofika 100 nkawa siandiki tena na pesa nikawa naingiza.

Swali 02
Source yangu ya picha ikiwa unsplash je itakuwa na ulazimw wawapa credit kwenye post zangu.

Pia vipi kutumia picha za shutterstock
Kujibu swali la kwanza, kuandika post mpya kwa mkupuo hutopata hela yoyote, na ukifanikiwa kupata au hata hio Organic Traffic utakua na bahati tu, sema sio creative na haiku define kama Blogger.


Blog nyingi za ivo zimekuwepo kibao, 18th August, Google wakaleta kitu inaitwa 'Helpful Content Update' hii inachuja makala zote na blog zilizoandikwa kwa hio system kama yako( log zilizolenga kupata traffic na ad clicks basi, na sio kusaidia wasomaji)

Na blog nyingi kama una bloggers wenzio, waweza uliza; kama walikua wanavuta visitors 500 hadi 10,000 kwa siku. Now wanavuta visitors wachache mno. Mpaka wabadili hio approach ya uandishi.


Unazo post 100 already, WordPress kuna kitu inaitwa Post Scheduling. Unaziandika zote lakini kila post unaipea muda wake wa kua published.

Ila kama unaandika ile ya rasha rasha/kiroboti; ukweli mchungu ni bado kutoboa itakuwia ngumu
 

Kainetics

Senior Member
Jun 20, 2022
116
170
Safi Happ kwenye picha ndipo pakikuwa pananiumiza kichwa vibaya.

Swali 01
langu mfano Niche nayotaka ifanya sio ya kuandika kilasiku mfano ukiandika Post 100 almost Kama umeshaandika kilakitu kwenye hiyo Niche na Blog Ni jambo endelevu miaka na miaka mbele je ninaweza andika post hizi zinzofika 100 nkawa siandiki tena na pesa nikawa naingiza.

Swali 02
Source yangu ya picha ikiwa unsplash je itakuwa na ulazimw wawapa credit kwenye post zangu.

Pia vipi kutumia picha za shutterstock
Kujibu hlo swali la tatu, kwenye disclaimer unaweza sema picha zako unazitoa Unsplash na Pexels. Kurahisha mambo, tafuta artist watano wanaoendana na ninche yako, wafollow hao ndo uwe unachukua picha kwao, tu.
Kuwapa credit ya picha watu watano kwa pamoja kwenye disclaimer ni simple kuliko kutoa credit kwa kila picha.

Pia, WordPress wameweka feature ukiwa unaandika unaweza import picha directly from Pexels na kuibandika kwenye post. Credits zitawekwa automatically.

95% ya Picha zilizoko Shutterstock haziko free for commercial use. Sioni ulazika wa kujisimbua kama free alternatives zipo. Ila kama umelipia hio subscription ya Shutterstock nadhani sio kesi, mbal na hapo ni kujipandia matatizo.
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom