Wabongo Hawatumii Consultants vizuri ndio maana wengi wanafeli kwenye biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,506
5,544
Kwanza nianze kwa kusema kwamb mimi ni msahuri mwelekezi wa Kibiasha kwa wajasiriamali wadogo na wakati hasa wanaofanya biashara zneye Mtaji au annual turnover ya kati yz TZS 10,000 hadi TZS Milion 500.

Nimebahatika kufanya kazi na wajasiriamali wengi na nikagundua kwamba Wajasiriamali wengi wanakwama na kushindwa katika biashara kwa sababu ya kutokufahamu nafasi na jinsi ya kuwatumia Business Consultant.Wengi huamini katika hadithi za kusimuliwa,uzoefu na stori za hapa na pal.Hali hupelekea wengi wao kufanya makosa yale yale yanayopelekea biashara zao kutokukua.

Mshauri katika biashara yoyote ana nafasi kubwa ka mentor,critic na motivator,Mentor anakupa mwongozo,Critic anakufanya ufikiri zaidi na motivator anakutia moyo.Unapofanya biashara yeyote ni lazima uwe na watu wote watatu au ue na mmoja anayefanya kazi zote tatu.Huyu anaitwa Consultant.

Kzi ya consultant ni kufikiri badala yako,kupanga badala yako,kutafuta taarifa badala yako.Nimekutana na watu wengi sana ambao hawataki habari za ushauri na wengine wanatka kupewa ushauri wa bure bila kulipia.Kitu wasichojua ni kwamba sisi tumewekeza rasilimali katika kutafuta taarifa na maarifa pamoja na kujenga mtandao.Wanataka tu msaada lakini ukiwaonjesha kidogo kisha ukataka wakulipe wanachukizwa

Vile vile wengine wanakuwa na kasumba ya kujifanyia mambo kienyeji jambo ambalo nalo linashangaza sana hasa ukizingatia wengine ni wasomi wakuwa kabisa.

Niwaombe wajasiriamali wote wadogo na wakubwa,usiogope kutumia gharama ili kupata taarifa na maarifa sahihi.
 
Tangazo halijakamilika kamanda. Weka namba ya simu au website ya kampuni yako ili wajasiriamali waanze kukutafuta...

Na kwa kukunong'oneza tu ni kwamba sisi haya mambo ya sijui ya consultancy, business plans sijui na vitu gani huko bado kidogo. Sisi tunaangalia tu ni biashara gani imemtoa jirani nasi tunafungua hiyo hiyo.

Mambo mengine tutajuana huko huko mbele ya safari. Wakati mwingine tunatoboa, mara nyingi tunakwama ila maisha yanaenda.
 
Mkuu mm nafanya biashara ya kubadilisha Gas mtaji sio mkubwa kivile ,nifanyaje ilo nipate au niongeze wateja wapya maana kila mwezi wateja ni wale wale wa mtaani ??
Kwa mujibu wa maelezo yako wateja ni wale wale wa mtaani kwako,Je umewafikia wateja wote wa mtaani kwako?Je unalenga wateja wapya wa mtaa gani?Je Gas tu ndo unawauzia au kuna huduma nyingie?
 
Tangazo halijakamilika kamanda. Weka namba ya simu au website ya kampuni yako ili wajasiriamali waanze kukutafuta...

Na kwa kukunong'oneza tu ni kwamba sisi haya mambo ya sijui ya consultancy, business plans sijui na vitu gani huko bado kidogo. Sisi tunaangalia tu ni biashara gani imemtoa jirani nasi tunafungua hiyo hiyo. Mambo mengine tutajuana huko huko mbele ya safari. Wakati mwingine tunatoboa, mara nyingi tunakwama ila maisha yanaenda.
Mkuu mawasiliano yetu ni Whatsap +255710323060 au Email masokotz@yahoo.com

Ni wakati sasa wa kubadilisha fikra na kuanza kufikira beyond that ingawa ni namna moja ya kuelewa ila,Wakati mwingine Jirani anaweza akawa na namna nyingine ambayo wewe huijua ukaangukia Uso.Hapo ndipo Consultants wanakusaidia kutambua kwa hakika kama chanzo cha mafanikio ni biasahra ama la?
 
Kwa mtazamo wangu na uzoefu wa kufanya ujasiriamali/biashara:

1. Consultation inafanya kazi vizuri zaidi katika medium na large scale businesses ila kwa biashara ndogo kidogo ni mtihani.

2. Mifumo yetu mingi sio rasmi wakati Consultants wetu mara nyingi wanatoa ushauri ambao si mbaya bali unahitaji mifumo rasmi kuoperate.

3. Wafanyabiashara wetu kwa asilimia kubwa wana magumashi mengi kuanzia kwenye namna ya upatikanaji wa mtaji, uendeshaji, ulipaji kodi nk nk hivyo wanaoperate nje ya uhalisia ndio maana hawaoni kama consultation ni jambo lenye maana.

4. Wafanyabiashara wengi huiga anacho fanya fulani hivyo wanaona kama kulipia consultation ni kuchezea pesa.
 
Tangazo halijakamilika kamanda. Weka namba ya simu au website ya kampuni yako ili wajasiriamali waanze kukutafuta...

Na kwa kukunong'oneza tu ni kwamba sisi haya mambo ya sijui ya consultancy, business plans sijui na vitu gani huko bado kidogo. Sisi tunaangalia tu ni biashara gani imemtoa jirani nasi tunafungua hiyo hiyo. Mambo mengine tutajuana huko huko mbele ya safari. Wakati mwingine tunatoboa, mara nyingi tunakwama ila maisha yanaenda.
Anatoa Ushauri wa biashara lakin yeye hana biashara
Daaah wabongo ni shiiida
Utopolo
 
Kwa mtazamo wangu na uzoefu wa kufanya ujasiriamali/biashara:

1. Consultation inafanya kazi vizuri zaidi katika medium na large scale businesses ila kwa biashara ndogo kidogo ni mtihani.

2. Mifumo yetu mingi sio rasmi wakati Consultants wetu mara nyingi wanatoa ushauri ambao si mbaya bali unahitaji mifumo rasmi kuoperate.

3. Wafanyabiashara wetu kwa asilimia kubwa wana magumashi mengi kuanzia kwenye namna ya upatikanaji wa mtaji, uendeshaji, ulipaji kodi nk nk hivyo wanaoperate nje ya uhalisia ndio maana hawaoni kama consultation ni jambo lenye maana.

4. Wafanyabiashara wengi huiga anacho fanya fulani hivyo wanaona kama kulipia consultation ni kuchezea pesa.
 
Consultation nyingi za kibongo ni za kimagumashi sana... they dont give you the actual business fever .. ila wanakupa uhalisia tu wa kwenye makatatasi

Lakini baadhi ya consultants they dont know industries, bongo hapa tafuta consultants wa Tech uone unavyosaga lami umwambie kuwa unataka kuanzisha "peer to peer sharing economy platform" umeshampoteza maboya hao ndio consultants wetu

Consultant anatakiwa ajue masoko yakoje, uelekeo wa soko la dunia likoje na kila sector unakuta kuna expert wake ndio maana kampuni kama McKinsey and company iko juu sababu ya hii

Njoo hapa sasa kampuni ina consultant mmoja kwenye madini yumo, kwenye sekta ya fedha yumo, kwenye michezo yumo, kwenye teknolojia yumo

Ndio maana wazungu kama sio sekta yao wanakwambia black and white kuwa hatu consult biashara za aina fulani

Sasa basi kibongobongo mtu akiona hivyo anajua ni dili
 
Mkuu mawasiliano yetu ni Whatsap +255715323060 au Email masokotz@yahoo.com

Ni wakati sasa wa kubadilisha fikra na kuanza kufikira beyond that ingawa ni namna moja ya kuelewa ila,Wakati mwingine Jirani anaweza akawa na namna nyingine ambayo wewe huijua ukaangukia Uso.Hapo ndipo Consultants wanakusaidia kutambua kwa hakika kama chanzo cha mafanikio ni biasahra ama la?

Wewe unabiashara yoyote mkuu?..
 
Kwa mtazamo wangu na uzoefu wa kufanya ujasiriamali/biashara:

1. Consultation inafanya kazi vizuri zaidi katika medium na large scale businesses ila kwa biashara ndogo kidogo ni mtihani.

2. Mifumo yetu mingi sio rasmi wakati Consultants wetu mara nyingi wanatoa ushauri ambao si mbaya bali unahitaji mifumo rasmi kuoperate.

3. Wafanyabiashara wetu kwa asilimia kubwa wana magumashi mengi kuanzia kwenye namna ya upatikanaji wa mtaji, uendeshaji, ulipaji kodi nk nk hivyo wanaoperate nje ya uhalisia ndio maana hawaoni kama consultation ni jambo lenye maana.

4. Wafanyabiashara wengi huiga anacho fanya fulani hivyo wanaona kama kulipia consultation ni kuchezea pesa.
Uzi ufungwe umemaliza kila kitu
 
Consultation nyingi za kibongo ni za kimagumashi sana... they dont give you the actual business fever .. ila wanakupa uhalisia tu wa kwenye makatatasi

Lakini baadhi ya consultants they dont know industries, bongo hapa tafuta consultants wa Tech uone unavyosaga lami umwambie kuwa unataka kuanzisha "peer to peer sharing economy platform" umeshampoteza maboya hao ndio consultants wetu

Consultant anatakiwa ajue masoko yakoje, uelekeo wa soko la dunia likoje na kila sector unakuta kuna expert wake ndio maana kampuni kama McKinsey and company iko juu sababu ya hii

Njoo hapa sasa kampuni ina consultant mmoja kwenye madini yumo, kwenye sekta ya fedha yumo, kwenye michezo yumo, kwenye teknolojia yumo

Ndio maana wazungu kama sio sekta yao wanakwambia black and white kuwa hatu consult biashara za aina fulani

Sasa basi kibongobongo mtu akiona hivyo anajua ni dili
Very true.
Na kinachosababisha kuwa hivyo ni kwamba Watanzania tuko nyuma kidunia kwenye mambo yote yanayohusu taaluma.
Yaani unakuta mtu akishamaliza chuo basi kamaliza anajiona ni expert tayari na anakuwa hana mpango wa kujiendeleza kwa kufuatilia kozi mbalimbali za kidunia.
Ingekuwa tunapata nafasi ya kujilinganisha na wataalamu wa nchi mbalimbali tungepata uhalisia ulivyo na tungekazana.
 
Mkuu unakosea,

Tatizo wala si kwamba ni Wabongo.

Tatizo ni kwamba hao wafanyabiashara unaowalalamikia ni kwamba hawaoni VALUE yoyote toka kwako wewe consultant.

Kwa kawaida ukiwa consultant wa ukweli watu wanakufuata wenyewe.

Inabidi watu waone bila shaka kwamba wewe ni mjuzi wa biashara unayotaka watu wakupatie pesa kwa ushauri + mbinu zako.

Waonyeshe baadhi ya biashara ulizozisaidia na kweli zimefanikiwa. Au waonyeshe biashara yako iliyofanikiwa ili waamini.

Hiyo inaitwa social proof.

Tofauti na hapo utabakia kulaumu wafanyabiashara bure tu.
 
Back
Top Bottom