Mafunzo ya Jinsi ya Kuanzisha na Kusimamia Biashara Ndogo

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,494
5,529
Habari za wakati huu;

Kama wewe ni mfuatiliaji wa makala zetu basi utafahamu kwamba tumekuwa tukijitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kushea baadhi ya maarifa na taarifa ambazo tunazo kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wadog na wakati katika kusimamia na kuendesha biashara zao.Wengi ambao wamekuwa wakisoma makala zetu huenda wakawa na mtazamo na fikra tofauti kuhusu huduma na bidhaa zetu.Moja kati ya mitazamo yao ni kwamba huenda sisi tuliokuwa tunawaandikia makala hii huenda ni matajiri wa kiwango cha juu na kwamba tupo hapa kuwapa watu siri na njia tulizopitia kufikia ngazi ya juu ya maisha.Pia kuna wengine ambao wanafikri sisi ni Category ya watu ambao waswahili huwaita MOTIVESHENO SPIKA ambao ni watu muhimu katika maisha ingawa pia lazima tukubali kwamba kuna wakati hawa MPs wanakuwa kama wanasiasa wakihamasisha watu wafanye mambo fulani huku wao wakifanya mambo mengine.Yote kwa yote sisi ni watu wa kawaida tunaokumbana na changamoto za kawaida ambao kwa kadiri ya karama alizotupa Mungu na kiu yetu ya kutaka na sisi kuwa sehemu ya Mafanikio ya maisha ya watu fulani tunajitoa katika kufanya tafiti,kujifunza,kukagua na kujitahidi kuelewa mambo mbalimbali ambayo tunaamni kwamba yanaweza kutusaidia sisi na wengine.Hivyo basi vyovyote utakavyoelewa zingatia kwamba SISI hatukupi njia mbadala ya kufanikiwa na wala hatukupi guarantee ya kwamba maandiko yetu na mbinu zetu zitakupa nafasi kubwa ya kufanikiwa katika maisha au biashara yako.

Hata hivyo kwa mujibu wa utafiti yuliofanya tunatambua kwamba kila mwanadamu anao ukomo wa uwezo wake na kwamba kuna wakati tunahitaji ama kukubaliwa au kupewa maoni mbadala ili tuweza kupata picha kamili ya uelekeo wa biashara au maisha yetu.Katika kazi hii ya kujaribu kufanya kazi na biashara ndogo na za kati nimekutana na watu wa aina tofauti na biashara tofuati.Nimejifunza mambo mengi yaliyoko katika fani yangu na nje ya fani yangu.Pamoja na hayo yote bado nimekuwa nikijiona kuwa mtupu kwani kila mara najikuta inabidi nirudi tena darasania na kujifunza upya.Mimi ni muumini wa life long learning na ninaamini kwamba kujifunza hakuna ukomo.Ninaamini katika umuhimu wa kujifunza na kugawana maarifa hivyo basi ni muhimu sana kwangu kujitahidi kutoa marifa niliyonayo kwa kadiri niwezavyo kwani kuna ambao wanayo maarifa mengi kuliko yangu lakini ama hawajapata nafasi ya kuwapa maarifa hayo watu wengine au hawajataka kuwapa watu wengine maarifa kwa hofu ya kuzidiwa.

Wapo watu wengi sana ambao nimewahi kuwapa mafunzo binafsi na katika makundi pasi na kutoa mualiko kwa watu kushiriki.Moja kati ya sababu inayochangia hilo ni ukweli kwamba mwamko wa kupata maarifa ni mdogo na wengie tunata mafanikio kwa njia ya mkato.Mazoea ya kupenda njia ya mkato imepelekea watu wengi kujikuta wakishindwa kufikia malengo yao kimaisha na wengine kujikuta thamani yao au biashara zao zikikwama pale wanapokosa namna ya kuweza kusonga mbele kwa sababu ya kukosa maarifa.

Baada ya kutafakari kwa kina na kuona kwamba upo uhitaji wa mafunzo haya na kwamba watu wengi wanakosa uelewa wa masuala madogo kama masuala yahusuyo sheria za biashara,sheria za kodi na elimu kuhusu teknolojia mbalimbali za kibiashara pamoja na biashara za kimataifa nimezungumza na wataalamu mbalimbali wa kisheria,kodi na wafanya biashara wazoefu ambao wanaweza kutumia muda wao mchache katika kuwashauri watu wanaoibuka katika biashara au ambao wanahitaji elimu ya biashara iliwaweze kutenga muda wao kwa ajili ya kuwapatia ABC za biashara na pia kuwapa huduma ya coaching na mentorship.Baadhi ya watu hawa wameonesha pia interest ya kutaka kuwekeza katika baadhi ya biashara ndogo ambazo ni promising au hata kuwapa watu hawa connection za biashara.Watu hawa sio wengi na hawana muda mwingi bali wametenga nusu saa hadi lisaa limoja kwa ajili ya shughuli hizi ambazo wanafanya kwa kujitolea.

Hivyo basi ninatoa mualiko kwa mtu yeyote ambaye ana nia ya dhati ya kujifunza kuhusu mbinu za kibiashara katika maeneo mbalimbali au ambaye angependa kuwa na mentor ambaye ana uzoefu katika biashara au usimamizi ili amuongoze katika baadhi ya mambo basi atume email fupi yenye maelezo mafupi kuhusu biashara yake kwa lugha ya kiswahili au kiingereza kwenda katika email yetu ya masokotz@yahoo.com.Kulingana na mahitaji yako unaweza kuwa specific kwa kile unachohitaji,mahali biashara yako ilipo na taarifa nyingine kuhusu biashara yako.Zingatia kwamba huduma hii kwa sasa ni bure kwa washiriki wote na sio kila ataketuandikia atapewa nafasi kwani nafasi na muda ulioko ni limited.Hata hivyo kama unahitajimafunzo ya kulipa unaweza kuweka maeneo ambayo ungependa kuelimishwa na bajeti yako na mahali ulipo ili tuweze kutazama namna ambavyo tunaweza kufanya kazi pamoja.

Kwa wale ambao wako Mkoa wa ARusha na Dar es Salaam kuna mafunzo kila MWEZI iwapo unapenda kushiriki katika mafunzo ya Darasani tuma email kwa mratibu wa mafunzo kwa email ifuatayo:libera@tzhosts.com

Kwa mawasiliano zaidi na taarifa zingine wasiliana nasi kwa email:masokotz@yahoo.com au Simu 0710323060

Karibuni na ninawatakieni kila la heri.
 
Back
Top Bottom