Nafikiri tatizo ni kwamba watu wanashindwa kuelewa mbeba maboksi ni mtu wa aina gani na yule mla vumbi pia. Ni yule mtu ambae "by chance" ameingia Ughaibuni na anachakarika.
Mbeba maboksi ni yule mtu ambae yupo Ulaya (hasa kwa UK) ama kwa muda mfupi (mwanafunzi) au mrefu (wale wenye ukaazi wa kudumu na wanashindwa kupata kazi nzuri kutokana na sifa haba) na anafanya kazi katika maeneo mbalimbali kwa mfano kwenye maghala, viwandani, ujenzi, uyaya, utunzaji wazee na wasiojiweza na hulipwa ujira kulingana na masaa anayofanya (worker) iwe ni GBP kuanzia (kwa sasa) 5.73 hadi 11 kwa saa.
Malipo kwa vibarua huchukua kati ya wiki au wiki mbili na unaweza kuishia na kati ya 250 au 350 GBP hizi ukiangalia na uchumi wa Tanzania utajua ni kiasi gani mtu anapata.
Mla au wala vumbi sijui ni walio katika kundi gani kwa hio sitaingia sana huko mpaka pale mtu yeyote atakaponipa maelezo kwamba ni watu wa aina gani.
Sasa tukirudi kwa mbeba maboksi utaona kwamba ukipata pesa ya ujira wa kazi yako hapo inabidi uzingatie vitu muhimu kama pango la chumba au nyumba ambayo utakuwa unachangia na wabeba maboksi wenzio, nauli ya kusafiria au kulipia mafuta ya gari kama unalo, bills za simu, gesi na umeme na kama ulichelewa kuwaambia watu wa halmashauri kwamba wewe ni mwanafunzi basi itabidi ulipe Council Tax.
Pamoja na mambo mengine mengi tu ukifika mwisho wa mwezi kulingana na kipato chako, ndio unaangalia masuala kama Western Union kwa ndugu nyumbani TZ na projects zozote kama utakuwa nazo huko.
Sasa kwa wale wenye ukaazi wa kudumu au "indefinite leave to remain" kama inavyojulikana au uraia kabisa, mambo ni mazuri kiasi kwenye masuala fulanifulani kama vile shule ambako utakwenda kwa hiari yako na fee haitakusumbua kwa maana kwamba itabidi uchukue mkopo.
Pia kwenye masuala ya nyumba kidogo kuna unafuu kwa kuzingatia kwamba sheria kwa sasa inawaangalia sana wale wenye ILR na raia wa UK kuliko wale wenye "time limit".
Sisi binadamu tunapofanya kitu chochote chenye kuwa na "positive impact"
naona kuna vitu vitatu ambavyo kwa kiingereza naviita motive, means and opportunity.
Kwa hio aidha uwe ughaibuni au Tanzania ukiweza kuangalia motive au dhamira yako ni nini je ni kuishi Ughaibuni na kutengeneza maisha ya Tanzania na utakuwa na nyenzo gani iwe ni elimu, au ajira na pia kama kuna "opportunity" au nafasi ya kufanya hayo au utaendelea kuishi katika mazingira ambayo hayamnufaishi kila mtu basi utakuwa na matokeo mazuri au mabaya.
Ukiangalia wale watanzania ambao wamesomeshwa na serikali katika nchi mbalimbali duniani ingawa ni kwa shida sana, wengi wao wameweza kurudi nyumbani na kuingia katika mazingira yaleyale walioyaacha ya ukiritimba wa kupita kiasi, rushwa na madudu mengine na wao kuwa sehemu ya "system" ileile. Ila kwa watanzania wengine tuishio ughaibuni tunaamini kwamba maendeleo yataletwa kwa kuonesha mfano na baadhi yetu wamekwishaonesha hayo.
Kwa hio nikihitisha maoni yangu hapa naona kwamba ni kheri mtu anaeishi Ughaibuni akitengeneza dorali au paundi huku akijenga nyumbani kwa kuwekeza na kuwa na vitega uchumi ingawa anakuwa na barriers kibao ambazo zinajulikana.
Beef haitakuwa kubwa baina ya makundi haya kwa kuangalia impact itakayokuja kutokana na mwamko wa mheshimiwa mtarajiwa Mwakalinga ambae ameonesha njia na sie wengine tupo nyuma kuwekeza Tanzania katika nyanja mbalimbali na mwishoe kuisimamisha nchi yetu kutoka katika dimbwi la ujinga uliotukuka.
Nnapenda kuona kwamba wale waliopo nyumbani Tanzania wanaelewa kwamba Ughaibuni mambo ni mswano tu kama utajitahidi kusoma au kwenda professional na ili ulipwe si chini ya GBP 1500 kwa mwezi kwa kazi za kawaida tu.
Pia tusisahau kwamba wale waishio ughaibuni wana exposure kubwa sana, na ukiangalia mfumo mzima wa kodi unavofanya kazi, mfano tu kwenye suala la kodi ya maendeleo huwa napenda sana.