Wabeba mabox vs wala vumbi: Chuki ya nini??

Wabeba mabox vs wala vumbi: Chuki ya nini??

wekezeni makwenu bana!taifa linajengwa na vijana,wataalamu wa nyanja mbali mbali!sio unaenda kusoma ki mastaz chako ukimaliza unaamua kubaki hukohuko UBEBE BOKSI,kisa bongo kuna njaa!.........

Mojawapo ya tatizo kubwa linalowakabili waTz ni kushindwa kuelewa wanachosema wengine na matokeo yake mijadala mingi inapoteza mwelekeo na kubakia ushabiki na vuta nikuvute ya watoto wa chekechea.
 
Kwani kujenga taifa wewe una ku-define vipi? Nachukia sana mijadala isiyosogea!

Igeni mfano wa Mwakalinga mkuu tunajua Taifa lina nguvu kazi nyingi sana kwenye mataifa ya wenzetu huko lakini mkiwa na umoja mkawekeza nyumbani hata sisi tutatoka tu. Tunashindwa resources mzee ndo maana wajanja watatuzunguka hapo.
 
Fidel80;

Hapana; popote penye kuwezesha mkono uende kinywani ni poa tu ndugu yangu.

Tuheshimiane tu bila kujali uwezo.

FP
 
poa wakuu!tupo pamoja sana,ila ni lazima tuelezane ukweli
 
Fidel80;

Hapana; popote penye kuwezesha mkono uende kinywani ni poa tu ndugu yangu.

Tuheshimiane tu bila kujali uwezo.

FP


Cha muhimu mkuu mapesa mnayo pata huko majuu njooni muwekeze nyumbani kama wanavyo fanya wenzetu Rwanda hapo nenda Kenya nao hivyo hivyo. Si mnaona mwenzetu Mwakalinga alivyo wekeza Kyela? Watu wamepata ajira pale tayari.
 
Semilong;

Nadhani umekuja TZ miaka ya zamani sana au haupo connected. Miaka ileee kulikuwa hakuna makampuni ya kigeni. Kulikuwa na kampuni na mashirika ya umma.

Baada ya makampuni ya kigeni kuingia tumeona kwa sasa kuna vijana below 40 years ambao ni ma CEOs, kuna wa UBA (sijui wamebadili jina?) na kuna Kenya commercial bank na wengineo (barcklays bank pia ni kijana).

Haya makampuni ya kigeni yanazingatia uchapa kazi wako sio kitu kingine, matokeo yake wabongo kibao wana nafasi nzuri na salaries za above 5000 Usd kwa mwezi kwenda mpaka 12,000 Usd (may be zaidi ila sina mfano wa above that)bila marupurupu kama nyumba , gari etc.

Sasa kama wewe unaona hizo salaries hazitoshi kuja kuwaangalia wabeba mabox basi una matatizo au umeamua tu kuwa mmbishi.

Uliza jamaa zako wa bongo watakwambia..

naona una hisi tu mambo na hujui mimi niko wapi
1. ceo is not an average tanzanian, ie walavumbi. pili hao ma ceo wako wangapi???? compare to 40m polpulation.
kumbe unafananisha wabeba mabox na ma-ceo waTZ?
2. ninavyojua mimi kampuni kubwa karibuni zote ma ceo wake ni wageni TBL, nmb, nbc, voda, cement, kasoro CRDB. na sababu kwa ajili waTZ tunaonekana sio wachapa kazi. kwenye hayo makampuni ya kati kama kcb, barrick nk hao wa ceo wako wangapi 100? tunajua waHindi wote wameweka ma ceo wahindi
3. how many people in TZ earn above $5,000 let alone $12,000?
unajua wabeba mabox ni watu wa hali ya chini sio hata middle class na wanaweza kuafford hivyo vitu vyote holiday, owning a home na nk. kumbe wewe unawafananisha na ma-ceo waTZ , nakubali ma ceo wa nchi yeyote wanaweza kwenda kokote kule but ma ceo sio average tanzanian..
inaonekana unaufahamu sana kuna ma ceo wangapi watu weusi TZ kwenye medium to large companies
 
Fidel80;

Uwekezaji unataka moyo. Sio kila mtu ni Mzalendo.

Naomba kuongezea neno hapa. Binafsi kama ningelijaaliwa mtaji wa maana ningaliwekeza sehemu ambayo italipa bila kuangalia mambo ya uzalendo. Nadhani mambo ya uzalendo yalikwisha malizwa pale Azimio la Arusha lilipowekwa kando. Sasa hivi mambo ni ubepari kila mmoja na lwake. Kutokana na hilo limenifanya kuwa na fikra za kibepari na naamini good investment haitakiwi iwe compromised na utaifa.
 
Shame on you. Unakuja hapa kusifia UFISADI? Unajua WTZ wangapi wanakufa kwa njaa kila siku kwa sababu ya watu kama nyinyi mnaondekeza UFISADI? Shame on you.

Bahati mbaya hujanielewa, ungekuwa umesoma sentensi yangu ya mwisho ungekuwa umejua nasema nini? Nachosema ni hivi, sasa hivi Bongo kuna pesa za nje nje na ndio mana vija mnaowaita wala Vumbi wana pesa na ndio maana hawana adabu mbele ya mbeba BOX. Wana pesa, mnataka kulazimisha hoja, ukweli ni kuwa nchi ina UFISADI na hii ndio sababu kuna watu wachache wana make na walio wengi wanateseka na hao mnaokutana nao ndio wale walio kwenye nafasi ya kumake.
 
**************************************************************
Je mmeacha kuchambia kopo???

Hoja hujibiwa kwa hoja! Nimejaribu kuyakinisha kwanini kumekuwa na chuki na chuki ilianza lini lakini naona mkuu umekosa hoja, kama hapa ni mahali pa wenye kufikiria nje ya box mbona huna majibu.

Nipe sababu za kuchukiana zilianza wapi, naweza kuwataja hata wana JF waliopo mtoni hapa kwenye Forum yetu wanaojaza mapost daily na wanashindanishwa maisha na walio waaacha bongo, kasumba ya kuona kuwa Ulaya na Marekani ndio kuna maisha imepitwa na wakati.

wengi wanaishi maisha ya kukimbizana na dakika na bills zisizo na vichwa wala miguu. Wale walioko Bongo, waliopata upenyo wa kupata deal ziwe za halali au sio halali wamewin, sasa kwa kuwin kwao wakaanza kuwaona wenzao walioonda mtoni hasa kwa kufoji mavyeti wamechemsha na ndipo walipoanza kuwaponda, umenielewa, najaribu kuonyesha wabeba box walianza kudharauliwa na wala vumbi lini na kwanini, It does not mean I am supporting corruption, Google mbogela and corruption then you will get my record men!
 
Bahati mbaya hujanielewa, ungekuwa umesoma sentensi yangu ya mwisho ungekuwa umejua nasema nini? Nachosema ni hivi, sasa hivi Bongo kuna pesa za nje nje na ndio mana vija mnaowaita wala Vumbi wana pesa na ndio maana hawana adabu mbele ya mbeba BOX. Wana pesa, mnataka kulazimisha hoja, ukweli ni kuwa nchi ina UFISADI na hii ndio sababu kuna watu wachache wana make na walio wengi wanateseka na hao mnaokutana nao ndio wale walio kwenye nafasi ya kumake.

Hizo hela za hao vijana unaodai wana hela ni hela zinazopatikana kiujanja ujanja, kifisadi fisadi tu. Bongo kumejaa vitapeli tapeli kibao. Ujinga mtupu! Kazi nzuri zinapatikana kwa kujuana au kubusiana makalio. WTF! It pissess me off
 
Siku hizi kumekuwa kuna tabia ya mtu ukitoka nje ukimuambia mtu kitu hata kama ni cha ukweli yeye ananga'ng'ania kubisha na kukuita mbeba box
unakuta unamuambia mtu kutokana na wewe umeona upande mwingine wa dunia lakini hataki kukusikiliza sio kama yeye anahoja hapana bali ni kutaka kukuletea zarau...
Na wengi wanakua wanaongea kwa chuki sana huku wakikuita mmbeba box

cha kujiuliza kwa nini kumekuwa na chuki kati ya wabeba mabox(watz wa nje) na wala vumbi(watz walioko tz)????

Kwanza lugha yako mwenyewe iko divisive.

Si kila mtanzania aliye nje ni mbeba box, kuna watu wanafundisha vyuo vikuu na kufanya kazi professional jobs sehemu kama Wall St na Silicon Valley.

Si kila Matanzania aliye nyumbani ni mla vumbi, kuna watu wanafanya mambo makubwa. Hii mentality ya kuruhusu kuwagawanya watu katika mafungu kirahisi kama nyanya rojo na nyanya fresh inachangia tatizo badala ya kutatua tatizo.

Heri nusu shari kuliko shari kamili, kama unafikiri mtu anakudharau ya nini kujihusisha naye?
 
Hizo hela za hao vijana unaodai wana hela ni hela zinazopatikana kiujanja ujanja, kifisadi fisadi tu. Bongo kumejaa vitapeli tapeli kibao. Ujinga mtupu! Kazi nzuri zinapatikana kwa kujuana au kubusiana makalio. WTF! It pissess me off

Now you are talking!
Kweli mkuu, sio tu pesa za ujanja ujanja hata kazi na tender zinatolewa kwa unamjua nani au utamfaidisha nani na nini? Na hapo ndio walipo pata vichwa hawa wana wa Mafisadi, na wao kuwadaharau wale walio nje kwani walipo rudi waliwakuta waliokuwa hapa nchi wamemake zaidi ya aliyekuwa amesafiri.

Lakini kumbuka jambo lingine muhimu lililowashushia heshima wabeba box ni miaka ya 90 vijana wengi wasio na sifa kufoji docu na kuingia front, na walipofika huko hawakusoma wala hawakuqualify kwa kazi nzuri, sasa hawa jamani tutawalinganisha na nani Bongo?
 
Hilo la vitu feki bongo usiseme,wizi mtupu.Mfano hai energy saving bulbs bongo life yake haizidi miezi 3 hadi minne.Nilibahatika kupata free sample energy saving bulbs( British Gas switch to Green Promo )leo miaka bado zinadunda,labelled 10 years life based on 10,000 hours

Ingawa nakubali bongo vitu chupri, mambo mengine ni stereotypes zetu zina ya enforce tu.

Hizi bulbs matoleo ya kwanza yalikuwa na matatizo karibu dunia nzima.
 
The truth is a majority of Africans who immigrate to the U.S. do manual labor na wana kua kwenye welfare ukilinganisha na immigrants toka nchi nyingine say za Asia ambao wao ni 1% ya immigrants but they are the biggest tax contributors of all immigrant groups. Hizi stereotype za ubeba mabox ina tokana na ukweli usio fichika kwamba majority of Africans in the U.S. and Europe are not blue collar workers(siyo wote).
mbona hii sentensi imekaa kushoto
blue collar workers naona haiendani na hii sentensi
blue collar workers ni watu ambao wanafanya manual labour na wabeba mabox ni watu wanaofanya manual labour, kwa hiyo wabeba mabox ni blue collar workers...
najua bongo blue collar workers ni class ya watu kastamu, benki na nk

ungesema are not white collar workers....
 
Kwanza lugha yako mwenyewe iko divisive.

Si kila mtanzania aliye nje ni mbeba box, kuna watu wanafundisha vyuo vikuu na kufanya kazi professional jobs sehemu kama Wall St na Silicon Valley.

Si kila Matanzania aliye nyumbani ni mla vumbi, kuna watu wanafanya mambo makubwa. Hii mentality ya kuruhusu kuwagawanya watu katika mafungu kirahisi kama nyanya rojo na nyanya fresh inachangia tatizo badala ya kutatua tatizo.

Heri nusu shari kuliko shari kamili, kama unafikiri mtu anakudharau ya nini kujihusisha naye?
lugha yangu iko divisive kwa ajili jumuiya iko divided. this is how they call one anaother...
najua si kila mtanzania ni mmbeba box na si kila mtz ni mla vumbi, lakini hata wabeba box wanastahili heshima na walavumbi wanastahili heshima
 
wabeba box mbona mna hasira.......?? tuacheni na vumbi letu.....tumeshalizoea karibuni kuna party ya ushindi wa kamanda zombe....
 
Mimi nadhani kuna jelousy fulani watu walio bongo wanaifeel kwa watu ambao wapo nje, nasema hivyo kwa sabu hiyo term Mbeba Boxi inatumika TU kwa watu wanaofanya kazi nje.
Hata siku moja sijawahi kuona mtu anayefanya manual labour bongo akaitwa maneno ya kejeli, lakini ukifanya nje taabu! Hiyo Mla Vumbi inatokana ni defensive response ya wabeba box, na wao si lazima wapate cha kusema bwana!
 
Yap Party imeanza hapa natamani ningekuwa na simu zenu na majina halisi niwaite hapa!
 
alafu mkimaliza kubeba hayo maboksi mrudi na hela muwekeze nyumbani kwenu!CLEAR?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom