Waarabu wameleta maendeleo, uungwana na ustaarabu Zanzibar

Waarabu wameleta maendeleo, uungwana na ustaarabu Zanzibar

Mzanzibari Huru

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2014
Posts
393
Reaction score
234
Wapenzi wanajamii

Katika mwaka 1806 wenyeji wa Zanzibar, ambao walikuwa na asili ya Kiomani na Kishirazi walikwenda huko Sultanate ya Kiomani na kumuomba baba wa wafalme waadhimu, wakarimu, waungwana, wenye kuona mbele, Sayyid Said Al Said, (Mungu ailaze roho yake palaha pema na kumpa pepo ya firdaus na waja wengine wema na weye msomaji uitikie ameen) kuja Zanzibar kuwaondoshea watawala makatili wa Kireno waliokuwa wakifanya vitendo vya kinyama hapa visiwani kwetu.

Baada ya kuwashinda maadui wakubwa wa Zanzibar kwa wakati huo, Wareno. Wanzibari wakauona, ujasiri huruma, ukarimu na ukakamavu wa Sayyid Said na wakamuomba aendelee kukaa na kuvilinda Visiwa vya Zanzibar ili wahuni wareno wasije kurejea tena.

Mnamo mwaka 1832 akafika tena Zanzibar na nia ya kuviboresha visiwa vyetu. Hapo nyota ya jaha ya Zanzibar ikaanza kung'ara, maisha yakaanza kubalidika, mandeleo yakaanza kuingia kwa kasi kubwa sana. Mnamo mwaka 1836, Umarekani wakaamua kufungua ofosi ya kibalozi Zanzibar, balozi wa kwanza alikuwa Bw Richard Waters, kutoka Salem, Massachusetts. Balozi ya Uengerza ilifunguliwa mwaka 1841 Bw Atkins Hamerton akawa ndie balozi wa kwanza. Balozi za Ufaransa 1844, Ujerumani, Austria-Hungary 1885, Italy na Belgium 1849

Baada ya kifo cha baba etu kipenzi cha mioyo yetu Sayyid said, mtoto wake Sayyid Baraghash, mjasiria mali, aliyepevuka katika utawala, aliyeipendelea Zanzibar kuwa katika nchi bora duniani alileta maendeleo makubwa sana, mfano umeme mwaka 1883, hapo Zanzinar ikawa ni katika nchi za tatu duniani kuwezesha matumizi ya umeme. Sultan Barghash alikuwa ni mtawala wa kwanza Afrika kuweka lift katika nyumba, lilikuwa lift lilovumbuliwa na Bw Elisha Otis, hapo ilikuwa ni 1883. Akaleta kilimo cha hali ya juu, aliagizia mikarafuu, minazi, miembe, na miti mengine kutoka bara la Asia.

Baada ya kifo chake, tunamuomba Mungu aibariki roho yake na kuipa pepo ya Firdaus, watalawa walikuwa ni wa muda mfupi mfupi lakni mtoto wake akatawala na kukakataa utawala wa Kiingereza Zanzibar, kama kawaida yao wazungu, wakaamua kufanya fujo la kijeshi na vita baina ya Sultan Khalid bin Barghash na serikali ya Uingereza vilipiganwa. Vita vilodumu kwa muda wa dakika 45 tu na ni vita vinavyotambulikana katika historia ya dunia kama ndio vita vifupi vyao duniani.

Katika mwaka 1890(the Heligoland-Zanzibar Treaty of 1890) Coastal area za Tanganyika zilikodishwa kwa wajerumani kwa miaka 99. Mikataba iliwekwa saini baina ya Sultan Ali Bin said na the German East Africa Company. Siku yoyote Zanzibar ikipata uhuru wake kamili eneo hilo la Zanzibar lililopo Tanganyika litarudi kwa Zanzibar mmiliki wake asilia. Nyaraka za kodi zipo

Katika mwaka 1893 Mombasa na coastal area za Kenya zilikodisha kwa Waengerza kwa muda wa miaka 99. Siku yoyote Zanzibar ikipata uhuru wake kamili maeneo hayo yatarudi kwa mwenyewe asilia Zanzibar. Nyaraka za kodi zipo.

Ilipofika mwaka 1896 Zanzibar tayari iliweka huduma za simu. Kwa upande wa bara la Afrika ilikuwa ni Misri, Afrika Kusini na zanzibar tu ndio wenye huduma hizo. Zanzibar ilikuwa ni katika nchi 35 duniani waliokuwa wanatumia huduma za simu.

Zanzibar ilikuwa ni katika nchi tajiri zaidi katika bara la Afrika, yenye elimu ya hali ya juu na ustaarba usio kipimo. NASA waliweka Tracking Station pale Tunguu 1960. Kituo hiki kilifungwa baada ya serikali ya Zanzibar kuingia katika mikono ya Waafrika.

Kwa ufupi tu, ustaarabu, uungwana, ukweli, uzalendo na upendo wa Waarabu ulidhihirika sana hapa Zanzibar. Kuja kwao hapa za zanzibar ilikuwa ni neema kubwa sana.

Ahsanteni.
 
20141018_MAP004_0.jpg

☝🏿
Ati.

Huo ni Ungwana?
 
Katika mwaka 1806 wenyeji wa Zanzibar, ambao walikuwa na asili ya Kiomani na Kishirazi walikwenda huko Sultanate
Huo ni upotoshaji.

Unawajua Wapemba/Wa-Bemba?

Unadhani kulikuwa na sababu zipi za msingi za Rais wa Msumbiji kufika Zanzibar?

=====

Muwe na shukurani kwa Baba wa Taifa la Zanzibar.

John Okello.

Okello kwa Dakika chache, kwa lugha na 'Lafudhi" yake, aliwaondoa Wanyanyasaji wa Kiarabu!

Katika mwaka 1806 wenyeji wa Zanzibar, ambao walikuwa na asili ya Kiomani na Kishirazi walikwenda huko Sultanate

Sayyid Said Al Said, (Mungu ailaze roho yake palaha pema na kumpa pepo ya firdaus na waja wengine wema na weye msomaji uitikie ameen)
Ameen...na aendelee kupata kichapo cha kaburi, na akifufuka, achapwe tena na kurudishwa Jehanam.
 
Hakuna upotoshaji hapo.
Huo ndio ukweli, labda uwe na history yako ya uzushi.
Unaelewa maana ya Wazenji?

Hao walikutwa karne ya 7 kisiwani humo. Jiridhishe

Kwanini kilichoandikwa hapa usiwe upotoshaji?
 
Wapenzi wanajamii

Katika mwaka 1806 wenyeji wa Zanzibar, ambao walikuwa na asili ya Kiomani na Kishirazi walikwenda huko Sultanate ya Kiomani na kumuomba baba wa wafalme waadhimu, wakarimu, waungwana, wenye kuona mbele, Sayyid Said Al Said, (Mungu ailaze roho yake palaha pema na kumpa pepo ya firdaus na waja wengine wema na weye msomaji uitikie ameen) kuja Zanzibar kuwaondoshea watawala makatili wa Kireno waliokuwa wakifanya vitendo vya kinyama hapa visiwani kwetu.

Baada ya kuwashinda maadui wakubwa wa Zanzibar kwa wakati huo, Wareno. Wanzibari wakauona ujasiri huruma, ukarimu na ukakamavu wa Sayyid Said na wakamuomba aendelee kukaa na kuvilinda Visiwa vya Zanzibar ili wahuni wareno wasije kurejea tena.

Mnamo mwaka 1832 akafika tena Zanzibar na nia ya kuviboresha visiwa vyetu. Hapo nyota ya jaha ya Zanzibar ikaanza kung'ara, maisha yakaanza kubalidika, mandeleo yakaanza kuingia kwa kasi kubwa sana. Mnamo mwaka 1836, Umarekani wakaamua kufungua ofosi ya kibalozi Zanzibar, balozi wa kwanza alikuwa Bw Richard Waters, kutoka Salem, Massachusetts. Balozi ya Uengerza ilifunguliwa mwaka 1841 Bw Atkins Hamerton akawa ndie balozi wa kwanza. Balozi za Ufaransa 1844, Ujerumani, Austria-Hungary 1885, Italy na Belgium 1849

Baada ya kifo cha baba etu kipenzi cha mioyo yetu Sayyid said, mtoto wake Sayyid Baraghash, mjasiria mali, aliyepevuka katika utawala, aliyeipendelea Zanzibar kuwa katika nchi bora dubniani alileta maendeleo makubwa sana, mfano umeme mwaka 1883, hapo Zanzinar ikawa ni katika nchi za tatu duniani kuwezesha matumizi ya umeme. Sultan Barghash alikuwa ni mtawala wa kwanza Afrika kuweka lift katika nyumba, lilikuwa lift lilovumbuliwa na Bw Elisha Otis, hapo ilikuwa ni 1883. Akaleta kilimo cha hali ya juu, aliagizia mikarafuu, minazi, miembe, na miti mengine kutoka bara la Asia.

Baada ya kifo chake, tunamuomba Mungu aibariki roho yake na kuipa pepo ya Firdaus, watalawa walikuwa ni wa muda mfupi mfupi lakni mtoto wake akatawala na kukakataa utawala wa Kiingereza Zanzibar, kama kawaida yao wazungu, wakaamua kufanya fujo la kijeshi na vita baina ya Sultan Khalid bin Barghash na serikali ya Uingereza vilipiganwa. Vita vilodumu kwa muda wa dakika 45 tu na ni vita vinavyotambulikana katika historia ya dunia kama ndio vita vifupi vyao duniani.

Katika mwaka 1890(the Heligoland-Zanzibar Treaty of 1890) Coastal area za Tanganyika zilikodishwa kwa wajerumani kwa miaka 99. Mikataba iliwekwa saini baina ya Sultan Ali Bin said na the German East Africa Company. Siku yoyote Zanzibar ikipata uhuru wake kamili eneo hilo la Zanzibar lililopo Tanganyika litarudi kwa Zanzibar mmiliki wake asilia. Nyaraka za kodi zipi

Katika mwaka 1893 Mombasa na coastal area za Kenya zilikodisha kwa Waengerza kwa muda wa miaka 99. Siku yoyote Zanzibar ikipata uhuru wake kamili maeneo hayo yatarudi kwa mwenyewe asilia Zanzibar. Nyaraka za kodi zipo.

Ilipofika mwaka 1896 Zanzibar tayari iliweka huduma za simu. Kwa upande wa bara la Afrika ilikwa ni Misri, Afrika Kusini na zanzibar tu ndio wenye huduma hizo. Zanzibar ilikuwa ni katika nchi 35 duniani waliokuwa wanatumia huduma za simu.

Zanzibar ilikuwa ni katika nchi tajiri zaidi katika bara la Afrika, yenye elimu ya hali ya juu na ustaarba usio kipimo. NASA waliweka Tracking Station pale Tunguu 1960. Kituo hiki kilifungwa baada ya serikali ya Zanzibar kuingia katika mikono ya Waafrika.

Kwa ufupi tu, ustaarabu, uungwana, ukweli, uzalendo na upendo wa Waarabu ulidhihirika sana haopa Zanzibar. Kuja kwao hapa za zanzibar ilikuwa ni neema kubwa sana.

Ahsanteni.
Mbona hujaongelea kuhusu utumwa? Halafu unaeleza kama vile waarabu walikuja zanzibar kwao na nchi haikua na mwenyewe. Waarabu walileta dhiki na utumwa tu. Kama ni maendeleo ni ya kwao wenyeji walipoteza heshima utu na uhuru wao. Ni ajabu mtu unakuja na uzi kama huu. Unajiamini kwa vile ni mbaguzi unajua binadamu ni waarabu. Ukome kutujia na propaganda za aina hii.
 
Kwa nini kuna historia ya mapinduzi mpaka kukawa na mapinduzi ya masaa 48.
Au unamsifia kizimkazi wako idd mama kwa watanganyika
Fbn

Nakushukuru sana kwa suala lako elimivu.

Mapinduzi yaliofanyika Zanzibar, mwaka 1964, ni mtiririko ule ule wa aina ya manduzi yaliofanyika katika nchi nyengine za Kiafrika. Wazungu wote wakiwemo Waingereza, Wafaransa, wabelgiji na Wareno wamekuwa wakiendesha kapeni kama hizi dhidi ya viongozi waliokuwa na msimamo wa nchi zao kwanza, waliopata uhuru kutoka katika makucha yao machafu. Wazungu walikuwa na triki mbili, ikiwa wameshinda kuwachochea majeshi kufanya mapindui basi wanatafuta mbinu za kumuuwa kiongozi aliyepewa uhuru. Na hapo Bara la Afrika likawa limajaa mapinduzi au vifo kwa viongozi waliopinga ukoloni mambo leo. Utasema kwanini Mwalimu Nyerere hakupinduliwa na alikuwa katika hotuba zake akisema sana kuhsu ukoloni mambo leo? Yeye alikuwa kibaraka wa Roman Catholics, ambao ni Wazungu wale wale tu.

Tukija kwa upande wa Zazniabr, visiwa vyetu adhimu hazikuwa vinatawalia direct na Wazungu kwahivyo mfalme na serikali yake alikuwepo. Zanzibar ilikuwa ni protectorate. Waingereza walijuwa wazi na kushangazwa sana kwamba Wazanzibari wanamthani zaidi mfalme wao kinyume na walivotaka iwe. Kwahivyo wakaamua kuwauwa mauwaji ya halaiki ya raia kuliko kutaka kumkamata au kumuua mfalme.

Walilofanya Wazungu ni kuwaleta ma mia ya Watanganyika waliokodiwa kwa kazi ya kuuwa na kufanya mauwaji ya halaiki kwa raia, Waarabu wasio na hatia wafikao 17,000 waliuliwa usiku mmoja na wakazikwa katika mashimo ya halaiki. Vikosi vya mauwaji vililetwa Zanzibar kupitia Tanga. Mfalme na familia yake watu wa karibu yake waliruhusiwa kuondoka, na meli ya Kiingereza iliwachukuwa kutoka Mombasa Kenya hadi Portsmouth Uk.

Kukupa hadithi yote refu hiyo ni kutaka ujuwe kwamba Wazanzibari hatukuthubu wala hatuwa na sababu ya kusaliti Sultan wetu adhimu, waliofanya mapunduzi ya mauwaji ya halaiki walikuwa ni Wazungu wakiwatumilia Watanganyika.

Kuanzia hapo 1964 Zanzibar ikaanza kutawalia na Wabara, wengine wakiwa kutokea Malawi, wengine kutokea Tanganyika. Hadi leo hii. Mzanzibari asilia yaani Mwarabu hawezi kuachiwa kuiongoza Zanzibar. kama unavyojuwa waarabu ni makini sana katika uongozi na hilo limedhihirika Zanzibar. Hii ndio maana tuko hahe hohe.
 
Mh kwa maendeleo gani? Au yale magofu?
 
Maendeleo yapi wakati Juzi mgonjwa kapelekwa hospitali kwa msaada wa Makuti?
Shadow 7

Nafikiri unazungumzia Zanzibar ya leo. Hilo ulolisema ni matokeo ya kuatawaliwa na Waafrika. Sisi Waafrika tukiweka mkono wetu katika jiwe la dhahabu linageuka shaba. Tuchukulie mfano huko kwenu Tanganyika, 60% ya ardhi yenu haijwekwa mguu wa binadabu, bado mumebarikiwa na wingi wa Maziwa, Mito, ya ukubwa wa kila size na mvua za mara kwa mara. Ingekuwa munalima kilimo cha kiwango cha biashara basi mungeweza kuilisha Afrika na Middle East nzima peke yenu. Lakini hamuonekanani kwamba munajuwa umuhimu wa raslimali yenu ya ardhi na mito na maziwa.

Bahari mulonayo, uchumi wenu ungetegea samaki kama vile Faroe Island. Lakini ni la kushangaza sana munaagizia samaki kutoka Uchina.

Tizama maadini mulobarikiwa, sekta ya maadini pekee ingekuwa inaendesha maisha ya Watanganyika wakipata mshahara wa chini kiwango kama dola 10,000. Leo hii tunasikia porojo tu kuhusu maadini wakiwemo gesi asilia na mafuta.

Siku ikifika bara la Afrika kutawaliwa tena, tuombe Mungu waje waarabu kututawala, mambo yatakuwa poa sana.
 
Mh kwa maendeleo gani? Au yale magofu?
Lavit

Wewe kama Mtanganyika huwezi kujuwa maana ya neno maendeleo maana kwenu hakujafika lolote tunaloweza kusema ni mendeleo, labda maendeleo ya ubadhiru na wizi wa pesa za umma
 
Hakuna Maendeleo Yameletwa na waarabu Zanzibar.

Maendeleo Zanzibar ni matokeo ya Fedha na Nguvu Kazi Kutoka Tanganyika.
 
Hakuna Maendeleo Yameletwa na waarabu Zanzibar.

Maendeleo Zanzibar ni matokeo ya Fedha na Nguvu Kazi Kutoka Tanganyika.
Kirchhoff

labda makala yangu hukuisoma nyema au hukuifamahu. nakuomba uirejee kama unao wakati.

Nimesema kuanzia 1964 Zanzibar ikaanza kutawaliwa na Waafrika yaani Watanganyika. Ndio shida ilipoanza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom