Waarabu na wahindi tangu utotoni wanafundishwa biashara, mbongo anasubiriwa hadi afike 25. Kuna haja ya kuendelea kumtafuta mchawi ?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,086
Na ndio chanzo kikubwa cha biashara nyingi zilizofanikiwa kuanza kuyumba pale baba akifariki kila kitu kinaparanganyika.

Unakuta familia tayari inajiweza kiuchumi inaingiza makumi ama mamia ya mamilioni kila mwezi lakini wazazi wanawakomalia watoto kusoma tu na matuisheni utadhani sio familia ya biashara, matokeo yake hapa hata mtoto hajui chochote kuhusu biashara anaanza kutamani hata kuajiriwa kwa mshahara wa kawaida tu na haya mambo tumeshuhudia sio ya kuandika tu.

Familia ya kibiashara inabidi iwe na damu ya biashara, watoto ni lazima waandaliwe mapema sana kuanza kuwa involved na biashara, nakuhakikishia kwamba hata kama mtoto kaishia darasa la saba, kama aliandaliwa mapema kwenye biashara huyo kakosa tu elimu lakini kwenye suala la kuchapisha pesa ni mashine hii, binafsi nimesoma na wasomali, wapemba, waarabu, n.k. elimu holaaa!! lakini kwenye biashara hawagusiki. ntoto anamjua supplier, mtoto anawajua tayari watu wa clearing pale bandarini, documents kashacheza nazo sana, malori ya usafiri anayajua tayari, n.k.

Uje kwa wabongo sasa utafurahi, mzazi with full onfidence anajipiga kifua mbele ya watu eti anasibiri mtoto hadi afikie 25 ndio aanze kumhusisha, isi this ideal at all kweli jamani, mtu mzima huyo tayari ulikuwa wapi muda wote kummegea experience yako afaidike tangu akiwa mtoto? khaa!!
 
Back
Top Bottom