Orodha ya ndoto karibia zote na maana yake.

kufanakupona

JF-Expert Member
Jun 18, 2015
522
417
NDOTO ZA UTAJIRI
1. 777
-Kuota vitu mafungu 3 kila fungu vipo 7.
2. UNAHIFADHI PESA SEHEMU SALAMA.
Sehemu salama kama kwenye kopo, droo, benki n.k
3. Kuokota pesa za sarafu za zamani.
4. Unafanya mtihani na umefaulu kwa alama za juu hadi unasifiwa.
5. Mwanamke kuota amejifungua mtoto wa kike ilhali si mjamzito, au mwanaume kuota mpenzi wake amejifungua mtoto wa kike.
6. Umekuwa rais au mtu mkubwa na watu wanakushangilia na kukuheshimu
7. Umepanda mlima mrefu sana kwa tabu na ukafika kileleni juu kabisa, ulipofika ukajikuta una hamu ya kukaa huko na usirudi tena ulikotoka.

NDOTO ZA DALILI MBAYA
1. UNAHESABU PESA
Nyota yako ya utajiri imeshaibiwa na wachawi.
2. UNAWAONA WATU WALIOKUFA
Tayari na wewe unaandamwa na roho ya umauti, unatafutwa kuuawa kivyoyote.
3. UMEYARUDIA MAISHA YA UTOTONI AU UNASOMA SHULE WAKATI USHAMALIZA ZAMANI
Unafuatiliwa na roho ya kuanguka, ni dalili ya kufungwa na roho za mizimu na mababu.
4. UNAFUKUZWA NA MAADUI
Wachawi wanakutumia kwenye mambo yao pasipo wewe kujijua.
5. UNAKULA USINGIZINI/NDOTONI
Umepandikizwa roho za kichawi na za mizimu mwilini mwako.
6. UNAFANYA MAPENZI
Unamilikiwa na jini mahaba.

NYOKA MWEUSI
~Ni jini ambaye ametumwa na wachawi na amekuingia mwilini
NYOKA ANAPAA ANGANI
~Ni jini aliyetumwa kwako kichawi, ni aina ya Twayyaara na amekuingia mwilini
KUFUKUZWA NA NYOKA
Unaandamwa na adui wa kichawi ambaye anatumia majini mabaya kukuangamiza
NGAMIA
Ni jini mkubwa mwenye nguvu katika majini.
NGAMIA AMEKUSIMAMIA NYUMA:
~Bado hajakuingia mwilini mwako ingawa anakuwinda.
NGAMIA AMEKUSIMAMIA MBELE:
~Tayari ameshakuingia mwilini
FARASI AU PUNDA
Ni jini ambaye hajatumwa na mtu yeyote, ila amekuingia mwilini kwa kukupenda, au kwa sababu anazozijua mwenyewe.
MBWA AU MBWA MWITU
Ni jini mbaya sana ambaye amekuingia, ana madhara makubwa kwa mwili na afya yako, lakini jini huyu ni dhaifu sana kwa mbinu wanazotumia majini, ukipata tabibu mzuri ni rahisi kuondoka.
SAMAKI AU CHOCHOTE CHA BAHARINI
Ni jini Ghawwaas, anapenda kuishi sehemu zenye majimaji kama bahari, chemchem, mito, madimwi na mabwawa na amekuingia mwilini.
SOKWE, NYANI, AU NGEDERE
Ni jini ambaye amekuingia na kuweka uchawi mwilini, ni majini wanaopenda sana kufanya mikataba ya makubaliano ya kuwatumikia wachawi katika kazi mbalimbali, lakini ni jini muoga sana anapokutana na wataalam wa tiba.
SIMBA
Ni jini kafiri, mkorofi na jeuri, ana madhara makubwa kwa mgonjwa na mtabibu, kama mtabibu si mjuzi wa kutosha
JINSIA ZA BINADAMU
Unafanya mapenzi na mtu unayemjua au humjui, iwe mpo katika furaha, huzuni.
Huyo ni jini mahaba.

ALIYEKUFA ANASWALI
Zimemfikia thawabu za matendo yake aliyokuwa akiyatenda duniani enzi za uhai wake.
ALIYEKUFA ANAKUAMBIA UTAKUFA
Wakati mwingine kauli yake huwa ni kweli, MLANGO UNAANGUKA
Muotaji ataugua kwanza halafu atapona.
UNAFUNGA MLANGO WA NYUMBA YAKO
Utampa talaka mke wako.
MSUMARI AU DARAJA
Mtu anayesaidia watu katika kutatua matatzo yao
KUPANDA NGAZI, MBAO AU MOTA
Utapata cheo, hadhi kubwa duniani
NYUMBA YAKO IMETEKETEZWA
Utasumbuliwa na wenye mamlaka au ugonjwa wa mlipuko.
ALIYEKUFA ANAKUPA MAWAIDHA AU ANAKUFUNDISHA
Utapata wema katika dini yako kwa kiasi cha mawaidha uliyopewa.
UNAMUOA MWANAMKE ALIYEKUFA
Utafanya jambo litakalokufanya ujute.
UNAFUFULIWA (PEKE YAKO AU NA WENGINE)
Wewe ni dhalimu.
UMEINGIA JEHANNAM
Utafanya madhambi makubwa, aliyesababisha uingie motoni ndiye atakayekupeleka kwenye mambo machafu.
JINI AMESIMAMA KARIBU NA NYUMBA YAKO
-Udhalili (unyonge)
-Hasara
-Nadhiri uliyoiweka
MAJINI WAMEINGIA NYUMBANI KWAKO NA KUFANYA MAMBO
-Wezi wataingia nyumbani kwako na kukudhuru.
-Maadui zako watavamia nyumba yako.
MSICHANA AMEJIPAMBA KIISLAM
Utaskia habari zitakazokufurahisha katika njia ambayo hukuitegemea.
MSICHANA YUPO UCHI
Utapata hasara katika biashara zako.
UNACHIMBA KABURI
Utajenga nyumba.
UMESIMAMA JUU YA UKUTA
Hadhi na nafasi yako.
UKUTA UNAPOROMOKA
Utakuwa ni kiongozi wa uharibifu.
KUUZA NYUMBA
Kufikia kikomo cha maisha.
KUBEBA MLIMA
Utabebebshwa mizigo mikubwa na watu wakorofi na wakali.
UNAPANDA KUELEKEA SEHEMU YA JUU
Kupata heshima, kutukuzwa na kupanda cheo.
MIAMBA NA MAWE
Ugumu wa moyo, ukorofi, ukatili na kiburi.
CHANGARAWE
Usengenyaji na kutoa shutuma dhidi ya mtu fulani.
MCHANGA, VUMBI AU UDONGO UNAKURUKIA
Utakuwa tajiri jitume sana katika kazi zako.
UNATEMBEA JUU YA MCHANGA AU KUOKOTA MCHANGA
Utafanya kazi ngumu za sulubu ili kuwa na mali.
MCHANGA AU VUMBI KURUKA HEWANI AU MBINGUNI.
Mambo yatavurugika.
MTOTO WA KIUME
Ni adui dhaifu ambaye atakuja kama rafiki kisha atadhihirisha uadui wake.
KWENU KUMEZALIWA WATOTO WENGI WA KIUME.
Majonzi na huzuni.
AJUZA AMEJIPAMBA NA AMEJIFUNUA
Utapata dunia yako na biashara za haraka
AJUZA AMEKUNJA USO
Kuondoka kwa daraja ya juu kwa mambo yako ya kidunia
AJUZA ANA SURA MBAYA
Mambo yako yatageuka
AJUZA YUPO UCHI
Kufedheheka.
USO WAKO NI MWEUSI KULIKO SEHEMU ZINGINE
Mkeo atazaa mtoto wa kike
UMEKATWA SHINGO KWA UPANGA NA USIYEMJUA
Utapona ugonjwa, utalipa deni, utahiji, utashinda vita, utapata faraja.
UMEKATWA SHINGO NA UNAYEMJUA
Vyote vitapitia kwake.
MWANAMKE KUOTA AMENYOLEWA
Ni ishara ya kifo au ataachwa
MWANAMKE KUOTA AMENYOLEWA NA MUMEWE
Mumewe atamfungia nyumbani kwake, hakika ndege hubakia kiotani wakati amenyonyolewa mbawa zake
UNASIKILIZA KWA MACHO NA KUONA KWA MASIKIO
Utampelekea binti yako au mkeo kufanya maasi
KIGANJA CHAKO KINA JICHO AU NYAMA
Utapata mali
KUANGUKA KISIMANI
Utakumbwa na huzuni na masikitiko mwishowe utapata furaha
KUZAMA KWENYE MAJI SAFI YA BAHARI
Utazama katika mambo ya utawala na serikali.
KUZAMA KWENYE MAJI MACHAFU YA BAHARI
Utapata tabu itakayokusababishia kuangamia
MWANAMKE ASIYEOLEWA KUOTA ANA NDEVU
-Hatozaa milele.
-Maradhi ambayo yatampata siku za usoni.
-Ziada ya mali ya mumewe na utukufu wa mwanawe wa kiume.
MWANAMKE ALIYEOLEWA KUOTA ANA NDEVU
Mumewe kuondoka
MWANAMKE MJAMZITO KUOTA ANA NDEVU
Atazaa mtoto wa kiume na litatimia jambo lake
MWANAMKE KUOTA ANA NDEVU ZIMEREFUKA NA KUWA NYINGI
Umri wake utakuwa mrefu na mali yake itazidi
kuongezeka
UNA MASKIO MATATU
Mke mmoja na mabinti wawili
UNA SIKIO NUSU
Kifo cha mkeo na utaoa mwingine baada yake
UNA MASIKIO MANNE
-Utakuwa na wake wanne
-Mabinti wanne wasiokuwa na mama
MASIKIO YAKO YAMEJAZWA VITU NDANI YAKE
Utakufuru
MENO YANAVUNJIKA
Utalipa deni kidogokidogo
MENO YANADONDOKA NA UNAHISI MAUMIVU
Kuondokewa na kitu katika vitu vilivyomo ndani mwako
MENO YAKO YA MBELE TU YANADONDOKA
Unazuiwa kufanya jambo lako ulilokuwa ukilifanya aidha kwa vitendo au maneno
KITU KINATOKA MDOMONI MWAKO
Utapata riziki, iwe ya halali au haramu.
UNA ULIMI MREFU
Kushinda katika ufasaha wa kuongea na adabu yako, upole na utukufu.
ULIMI WAKO UMEFUNGWA
Ufukara na maradhi
UNA MENO MEUPE NA MAZURI
Nguvu na mali ya daraja ya juu kwa watu wa nyumbani mwako
MWENYE ELIMU AKIOTA ANA MENO YA DHAHABU
Sifa nzuri.
ASIYE NA ELIMU AKIOTA ANA MENO YA DHAHABU
-Shari
-Watu wake watapata maradhi au kuangamia.
UNA MENO YA FEDHA
Kupata hasara katika mali yako,
UNA MENO YA KIOO
Umauti.
UNALISHA MASKINI
Utatoka kwenye majonzi na utapata amani kama ulikuwa na hofu.
UNASWALI KATIKA ALKAABA
-Utapata baadhi ya watukufu na viongozi
-Utapata amani na kheri.
UMEKUFA NA KUFUFUKA
Utafanya madhambi na utamuomba Mungu msamaha.
UNAKUFA BILA KUUMWA
Umri wako utakuwa mrefu.
UMEKUFA, WATU WANAOMBELEZA NA KUKUFANYIA SHUGHLI ZA MAZISHI
Dunia yako itakuwa nzuri lakini ahera yako imeharibika.
MAITI INAJIOSHA YENYEWE
Watu wako watatoka kwenye majonzi na mali yao itazidi
UNAONA SANDA
Zinaa
SANDA IMEVISHWA LAKINI HAIJAKAMILIKA UVAAJI WAKE
Utatiwa kwenye zinaa lakini hutokubali UMEFUNGWA KWENYE SANDA VILEVILE KAMA MAITI
Kifo chako.
UPO KWENYE JENEZA
Utajenga udugu na mtu kwa ajili ya Mungu UPO KWENYE JENEZA NA WATU WAMELIBEBA
Utatawala na kupanda daraja na watu watakufuata kama ulivyowaona ndotoni
UMEBEBA MAITI
Utapata mali ya haramu
UNAMPELEKA MAITI SOKONI
Utapata mahitaji yako na faida kwenye biashara zako
JENEZA LINAPITA HEWANI
Atakufa mtu mwenye cheo kikubwa katika nchi
UMEKUFA NA UNAZIKWA
Utasafiri safari ya mbali na utapata mali
UMEMFUFUA MAITI
Utamshuhudia mtu wa dini nyingine kuwa dini yako, au mtu muovu atatubia dhambi zake kwako
DADA YAKO ALIYEKUFA ANAISHI
Utajiwa na mgeni kutoka safarini na utafurahi

1) unakula kabeji= utapata maradhi ya kujitakia.
(3) unaona karanga= vurugu haziishi nyumbani
(4) umevaa nguo mpya= utazawadiwa
(5) umevaa nguo nyeusi= utapata mikosi.
(6) umevua nguo safi= utapata hasara
(7) umevua nguo chafu= mikosi ita kuondoka.
(7) Unavaa nguo zilizo chanika= utapatwa na aibu
(8) umevaa nguo za mapambo/maua=utapata furaha.
(9) unaendesha kigari cha farasi= utakua ombaomba.
(10) unachoma mkaa= utaoa mwanamke alie achika.
(11) umepata mafua= una maadui wa kisirisiri.
(12) umeona mahindi= utapata faida katika shughuli zako.
(13) uko kwenye ukumbi wa muziki = utapata habari nzuri toka kwa rafiki yako wa karibu. (14) kiza kinene= utadanganywa au utatapeliwa.
(15) mfungwa kuota giza kisha mwanga=atafunguliwa
(16) ambaye si kuota giza kisha mwanga=mambo yake yatafunguka.
(16) uko msibani= harusi, ikijirudiarudia una jini maiti.
(17) jinni limekudhuru au umeliogopa kupita kiasi= kuna hatari mbeleni. (18) unachimba shimo na kisha likapotea=kukosa mazao, utafukuzwa kazi, kukosa mvua. (19) unatumbukia shimoni= utapata mikosi na utateseka sana kimaisha. (20) unavuka mto kwa kutumia gogo= utapata watetezi katika mambo yako, utashinda kesi kwa msaada wa mtu. (21) umemuona dragon = utapata utajiri kwa njia za kishirikina
(22) umemuona chatu= utapata utajiri.
(23) Mwanaume akiota anaona nguo ya kike imeanikwa= atapatwa na mabalaa. (24) unakunywa maji kwa mkono wa kushoto wakati jua linachomoza=utapata maradhi. (25) unalewa pombe kupita kiasi= utapata marafiki wa maana na pia ni mafanikio kimapenzi. (26) unazama ndani ya maji =kupata mikosi.
(27) unamuona mtu anazama ndani ya maji=mikosi yako itaisha.
(28) unaona funza= kaa chonjo kuna maadui.
(29) unakula= mikosi.
(30) unalishwa kitu= ni kweli umelishwa.
(31) umekufa kwa kupigania dini= amali zako ni njema.
(32) unakunywa maziwa= utapata mafanikio.
(33) mkeo ana matiti makubwa= utapata mafanikio.
(34) mbalamwezi inang'aa= utapata furaha na mafanikio
(35) umepoteza pesa= utapata hasara kibiashara.
(36) umepata hela = mafanikio ila si kuokota.
(37) unaokota hela= utapata mikosi.
(38) umekunja chuma= umewashinda maadui.
(39) nyota inang'aa wakati huo una mchumba= mtafarakana na mchumba wako. (40) nyota imeanguka= afya njema.
(41) umemuona bata mzinga= ndoa yenu ni ya mafanikio na mtapata watoto wengi. (42) unang'oka jino= utapoteza rafiki wa karibu.
(43) Ukiota umeng'oka meno ya mbele= utapoteza marafiki wengi na ndugu watakuchukia. (44) unakunywa maji masafi= utapata furaha.
(45) unakunywa maji machafu= matatizo yanakunyemelea.
(46) unaona mamba= utapata maumivu.
(47) unachomwa mwiba= utapoteza pesa.
(48) radi inapiga= mafanikio katika biashara.
(49) radi imekupiga= umekumbwa na jini.
(50) umemuona kobe= biashara zako zitaenda polepole
(51) unakula kobe= mtarekebisha tofauti zenu za ndoa.
(52) Mwanamke alie achika akiota anafunga ndoa= ni mikosi.
(53) Mgonjwa akiota anafungandoa na mwanamke aliyeachika= atakufa. (54) Unalia= ni furaha na upendo.
(55) Mgonjwa akiota anafunga ndoa na msichana ambaye hajaolewa= atapona (56) unaona karatasi nyeupe= utapata mke wa maana na watoto wa heri. (57) unachana karatasi= utaendekeza umalaya.
(58) unatembea katika barabara iliyonyooka= mafanikio mbele yako, afya njema. (59) Mwanaume akiota anamuona tausi= atapata mke mzuri na atatajirika. (60) Mwanamke akiota anamuona tausi= atapata mwanamme tajiri ila ni mwongo mwongo. (61) unamuona bundi= mikosi na vifungo
(62) njegere zimepikwa= mafanikio.
(63) unakula mkaa= utapata mikosi.
(64) unaona vitunguu= utapata habari njema.
(65) Mwanaume akiota anaona vitunguu= atapata mwanamke mwaminifu ila ni mwenye hasira. (66) unachimba kaburi= jini maiti, pia kuna tabia unayoifanya si nzuri itakuingiza katika wakati mgumu. (67) unalima kwa ng'ombe= mafanikio.
(68) watu wanalima na ng'ombe lakini zinazama= mavuno mabaya.
(69) watu wanalima juu ya mlima= utapoteza mifugo.
(70) umepewa tunda damu chachu=utagombana na rafiki yako.
(71) Tajiri akiota anasali= furaha
(72) Maskini akiota anasali= matatizo na mikosi.
(73) Mwanaume akiota anachota maji kisimani= ataoa.
(74) Mwanamke akiota anachota maji kisimani= ataolewa.
(75) unakunywa wiski= mikosi, mabalaa, majuto.
(76) upepo wa kimbunga= utaoa mke mwenye makelele.
(77) Tajiri akiota amebeba mbao= mikosi
(78) Maskini akiota amebeba mbao= bahati.
(79) una andika=jihadhari na kauli zako.
(80) unapiga miayo= rafiki zako wamekuchoka.
(81) unaona kitu chochote cha njano= mafarakano katika mapenzi yenu. (82) unamuona pundamilia= kua mwangalifu katika maisha yako.
(83) watu wanapiga tarumbeta= utapata mikosi na matatizo.
(84) unaona ndimu= utapata ugomvi au kutukanwa.
(85) unaona mwanamke bikra= utapata habari njema.
(86) Maskini akiota anatapika =atapata pesa
tajili akiota anatapika=atafilisika.
(87)vita= matatizo na huzuni.
(88)unamuona mama mkwe= utaugua.
(89)unaongea na mama yako vizuli= uta fanikiwa kwa lolote.
(90)mpishi yuko ndani ya nyumba= utao mwanamke wa
maana na kama una matatizo.
Yataondoka.
(91) Mgonjwa akiota anamuona mpishi= hali yake itakua
mbaya.
(92)unaona kisu= mafaninio. (93)unamuona paka utaibiwa.
(94)paka amekuuma= utaletewa habali za uongo.
(95)unakula keki= furaha na mafanikio.
(96) mshumaa unawaka kasha ukazimika= mambo yako
yatahalibika pia ni ishala ya kufilisika.
(97) Mgonjwa akiota mshumaa umawashwa = atapona.
(98) mshumaa ambao haujawashwa= utapata zawadi nono.
(99) unaona watoto wengi ndani ya nyumba=kufungika kwa
kizazi
(100)unakunywa kahawa= marafiki zako ndo maadui zako.

Mtoto wa kiume:
-Mtu asiyekuwa na heshima,
-Adui,
-mali iliyofichwa,
-ushirikina,
-mabadiliko
-uwezo
-kiongozi mbaya
Mwanamke:
-mtu anayeishi Bondeni,
-Uadui kutoka kwa wakwe zako, watoto au ni wivu kutoka kwa majirani zako. Ukimuona nyoka:
utadanganywa na mkeo au mumeo.
Unapigana na nyoka:
kuwashinda au kuwapindua adui zako.
Unakimbizwa na nyoka: uadui unaokujia kutoka kwa adui yako.
Umemuona nyoka mwenye vichwa saba:
ni ishara ya kutenda dhambi au makosa makubwa.
Unamuona chatu anakushambulia:
mwanamme au mwanamke mwenye uwezo
ambaye ni adui yako atakusumbua sana. Kama ameshindwa kukuumiza: utapewa sifa za uongo.
Umemuua chatu:
kuwashinda maadui zako.
Chatu amejikunja:
-kupatwa na hatari au kifungo, kupata maradhi na kuchukiwa na watu. Chatu amelala:
adui aliyelala hasa kwa mtu ambaye ni muovu.
Nyoka wa kwenye maji:
utapokea msaada au utapata uamuzi kuhusu jambo lako.
Unafuga nyoka au unamiliki nyoka: kupata uwezo au madaraka.
Nyama ya nyoka:
-fedha za adui
-kupata furaha.
Umevaa ngozi ya nyoka:
utamgundua adui yako.
Umemuua nyoka na damu yake ikakurukia kwenye mikono:
utamshinda vibaya adui yako.
Umemwona nyoka anauliwa barabarani: kutokea vita au ugomvi.
Nyoka mdogo:
matatizo kwa mtoto wako au mtoto yeyote unayemhudumia au kumsaidia. Unawinda nyoka:
utamdanganya adui yako.
Nyoka mweusi:
adui yako mwenye nguvu.
Nyoka mweupe:
adui mnyonge.
Nyoka anakusemesha na anakuambia maneno mazuri:
utapata bahati ya kukaa vizuri na adui zako na utanufaika nao.
Nyoka anakusemesha na anakukaripia kwa maneno makali:
adui yako atakutesa na kukunyanyasa.
Umegeuka nyoka:
utatoka dini yako na kwenda dini nyingine.
Umegeuka nusu nyoka na nusu mtu:
utafanikiwa kupunguza nusu ya nguvu za adui yako.
Umegundua ngozi ya nyoka ambayo imetengenezwa kwa dhahabu:
utagundua mali iliyofichwa.
nyoka anakumeza:
kupata madaraka makubwa ya uongozi.
Nyoka amekukalia kichwani:
kupata heshima kubwa kutoka kwa watu wenye madaraka au viongozi. Uwanja mkubwa uliojaa nyoka:
itanyesha mvua kubwa ambayo italeta madhara.
Nyoka mwenye pembe:
kupata mafanikio ya kibiashara.
Nyoka mweusi na chatu:
viongozi wa kijeshi.
Nyoka wa majini:
pesa au utapata pesa.
Shamba lako limejaa nyoka:
utapata mazao mengi msimu huo.
Nyoka anaondoka nyumbani kwako:
nyumba yako itavunjwa.
Umemuua nyoka:
-ndoa
-utawashinda adui zako na wote wanaokuchukia.
Unakula na nyoka meza moja: utatengana na rafiki yako.
Umemwona nyoka wa jangwani:
mtavamiwa na majambazi.
Nyoka amekufa:
Umeepushwa na uadui na shari yake
Nyoka mdogo:
kupata mtoto
Umemuua nyoka juu ya kitanda chako:
utafiwa na mkeo
Umemuua nyoka kwa fimbo:
utaoa
Umemuua nyoka kwa jiwe:
kupona uchawi uliyonao na kutoka kwa jini mwilini mwako
umemuuwa nyoka kwa upanga na kumgawa vipande vitatu:
utamtaliki mkeo talaka 3
Joka kubwa linajizongazonga mwilini mwako:
jini alioingia mwilini anatafuta sehemu ya kujificha
nyoka anaungua kwa moto:
kufanya kazi kwa maombi aliyofanyiwa mgonjwa
unafukuzwa na nyoka:
Jini aliyekuingia hajakaa vizuri mwilini mwako, au ni jini Afriti, jini mbaya anakuandama
Una nyoka shingoni mwako ukamkata kata:
utatoa talaka kwa mkeo
Kuota nyoka mara kwa mara:
una Jini mahaba anakuandama mwilini mwako.
Umetumbukizwa kwenye Kisima:
Ndugu zako wanataka kukutendea uadui, lakini kwa uwezo wa Mungu hawatafanikiwa. Ndege amekudondoshea jiwe kichwani: Unaonywa kuwa unafanya yaliyovuka mipaka hivyo utaangamia. Ndege anaokuambia kitu:
Habari anayokuambia ni ya kweli hivyo unatakiwa uifanyie kazi haraka. Unakurupuka na ukaambiwa kiama!,watu wengi wanakwenda wasipopajua: unapewa onyo kuna jambo linalomchukiza Mungu
unalifanya acha mara moja.
Kitu chochote chenye ncha kali:
habari mbaya za kifo, au kufungwa, ugonjwa, kufukuzwa kazi, kuibiwa, kutapeliwa, moto Kitu chochote chenye kung'ara au cheupe:
kupata “bahati nzuri au mambo mazuri"
kitu chochote kichafu au kisichopendeza: kupata bahati mbaya au mkosi. Unapanda juu kwa njia yoyote:
kupata mafanikio ya kimaisha, kadri unavyozidi kupanda ndiyo mafanikio yatakuwa zaidi. Unashuka au unaanguka kwa njia yoyote ile:
kukwama na kupata pingamizi katika mambo yako, kadri
unavyozidi kwenda chini ndio kiwango cha kuharibikiwa kwa
mambo yako
Unafurahi:
mafanikio
haufurahi:
kupata bahati mbaya.
Kabati limejaa:
mambo yako yatakuwa mazuri.
Kabati tupu:
mambo yako yatakuwa mabaya.
Maji yametulia:
mafanikio na bahati nzuri, utashinda kila kitu.
Maji ynye mawimbi:
Ugumu wa mambo na matatizo.
Maji machafu:
bahati mbaya. Katika jambo lako lolote unalotaka kufanya.
Pingamizi mfano Ukuta, mlango, kufuli,
dirisha, bonde, milima, au uzio:
Ugumu na upinzani katika mambo yako Mlango unafunguka kirahisi:
kupata upinzani mdogo,
Mlango unafunguka kwa tabu:
pingamizi kali au ugumu mkubwa katika
mambo yako.
Unalia:
-utacheka
-utapata hasara katika jambo lako lolote.
Una woga:
utapata ujasiri.
Umekua:
utapata umasikini.
Umepoteza:
utapata.
Unakula nyama:
punguza kusengenya watu.
unaona watu wanakula nyama:
Unasengenywa, angalia kasoro zako.
Unacheza karata= utapata bahati
Unakula kabeji= utapata maradhi ya kujitakia.
Unaona karanga= vurugu haziishi nyumbani.
Umevaa nguo mpya= utazawadiwa
Umevaa nguo nyeusi= utapata mikosi.
Umevua nguo mpya= utapata hasara
Umevua nguo chafu= mikosi itakuondoka.
Unavaa nguo zilizo chanika= utapatwa na aibu.
Umevaa nguo za mapambo/maua= utapata furaha.
Unaendesha kigari cha farasi= utakua ombaomba.
Unachoma mkaa= utaoa mwanamke aliyeachika.
Umepata mafua= una maadui wa kisirisiri.
Umeona mahindi= utapata faida katika
shughuli zako.
Uko kwenye ukumbi wa muziki = utapata habari nzuri toka kwa rafiki yako wa karibu. Kiza kinene= utadanganywa au utatapeliwa.
Mfungwa akiota giza kisha mwanga=atafunguliwa
Ambaye si mfungwa akiota giza kisa mwanga=mambo yake yatafunguka.
Uko msibani= harusi.
Mara kwa mara uko msibani = una jini maiti.
Jini limekudhuru au umeliogopa kupita kiasi= kuna hatari mbeleni. Unachimba shimo kisha likapotea=kukosa mazao, utafukuzwa kazi, kukosa mvua. Unatumbukia shimoni= utapata mikosi na utateseka sana kimaisha. Unavuka mto kwa kutumia gogo= utapata watetezi katika mambo yako, utashinda kesi kwa msaada wa mtu. Umemuona dragon= utapata utajiri kwa njia za kishirikina
Umemuona chatu= utapata utajiri.
Mwanaume kuona nguo ya kike imeanikwa=atapatwa na mabalaa.
Unakunywa maji wakati jua linachomoza kwa mkono wa kushoto= utapata maradhi. Umelewa pombe kupita kiasi= utapata marafiki wa maana na pia ni mafanikio kimapenzi. unazama ndani ya maji =mikosi.
Unamuona mtu anazama ndani ya maji=
mikosi yako itaisha.
Unaona funza= kaa chonjo kuna maadui.
Unakula= mikosi.
Unalishwa kitu= ni kweli umelishwa.
Umekufa kwa kupigania dini= amali zako ni njema.
Unakunywa maziwa= utapata mafanikio.
Mkeo ana matiti makubwa= utapata mafanikio.
Mbalamwezi inang'aa= utapata furaha na
mafanikio
Umepoteza pesa= utapata hasara kibiashara.
Umepata hela = mafanikio ila si kuokota.
Unaokota hela= utapata mikosi.
Umekunja chuma= umewashinda maadui.
nyota inang'aa wakati huo una mchumba=
mtafarakana na mchumba wako.
Nyota imeanguka= afya njema.
umemuona bata mzinga= ndoa yenu ni ya
mafanikio na mtapata watoto wengi.
unang'oka jino= utapoteza rafiki wa karibu.
umeng'oka meno ya mbele=utapoteza marafiki wengi na ndugu watakuchukia. unakunywa maji safi= utapata furaha.
Unakunywa maji machafu= matatizo
yanakunyemelea.
unaona mamba= utapata maumivu.
unachomwa mwiba= utapoteza pesa.
Radi inapiga= mafanikio katika biashara.
Radi imekupiga= umekumbwa na jini.
Umemuona kobe= biashara zako zitaenda plepole
Unakula kobe= mtarekebisha tofauti zenu za ndoa.
Mwanamke aliyeachika akiota anafunga ndoa= mikosi.
Mgonjwa akiota anafunga ndoa na mwanamke alie achika= atakufa.
Unalia= furaha na upendo.
Mgonjwa akiota anafunga ndoa na msichana ambae hajaolewa= atapona, Unaona karatasi nyeupe= utapata mke wa maana na watoto wa heri. Unachana karatasi= utaendekeza umalaya.
Unatembea katika barabara iliyonyooka=
mafanikio mbele yako, afya njema.
Mwanaume akiota anamuona tausi= atapata mke mzuri na atatajirika. Mwanamke akiota anamuona tausi= atapata mwanaume tajiri lakini ni mwongo mwongo. Unamuona bundi= mikosi na vifungo
Njegere zimepikwa= mafanikio.
Unakula mkaa= utapata mikosi, dalili ya umelishwa kitu.
Unaona vitunguu= utapata habari njema. Mwanaume akiota anaona vitunguu= atapata mwanamke mwaminifu ila ni mwenye hasira. Unachimba kaburi= jini maiti, pia kuna tabia ambayo unayoifanya si nzuri itakuingiza katika wakati mgumu. Unalima na ng'ombe= mafanikio.
Watu wanalima na ng'ombe lakini zinazama= mavuno mabaya.
Watu wanalima juu ya mlima= utapoteza mifugo.
Umepewa tunda damu chachu= utagombana na rafiki yako.
Tajiri akiota anasali= furaha
Maskini akiota anasali= matatizo na mikosi.
Mwanaume akiota anachota maji kisimani= ataoa.
Mwanamke akiota anachota maji kisimani= ataolewa.
Unakunywa wiski= mikosi, mabalaa, majuto.
Upepo wa kimbunga= utaoa mke mwenye makelele.
Tajiri akiota amebemba mbao= mikosi
Maskini akiota amebeba mbao= bahati.
Unaandika=jihadhari na kauli zako.
Unapiga miayo= rafiki zako wamekuchoka.
Unaona kitu chochote cha njano= mafarakano katika mapenzi yenu. namuona pundamilia= kua mwangalifu katika maisha yako.
Watu wanapiga tarumbeta= utapata mikosi na matatizo.
Unaona ndimu= utapata ugomvi au kutukanwa.
Unaona mwanamke bikra= utapata habari njema.
Maskini akiota anatapika= atapata pesa tajiri akiota anatapika= atafilisika. Vita= matatizo na huzuni.
Unamuona mama mkwe= utaugua.
unaongea na mama yako vizuri= utafanikiwa kwa lolote.
Mpishi yuko ndani ya nyumba= utaoa mwanamke wa maana, matatizo yako yataondoka. Mgonjwa akiota anamuona mpishi= haliyake itakua mbaya.
unaona kisu= mafanikio.
unamuona paka=utaibiwa.
paka amekuuma= utaletewa habari za uongo.
unakula keki= furaha na mafanikio.
mshumaa unawaka kisha ukazimika=
mambo yako yataharibika, kufilisika.
Mgonjwa akiota mshumaa umewashwa = atapona.
Mshumaa ambao haujawashwa= utapata zawadi nono.
Unaona watoto wengi ndani ya nyumba=kufungika kwa kizazi.
unakunywa kahawa= marafiki zako ndo
maaduizako.
Panya anatoka nje anaingia ndani=mkeo
ni mzinifu.
Umeokota au unacheza na funguo=utapata neema.
Mwili umekosa nguvu, kama umepooza=kupoteza control katika maisha Unaanguka=mambo katika maisha yako hayaendi vizuri kikazi, kimahusiano au masuala ya fedha. Umetoka meno=una uoga wa kujiona hauna mvuto, inaweza kuhusiana na hisia ya kujiona umefedheheshwa na kitu maishani mwako. Unakimbizwa=unaepuka hisia inayokutisha ama ikuumizayo, mtu ama
jambo fulani baya.
Maji=mabadiliko au vitu vipya, kubadilika mambo/vitu katika maisha yako. Vyombo vya usafiri=muelekeo ambao maisha yanatupeleka.
Unajisaidia haja ndogo=utaondokewa na matatizo madogomadogo.
Kuanguka kisimani=Utakumbwa na huzuni na masikitiko mwishowe utapata furaha. Kuzama kwenye maji safi ya bahari=
utazama katika mambo ya utawala na serikali.
Kuzama kwenye maji machafu ya bahari=
utapata tabu itakayokusababishia kuangamia.
Kunguru=mtu fisadi na asiyekuwa na haya.
Kizingiti cha mlango kimetukoea=
mwanamke wako atakutoroka.
Ubavu wako umechomoza= mwanamke wako atakutoroka.
Unakula majani=utakula mtaji wa biashara yako.
Unakula mkaa=utapata maradhi ya tumbo.
Unauza mkaa=utafilisika.
unaingiliwa kinyume na maumbile=adui yako atakushinda.
unamwingilia mwanaume mwenzio kinyume na maumbile=utamshinda adui. mara kwa mara misiba=una majini wachafu.
unapigana na ukapaa=kuna uadui unakunyemelea, wanga wanakuwangia lakini una viumbe wanao kusaidia. visiki vingi viko njiani=kuna watu wanaokwamisha mipango yako.
unakula nyama ya mtu=msengenyaji.
Unapigana na radi kisha ukaishinda=kuna jini alitaka kukuingia lakini kashindwa. unakabwa=huyo ni jinamizi, ila ukimjua anayekukaba huyo ni mwanga.

UNAKIMBIZWA NA WANYAMA WAKALI:
Mashambulizi ya kipepo na nguvu za giza vimejizatiti dhidi ya maisha yako. KUONA DAMU:
-hatari mbele
-kifo na ajali.
MAMA MJAMZITO KUOTA ANAONA DAMU
Mimba yake itaharibika
KUZINGIRWA NA NYUKI:
shambulizi la kiroho na kutofanikiwa kimaisha.
KUOGA:
utakaso wa rohoni (utakatifu).
KUPOTEZA MSAHAFU/BIBLIA:
kurudi nyuma kiroho na kukosa imani.
PAKA:
wachawi wanafuatilia maisha yako.
KUIBIWA TAJI:
-kupoteza umaarufu na kurudi nyuma.
-kushushuka cheo kiofisi, kiuchumi au kisiasa.
MLANGO WA OFISI YAKO UMEFUNGWA:
-utapoteza kibali au kufukuzwa kazi
-biashara yako itakufa
JENEZA:
roho ya mauti inafuatilia maisha yako au umpendaye
AGANO:
kifungo cha kiroho.
MSALABA:
mzigo mkubwa na shida/tabu.
GIZA:
-kuchanganyikiwa na kurudi nyuma.
-kuzorota kiroho.
DENI/KUDAIWA:
kudorora kiuchumi, kufilisika.
KUCHEZA NA MBWA AU KUMBEBA MBWA
roho chafu ya uzinzi
NDUGU ALIYEKUFA:
uwepo wa mzimu wa familia.
(Uwe mwangalifu, unaoweza kuona kama unapewa taarifa muhimu ndotoni, lakini MUNGU hatumii njia za kipepo kusema na watu) KUNYWA POMBE:
kupenda ya dunia
ALAMA ZA KIPEPO:
magereza ya kiroho na kutumikishwa na mapepo.
PUNDA:
ugumu wa mateso au shida katika maisha.
MITIHANI:
majaribu na hali, kipindi kigumu.
KUPAA:
kutawaliwa na wachawi, shambulizi la kiroho, huenda utachanganyikiwa. KUVUA SAMAKI:
kuhubiri neno la MUNGU
MOTO:
kupoteza na majanga.
KUPOKEA MAUA TOKA JINSIA NYINGINE:
Kama siyo mwenzi, huenda huyohuyo ndiye atakaye kuja kua wa maisha KUPIGWA RISASI IKAKUJERUHI:
-udhaifu wa kiroho
-shambulizi na maadui wamejipanga kuharibu maisha yako.
KUPIGWA RISASI ISIKUJERUHI:
ulinzi wa kiUNGU na ushindi juu ya adui zako.
KUVUNA:
Baraka za Mungu.
ASALI:
Afya na mafanikio maishani mwako.
NYUMBA TUPU:
hali ngumu na umaskini.
KUJIFICHA:
maadui wanapigana/wanafuatilia maisha yako lakini uko chini ya ulinzi wa MUNGU. SAFARI ISIYOKUWA NA MWISHO:
unachofanya au unachotaka kufanya itakuwa ni kupoteza muda na nguvu. KUPOTEZA FUNGUO:
Mlango wa baraka zako utafungwa. Hali hiyo ikakuletea hitimisho la mipango chanya, matarijio na matumaini yako kuhusu mafanikio. FUNGUO NYINGI:
Baraka za fursa nyingi zinakusubiri maishani mwako.
KUPOTEZA PESA AU MALI:
-Mambo mabaya
-Wezi wanaweza kuiba pesa au vitu vyako.
-unataka kufanya biashara isiyo sahihi
-kuangukia kwenye mitego ya matapeli na makundi ya mafisadi.
MZIGO:
hali mbaya katika mateso na umasikini.
UNAPEWA MSAADA WA PESA:
kibali, neema maalumu na mpenyo wa kipesa mbele yako.
KUONA MAITI:
mauti inakufuatilia wewe, au inamfuatilia uliyemwona kwenye ndoto. UKICHAA:
-mvurugano katika maisha yako.
-shetani anataka/yuko tayari kukudhuru.
UNACHEZA NA WATU WENYE VICHAA:
shambulizi la kiroho ili kukusambaratishia amani na utulivu. UNAKIMBIZWA NA WAHUNI:
nguvu za giza na wachawi wanajaribu kukuharibu(kukuua).
RUNGU:
nguvu, ukakamavu kiroho na ulinzi wa kiungu.
UNAFUNGA NDOA NA MTU USIYEMJUA:
mume/mke wa kipepo
UNAFUNGA NDOA NA UNAYEMJUA ILA ANA NDOA YAKE:
kufanya kosa kubwa katika ndoa.
UNAFUNGA NDOA NA UNAYEMJUA NA HANA NDOA:
mwenzi wa maisha.
MJAMZITO KUOTA MIMBA YAKE IMETOKA/HARIBIKA:
Asiichuklie kirahisi, inaweza kutokea kiuhalisia.
UCHI/KUVUA NGUO:
aibu au fedheha
UMESHAMBULIWA NA SIMBA UKAFANIKIWA KUMUUA:
umemshinda na kumua mtu aliyekuwa anataka kuharibu maisha yako.
KUONA BUNDI:
-ubaya
-kitu kibaya kitatokea.
MTU UNAYEMJUA ANAKUFUKUZA ANATAKA KUKUUA:
-mtu huyo anaweza kuwa hana mawazo mazuri juu yako.
-wachawi hutumia sura ya mtu yeyote.
UNACHEZA NA NGURUWE AU KUONA NGURUWE:
uchafu kiroho, uzembe na kutokuwa makini katika maisha ya kiroho. SHIMO:
mipango mibaya dhidi yako.
KUCHEZA NA NYOKA:
umefungwa/unatawaliwa na yule nyoka shetani.
KONOKONO:
kudumaa na kuzuiliwa kwa maendeleo au kukua kwa mtu.
SHULE:
unahitaji kupata mafunzo ili kufanya vizuri katika taaluma yako katika maisha. KURUDI SHULE ZA MADARASA YA CHINI:
kudumaa, yaani badala au kupiga hutua mbele unarudi nyuma kimaendeleo. MAJOKA:
umetawaliwa na roho za majini, umeingia au umeingizwa kwenye agano hilo la mapepo/ majini ya pwani baharini au mtoni. NYOTA:
ukuu.
MOSHI:
shutuma na majaribu.
MVUA KUBWA YA MAWE ILIYOAMBATANA NA RADI:
matatizo na kuchanganyikiwa siku za usoni.
KIJIJI CHAKO WAKATI UNAISHI MJINI
laana za mizimu zinajitokeza kukurudisha nyuma.
KUNGURU:
kifo au mauti mbele yako.
MWANANDOA KUPOTEZA PETE YA NDOA:
kuwa mwangalifu sana na ndoa matatizo ya ndoa mbele yako.
UMEPEWA PETE YA NDOA UJANANI:
Utafunga ndoa hivi karibuni, wa ndotoni ndiye mwenzi wako wa maisha KUTEMBEA BILA VIATU:
shetani anataka kukuchanganya kukupa aibu na hali ngumu.
CHAKULA NDOTONI:
unafanya maagano kwenye ulimwengu wa roho, hasa mikataba ya kichawi
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Unahitaji kufunguliwa minyororo ya utumwa wa ushirikina na ujinga.

Ndoto hazina maana yoyote zaidi ya kuwa ndoto. Hata paka wanaota ndoto.
 
Umejitahidi kukusanya hizo habari.

Asante Google Asante mleta uzi.
 
Ndoto zina maana kubwa lakini si kwakukurupuka na tafsiri, maana kwa MUNGU kuna mlango wa ndoto pia hata kwashetani kuna mlango wa ndoto
 
Mi sina bahati ya kuota kabisa,au kwa sababu sijawahi kulala nikiwa sober, daily nalala nikiwa tungi mtu.

Ukichanganya tungi na mchakato Wa ppchi,nikilala nimelala nashtushwa na alarm saa11:45 am.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom