Waandishi wa habari za uchunguzi,chukueni ripoti ya Dk Mwele,ingieni mtaani muwahoji waliopimwa ZIKA

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
Hii ni fursa kwa waandishi wa habari za uchunguzi kuingia "chimbo" wakiwa na ripoti ya dk Mwele Malecela mkononi,waandishi watembelee mikoa na hospitali zilizohusika na utafiti,wawahoji(na kuficha utambulisho)wa madaktari wa mikoa hiyo,ma nesi wa wodi za wazazi,na ikibidi wawasake watoto waliokutwa na dalili za ZIKA,wawahoji wazazi wao,na ikibidi,wapewe nakala ya vyeti kuthibitisha kwamba wamepatikana na ZIKA.

Najua ni mtihani kwa waandishi hasa kipindi hiki ambacho tasnia yao iko machoni pa wakubwa
IMG-20161217-WA0116.jpg
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,791
2,000
Hii ni fursa kwa waandishi wa habari za uchunguzi kuingia "chimbo" wakiwa na ripoti ya dk Mwele Malecela mkononi,waandishi watembelee mikoa na hospitali zilizohusika na utafiti,wawahoji(na kuficha utambulisho)wa madaktari wa mikoa hiyo,ma nesi wa wodi za wazazi,na ikibidi wawasake watoto waliokutwa na dalili za ZIKA,wawahoji wazazi wao,na ikibidi,wapewe nakala ya vyeti kuthibitisha kwamba wamepatikana na ZIKA.

Najua ni mtihani kwa waandishi hasa kipindi hiki ambacho tasnia yao iko machoni pa wakubwa View attachment 447328
Epidemiology ya kawaida inapredict kuwa huwezi kuwa na ugonjwa Uganda usifike Tanzania, ndio maana HIV ilianzia Uganda na kusambaa kwa haraka Kagera being the nearest neighbour!
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,640
2,000
Makala za utafiti zinahitaji jicho la tatu kuzielewa. Hitimisho limesema more research/study is required to ascertain.....
Maana yake bado kuna utafiti unahitajika kuthibitisha matokeo hayo.
Nashindwa kuelewa limempita vipi hili mtafiti Mwele.
Kutoka lugha ya kitafiti ai sayansi kuja kwenye lugha ya kawaida si kazi ndogo.
 
moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,323
2,000
Hakuna sehemu tafiti hiyo imesema watoto walikuwa na dalili za zika,,sampuli (damu) zilizochukuliwa toka kwa watoto hao (15%) zilionyesha virus wa zika.
Hakuna logic ya kuchukua waandishi wa Habari kuwafanyia mahojiano wazazi wa watoto,kinachoweza kufanyika ni kutumia wanataalamu wengine kufanya utafiti ule ule kuthibitisha.
Nb:kumbuka ata hitimisho la tafiti hiyo wamependekeza tafiti zaidi zifanyike.
 
Sasa kama sampuli zinaonyesha wana ZIKA virus,maana yake tayari ZIKA IPO Tanzania

Waandishi wakawahoji hao hao,hasa wazazi
 
moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,323
2,000
Sasa kama sampuli zinaonyesha wana ZIKA virus,maana yake tayari ZIKA IPO Tanzania

Waandishi wakawahoji hao hao,hasa wazazi
Nilikuwa nakusahisha kwenye paragraph uliyosema (watoto walikutwa na dalili za zika )kuna tofauti ukisema watoto walionyesha dalili za zika na ukisema sampuli ya damu kuonyesha virus vya zika.
Huwezi tumia waandishi wahabari kuthibitisha tafiti ya kisayansi.
Cha muhimu ni wewe kukubali ya kwamba ni kweli utafiti huu ulifanyika cha muhimu ni kuthibitisha majibu waliyopata yana ukweli kwa kiasi gani kwa kutumia njia za kisayansi.h
 
Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
9,835
2,000
Kutokana na utafiti kuwa na sociopolitical pressures from a society and politicians including governments hasa kwa ule wa sayansi ya jamii au kuhusisha watu kwenye kukusanya data, mtafiti anatakiwa kuwa na sifa kubwa moja ambayo inazaa nyingine kama ifuatavyo:
1. anatakiwa kuwa 'ethical'/ muadilifu/ kufuata maadili/ miiko ya utafiti
a. an ethical researcher protects research participants,
b. an ethical researcher conducts research honestly in accordance with codes of ethics,
c. an ethical researcher avoids interference from sponsors,
d. an ethical researcher disseminates results in an open, clear manner​
Source: Neuman, 2014, pp. 529-530

Naona kama Dr. Mwele, former CEO of NIMR, kama anazo sifa hizi.
 
ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
9,105
2,000
Hiyo b ....codes of ethics ...naona kama imemuangusha ....... is it ethical to go on public without consultation with a responsible minister?
 
Wamunzengo

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
810
250
Kweli kabisa
Kwa hiyo wakishapata majibu ya kukuridhisha wewe ndo wakuletee uya publicize au.!?

ha ha haaa.! akili zingine buana. Haya buana, washauri wafanye hivyo unavyotaka, wapate matokeo halaf wakuletee wewe tuone utafanya nn.?
 
H1N1

JF-Expert Member
May 29, 2009
4,218
2,000
Makala za utafiti zinahitaji jicho la tatu kuzielewa. Hitimisho limesema more research/study is required to ascertain.....
Maana yake bado kuna utafiti unahitajika kuthibitisha matokeo hayo.
Nashindwa kuelewa limempita vipi hili mtafiti Mwele.
Kutoka lugha ya kitafiti ai sayansi kuja kwenye lugha ya kawaida si kazi ndogo.
...utafiti zaidi ..ni kawaida kuandikwa kwenye tafiti za waelewa ikimaanisha wao sio ukomo wa utafiti
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,033
2,000
Propaganda spreading over my name;
Say you wanna bring another life to shame.
Oh, man, you just a-playing a game
And then you draw bad cyard (draw bad cyard);
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,640
2,000
...utafiti zaidi ..ni kawaida kuandikwa kwenye tafiti za waelewa ikimaanisha wao sio ukomo wa utafiti
Kuna tafiti zina "conclusive" na wanasema hivyo. Si nyingi sana lakini zipo. Lakini kwa utafiti huu, waliweka angalizo kubwa sana. Tatizo lipo kwenye namna ya kuwasilisha matokeo kwa watu ambao si fani yao. Namna ya kuandika hizo policy brief!
 
Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,464
2,000
Hii ni fursa kwa waandishi wa habari za uchunguzi kuingia "chimbo" wakiwa na ripoti ya dk Mwele Malecela mkononi,waandishi watembelee mikoa na hospitali zilizohusika na utafiti,wawahoji(na kuficha utambulisho)wa madaktari wa mikoa hiyo,ma nesi wa wodi za wazazi,na ikibidi wawasake watoto waliokutwa na dalili za ZIKA,wawahoji wazazi wao,na ikibidi,wapewe nakala ya vyeti kuthibitisha kwamba wamepatikana na ZIKA.

Najua ni mtihani kwa waandishi hasa kipindi hiki ambacho tasnia yao iko machoni pa wakubwa View attachment 447328
Hilo unalo lisema ndio lipo linafanyika sasa mkuu watu wako chimbo kwa sasa na sio waandishi pekee hata wewe waweza tu tafuta ukweli ili ujikinge na ZIKA ukisubiri tafiti ndio uanze kujikinga shauri yako.
 
H1N1

JF-Expert Member
May 29, 2009
4,218
2,000
Kuna tafiti zina "conclusive" na wanasema hivyo. Si nyingi sana lakini zipo. Lakini kwa utafiti huu, waliweka angalizo kubwa sana. Tatizo lipo kwenye namna ya kuwasilisha matokeo kwa watu ambao si fani yao. Namna ya kuandika hizo policy brief!
Hivi utafiti huo ukiwekwa kwenye majarida mtafanyaje ? Mtazuia usambazaji wa majarida au mtanunua majarida yote.
Dr. Mwele ni mwathirika wa mikurupuko ya wanasiasa. Akili ya wapi Mimi nifanye utafiti lakini kutangaza utafiti wangu niombe ruhusa ?
Utafiti uliohitimishwa mfano wake ni ule wa HIV kuwa chanzo cha AIDS simply kwa kuwa big brother ana agenda yake na ukimwi lakini madhara yake tutayaishi hadi pale milango ya utafiti kuhusu ukimwi na sababu zake itapowekwa wazi tena.
Dr. Mwele kaonewa
 
Kutangaza matokeo ya utafiti kwenye academic forum au taasisi za utafiti ni tofauti sana na kwenye press conference. Hapo kuna tofauti kubwa sana. Kwenye academic circles unatangaza na kupata challenge kuanzia, results, methods zilizotumika kwa kuwa unakuwa na wataalam wenzio au waliobobea kukuzidi.
Hao wandishi wa habari hawana uwezo wa kutafsiri results toka kwenye majarida ya kisayansi. Si kosa lao. Ndiyo maana huko hawaingii hata wakiyaona majarida!

Conclusion ya utafiti wenyewe ilisema wazi kwamba... more studies required to ascertain the impact of ZIKA virus in the malformation abserved. (Sijatumia exact words lakini hilo ndiyo hitimisho). Mwanasayansi wa calibre ya Dr. Mwele hatakiwi kukurupuka kwa hitimisho kama hilo.
 
Soma vizuri hitimisho ndugu yangu.
Kwani NIMR wao wapo kama gwaride la Jeshi siku ya Uhuru. Sheria iliyowaunda inakataza kutangaza tafiti zao ?
Ni utafiti wa kwanza NIMR kuutangaza kama sio kwa nini huu ndio umekosewa ?
Kwanini hamuweki hiyo code of conduct aliyoivunja ili kuweka wazi ukweli.

Hitimisho la utafiti liko wazi kabisa na halisemi utafiti zaidi kujua ukweli wa kuwapa watz wenye virusi vya Zika Bali kujua athari za virusi vya Zika
Tusipotoshe utafiti
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom