JamiiForums, UTPC kunoa Waandishi wa Habari za Uchunguzi (IJ) na Maslahi ya Umma (PIJ)

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,279
24,150

Alhamisi, Desemba 15, 2022

JamiiForums, UTPC kunoa waandishi 500 wa habari-uchunguzi​


D6310438-D3BC-4EA1-8143-7B0609A27923.jpeg


Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo na Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania ( UTPC), Kenneth Simbaya wasaini mkataba wa ushirikiano kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari za uchunguzi.

UTPC na Jamii Forums wamesema wameingia katika Ushirikiano wa Kimkakati kwa lengo la kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari Nchini katika kuandaa Habari za Kiuchunguzi (IJ) na zenye Maslahi ya Umma (PIJ) ili kuchochea Uwajibikaji na utawala bora

Pia, Waandishi watajengewa uwezo kuhusu Usalama wa Kidijitali, matumizi sahihi na bora ya Vifaa na Mifumo ya Kidijitali na namna bora ya kutumia Uwanja wa Kidijitali kuendeleza kazi zao

Aidha, Mkurugenzi wa JamiiForums amesema litaanzishwa shindano la #StoriesOfChange litakalowalenga Waandishi wa Habari na Washindi watatuzwa baada ya mchujo.

Ushirikiano huu ni miaka 2, utaanza rasmi Januari 2023 na unaweza kuhuishwa baada ya kufanya tathmini.
 
Vema sana siyo waandishi wanakutana na waziri hawamuulizi maswali wanaishia kulamba viatu Kama Mwijaku

Mwigulu alipoita mkutano na waandishi wa habari pale ilibidi apigwe maswali ya ukweli
hahaha utafikiri wapo kwenye kipindi cha kipima joto. mwalikwa anapewa maswali wiki mbili kabla. anayadesa wee kisha anakuja kuyaimba mbele ya bi Farhia midle. hakuna maswali toka kwa watazamaji mwanzo mwisho. ati kipima joto? unapima joto kwa maiti?
 
Huyu pascall mayalla Ni mkongwe na mwalimu ambaye waandishi wengine wanapaswa kujifunza kutoka kwake
Yea Pascal Mayalla anaandika hints fikirishi kuna nazo kuwa nazichukua kuna juzi kaandika Upigaji jeshini yaan walionunua vifaa vibovu nikaenda kufiatilia Suala hilo nilichokuta hatzkadrkfgakeofyzkaveifgzbbkwhrhfsgjwiejxgzkwvrkfhsvsfdioyebdosvakrycjsh
Britanicca
 
Mfano wa(kazi) habari za kiuchunguzi zilizoandikwa na hao wakufunzi ni zipi?

Mnataka kufunza watu kazi za aina hiyo ili waende wapi kuzifanya hizo kazi?

Unadhani ni wapi wanaweza kufanya kazi za aina hiyo?
 
Yea Pascal Mayalla anaandika hints fikirishi kuna nazo kuwa nazichukua kuna juzi kaandika Upigaji jeshini yaan walionunua vifaa vibovu nikaenda kufiatilia Suala hilo nilichokuta hatzkadrkfgakeofyzkaveifgzbbkwhrhfsgjwiejxgzkwvrkfhsvsfdioyebdosvakrycjsh
Britanicca
Hints fikirishi ndio zile za "Baada ya Magufuli Makonda atatufaa" au kuna zingine ?
 
Back
Top Bottom