BelindaJacob
Platinum Member
- Nov 24, 2008
- 6,474
- 4,022
Pasco mkuu, ukatae ukubali siku hizi waandishi bila bahasha hawatoi habari/pichaz..maslahi yamewekwa mbele kuliko taaluma..
Mkuu Ngambo Ngali, kujua nini ni rushwa na nini sii rushwa hauhitaji kuisoma definition, rushwa ni fedha inaotolewa kwa malengo ya kuifluence the natural course of action, sasa hizi bahasha za usafiri, chakula au vikao, ni kwa lengo la kuwezesha, empowering na sio ku influence positive coverage!. Kama uwezeshaji wowote ni rushwa, then Tanzania yote tukula rushwa maana kufuati umasikini wetu, makusanyo yote hayatoshelezi uendeshaji wa nchi, hivyo kuna budget deficit ambayo inakuwa covered the general budget support fung inayotolewa na mataifa ya ulaya, hivyo nchi yetu nzima tunahongwa!.
Usianzishe Jihad vs Crusade, walioanzisha tangu enzi za Continapole wameshindwa itakuwa wewe?. Si unaona jinsi Mazayuni wanavyowatesa ndugu zenu kule Mashariki ya Kati?, si umeona ana wanaopigania Uislamu wanafanywa nini?, amekiona kilichompata Saadam, Osama na juzi juzi Ghadafi?!, bado unataka kutangaza vita?.
Naomba tutafungua thread nyingine tufanye vita kati ya Uislamu na Ukristu, ipi ni dini ya kweli ya Mwenye Enzi Mungu tuone nani atashinda, au hata tuwashindanishe Mtume Mohammed (SAW) na Nabii Issa Bin Maryam (AS) tuone nani ndio mwenye darja ya juu kwa Mwenyenzi Mungu, (Allah subhana wa ta'ala). kwa sasa hebu tujadili hizi bahasha bila kuingiza udini!.
Mkuu Mzalendo80, Pasco wa jf ni mwandishi wa kujitolea wa jf, silipwi chochote na yeyote
Mkuu Lunyungu kwanza pole kwa hii, yote usemayo ni kweli mimi kama mwanahabari, nimeisha vipokea sana hivyo vibahasha na mpaka hapa nilipofika sasa mimi ndio navigawa hivyo vibahasha.
Usitubabaishe kwa maneno, hizo bahasha unalipwa na nani?
Mkuu Mzalendo80, Pasco wa jf ni mwandishi wa kujitolea wa jf, silipwi chochote na yeyote!. Hata utetezi wangu kwa Lowassa, wale mnaoamini nalipwa, kutokana na uwezo wenu wa kufikiri, endeleeni kuamini hivyo maana huo ndio uwezo wa fikra zenu!. Lakini wanaofikiri kwa kutumia logic zaidi, nadhani watakubaliana na mimi kuwa namtetea Lowassa for a reason, na kupitia hiyo reason behind, Lowassa hawezi kunilipa mimi nimpigie debe humu jf!.
5. Jee ni bahasha zipi ni rushwa?.
Baada ya kuzitaja bahasha ni bahasha genuine, sasa nitaziorodhesha bahasha ambazo ni rushwa.
Bahasha ya Kushinikiza Positive Covarage.
Hii ndio bahasha ya kwanza ya rushwa, hutolewa na source ili kuwa entice waandishi wawafanyie favourable covarage. Kwa kawaida bahasha hii inakuwa nene fulani, bahasha hii huandamana na obligation kuwa lazima story itoke. Bahasha hizi za shinikizo la story kutoka hazitolewi kwa waandishi wote, bali to only few selected, na kwa vile bahasha hizi ni rushwa, hutolewa kwa kificho!. Zile bahasha za halali kama za usafiri husainiwa wazi wazi na hukawiwa kila mtu akiona kwa sababu there is nothing to hide, lakini hizi hutolewa kwa kificho, no one will know nani amepokea bahasha na nani hajapokea kutokana mazingira ya usiri. Watoaji wa bahasha hizi wanajua ni rushwa na wapokeaji wanajua ni rushwa!. (to avoid conflict of interest, nawaombeni msiniulize zaidi kuhusu hizi!).
Waandishi na wana siasa wakiongopa hutumia rule ya "proverbial lies wrapped on truth", Pasco wewe unatumia "proverbial lies wrapped on lies".
Hata aje nani hapa huwezi kumkubalisha!
Mkuu Juma Kidogo, kama nilikuambia mpaka serikali na maufisa usalama, wapelelezi wanatembeza bahasha za rushwa halali ili kupata habari!. Hata katika baadhi ya matukio ya uhalifu, uhaini, kuna mshitakiwa katika kundi la wahalifu atakayekubali kukiri na kuwageuka wenzake, anapewa rushwa ya kutoshitakiwa na hivyo kugeuzwa shahidi number moja wa serikali PW1!.Maridadi sana, hapa napata somo kuwa pengine rushwa japo ni kosa kwa sheria za nchi. Lakini kwa upande mmoja wa shilingi inaweza kuwa na faida pia. Hapa tunaona waandishi wa habari za uchunguzi wanaweza kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya kusaka habari nyeti na mara nyingine hulazimika kutoa bahasha ili wapate habari kwa wepesi. Lakini pia hapa kuna jambo dogo nitahitaji msaada kidogo kuhusu matokeo ya faida ya rushwa atoayo mwandishi wa habari za uchunguzi . Kwa mfano: "Ikiwa mimi ni mwandishi wa habari za uchunguzi, nimepata fununu kuhusu taarifa ambazo pengine zinahusu njama zinazotishia usalama wa Taifa. Lakini kwa bahati mbaya yule mtoa taarifa anahitaji apewe bahasha kwanza ndipo anipe habari hiyo. Kwa bahati mbaya wakati nampa rushwa hiyo, jamaa wa Takukuru wananiweka kati na kunifungulia mashitaka ya kutoa rushwa. Mambo yatakuwaje hapo kwa upande wangu ikiwa nilikuwa natoa rushwa ili nipate habari kwa ajili ya maslahi ya Taifa? Je hii ni mfano wa rushwa halali? Samahani japo nimeuliza swali la kisheria, lakini naimani kwa uzoefu wako katika tasnia ya uandishi wa habari bila shaka umewahi kukumbana ama kushuhudia kesi ya aina hii. Nipe japo kwa ufupi.
Mkuu.
Nataka tufike mahali tukubaliane kuwa ili bahasha iwe ni rushwa, lazima iwe na malengo ya kuimfluence, lakini bahasha genuine yenye malengo ya uwezeshaji, sio rushwa!.
Pasco,
Nadhani tumekwishafika hapo. Kupewa grant au usafiri kukuwezesha kufanya kazi yako bila kuambiwa useme hiki na usiseme kile si rushwa. Lakini kama nitaitwa na Wassira, au Nyalandu anataka nifuatane naye kuonyesha kuwa anafanya kazi makini pale Kariakoo kuwaondoa machinga wa Kichina, huku akinipa bahasha, na Wassira ananiambia niripoti nini juu ya shughuli zake, au anakupa tu press release na wewe kama kasuku unaitumia hiyo press release kumpamba Wassira kwenye gazeti kuwa ni kiongozi makini, hicho ni kinyume cha maadili yetu. Naelewa hali ngumu ya kifedha kwa vyombo vyetu vya habari, kwamba Mengi hana slash fund ya kuwawezesha waandishi kulipia usafiri na matumizi mengineyo katika kazi hii, lakini tukiendekeza kupokea bahasha ndipo tufanye kazi yetu tunajilemaza wenyewe. Mfano mzuri ni yule jamaa wa Business Times. Unless kama wewe ulimkatia chochote kama anavyodai dada yetu FF, huo ni mfano wa kuigwa. Alifika pale kwenye press conference yenu akajiondokea na kuandika ripoti yake before deadline. Hivyo ndivyo tunavyotakiwa tuwe.
...mimi nikamwambia bosi, nitamlipa mimi!. ...
...kuja kumaliza jamaa wa Bussiness Times akaniaga, fasta, nikamlinda, akaondoka zake!. Wale wengine wakasubiria bahasha nene, by the time zimetoka ni saa 10 jioni!. Tukaondoka zetu.
.
Mkuu Paulss, waandishi wa habari kama ilivyo professionals nyingine zote, tunazo code zetu of ethis ambazo tunatakiwa tuzifuate, lakini kama zilivyo amri kuu za Mungu zipo na watu wanazivunja, itakuwa ethics?.Mkuu mimi si mwandishi wa habari lakini siamini kama kazi ya uandishi wa habari haina maadili yanayozuia kupoke chochote kutoa kwa mtu unayechukua taarifa toka kwake
Pamoja na sababu lukuki za uchovu wa vyombo vyetu vya habari ambapo nakubaliana na wewe lakini je maadili ya kazi yana ruhusu?
Naamini umesomea kazi hii na unajua naongelea nini
Rafiki Belinda Jacob (wewe ndie uliyekuwa rafiki yangu wa kwanza nilipojiunga tuu hapa jf!, ila hii lips yako rafiki!, usitutie majaribuni!).Pasco mkuu, ukatae ukubali siku hizi waandishi bila bahasha hawatoi habari/pichaz..maslahi yamewekwa mbele kuliko taaluma..
Mkuu Jasusi, nakubaliana na wewe 100 kwa 100!. Hatua hii, Nataka tufike mahali tukubaliane kuwa ili bahasha iwe ni rushwa, lazima iwe na malengo ya kuimfluence, lakini bahasha genuine yenye malengo ya uwezeshaji, sio rushwa!.Nataka tufike mahali tukubaliane kuwa ili bahasha iwe ni rushwa, lazima iwe na malengo ya kuimfluence, lakini bahasha genuine yenye malengo ya uwezeshaji, sio rushwa!.
Pasco,
Nadhani tumekwishafika hapo. Kupewa grant au usafiri kukuwezesha kufanya kazi yako bila kuambiwa useme hiki na usiseme kile si rushwa. Lakini kama nitaitwa na Wassira, au Nyalandu anataka nifuatane naye kuonyesha kuwa anafanya kazi makini pale Kariakoo kuwaondoa machinga wa Kichina, huku akinipa bahasha, na Wassira ananiambia niripoti nini juu ya shughuli zake, au anakupa tu press release na wewe kama kasuku unaitumia hiyo press release kumpamba Wassira kwenye gazeti kuwa ni kiongozi makini, hicho ni kinyume cha maadili yetu. Naelewa hali ngumu ya kifedha kwa vyombo vyetu vya habari, kwamba Mengi hana slash fund ya kuwawezesha waandishi kulipia usafiri na matumizi mengineyo katika kazi hii, lakini tukiendekeza kupokea bahasha ndipo tufanye kazi yetu tunajilemaza wenyewe. Mfano mzuri ni yule jamaa wa Business Times. Unless kama wewe ulimkatia chochote kama anavyodai dada yetu FF, huo ni mfano wa kuigwa. Alifika pale kwenye press conference yenu akajiondokea na kuandika ripoti yake before deadline. Hivyo ndivyo tunavyotakiwa tuwe.
Mkuu Jasusi, nakubaliana na wewe 100 kwa 100!. Hatua hii, Nataka tufike mahali tukubaliane kuwa ili bahasha iwe ni rushwa, lazima iwe na malengo ya kuimfluence, lakini bahasha genuine yenye malengo ya uwezeshaji, sio rushwa!.
Pasco,
Nadhani tumekwishafika hapo. Kupewa grant au usafiri kukuwezesha kufanya kazi yako bila kuambiwa useme hiki na usiseme kile si rushwa
Tunatatafuta hapa ni the deviding line kati ya uwezeshaji waandishi kutimiza wajibu wao bila influence na uwezeshaji waandishi ili kupata positive covarage nahadi nitafikia kwenye waandishi wanaoendekeza njaa na ile pettycash journalism!.
Mkuu Wacha1, hivi ulidhani wale waandishi wanaosafiri na Obama wanasafiri bure, wanakula bure na kulala bure?. Si wanapewa bahasha nene huko makazini kwao! Wanaotoa hizo pesa za hizo bahasha nene ni kina nani?.
Au unatazama na kusikiliza BBC ukijua ni bure tuu kama sadaka?!. Kila aliye Uingereza anakatwa pesa za kusikiliza na kuangalia BBC, usikilize, usisikilize, utazame, usitazame, unakatwa!.