The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,110
- 115,886
The Boss,
Mwaka 1998 niliendesha semina ya waandishi wa radio na TV pale DSM na Arusha. Tulipofika katika mada ya ethics nikazusha hili suala la kupokea bahasha kutoka kwa mawaziri au watu wakubwa. Waandishi wote pale walikuwa na msimamo kwamba bahasha ni essential kwa kazi zao, nikasema hapana. Tulibishana mpaka nikaona heri tukubaliane kutokukubaliana. Lakini niliwakumbusha kuwa huwezi kuwa partial unaporipoti juu ya mtu anayekupa bahasha. Utatoa ripoti nzuri tu juu yake. Ni kweli kama usemavyo wenzetu Tanzania, na nchi nyingine zinazoendelea ambazo zimeendekeza mtindo huu, zinajiundia utaratibu wa kipekee, na ndio maana Pasco amekazana kuziweka hizo bahasha katika mafungu mbalimbali. Ningepata fursa nyingine ningependa kukutana na wale wanaomiliki magazeti, radio na tv niwaambie kuwa lazima watenge fungu la expenses za waandishi wa habari kwa sababu kuendekeza hii tabia ya kutegemea vibahasha ndiko kulikopelekea waandishi wetu wawe wavivu, wasiwe critical, na washindwe kutimiza wajibu wao kama fourth estate.
asante aisee
nilianza kushangaa mno....