Waandishi wa habari mmegeuza JamiiForums ndiyo chanzo pekee cha kupata habari

baba anjela

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
431
310
Leo JamiiForums ndiyo Google kwa waandishi wetu wa habari. Mtu yupo nyumbani 24hrs macho yapo JamiiForums kutazama nini kimekuwa posted akopi na kupesti habari za watu. Hizo blog ndiyo kabisaaa wanakopi kila kitu.

Watanzania tupunguze uvivu, tukubali kutoka jasho. Ndiyo maana habari nyingi zimejaa upotoshaji. Kukopi na kupesti si sawa kabisa.
 
Kitendo cha waandishi kukodoa macho jamiiforums ni ushahidi tosha kwamba hili ni gulio muhimu la habari. hata hivyo wengi wao nao ndiyo wanaotupia habari ambazo haziandikiki kwenye magazeti lakini zina viashiria vya ukweli wake
 
Leo JamiiForums ndiyo Google kwa waandishi wetu wa habari. Mtu yupo nyumbani 24hrs macho yapo JamiiForums kutazama nini kimekuwa posted akopi na kupesti habari za watu. Hizo blog ndiyo kabisaaa wanakopi kila kitu.

Watanzania tupunguze uvivu, tukubali kutoka jasho. Ndiyo maana habari nyingi zimejaa upotoshaji. Kukopi na kupesti si sawa kabisa.
Sisi hao hao waandishi wa habari ndo wanachama humu na ndio tunaoleta hizo taarifa humu. Kama mnataka JAMIIFORUMS pia isitumie taarifa kutoka vyanzo vingine kama MAGAZETI na TV
 
Habari kama za chadema na ukawa unafikiri watazipata wapi wakati wamezuiwa kuongea na wananchi?
 
Back
Top Bottom