Tetesi: Waalimu sasa kuanza kupigwa picha pindi wanapoingia darasani

Katika kuhakikisha kuwa walimu wanaingia darasani kumeandaliwa utaratibu wa kuwapa tablet walimu wakuu na wakuu wa shule ili kumpiga picha kila mwalimu pindi anapoingia darasani ili kuthibitisha kuwa amefundisha!

Mara baada ya mwalimu kupigwa picha itatumwa kwenye ofisi za elimu wilaya ili
kuthibitisha kuwa mwalimu fulani ameingia darasani na amefundisha!
Hii taarifa ni kwa mujibu wa rafiki yangu wa karibu mwalimu wa primary mojawapo iliyopo wilayani kongwa dodoma ambapo tayari wao wameshapewa taarifa rasmi kupitia mwalimu mkuu wao kwamba utaratibu huo utaanza hivi karibu hivyo wajiandae kwa hilo!
sasa c bora wangefunga camera madarasan
 
Sahihisho. Walimu wakuu hawapati posho ya laki mbili na nusu. Wao wanapata laki mbili tu. Ni wakuu wa shule na waratibu elimu KATA ndio wanaopata laki 2.5 kwa mwezi tokea July mwaka huu na siyo Aug
 
1474846420262.jpg
 
Kama wanataka wafunge kamera za CCTV kila shule na kila darasa lakini kwa mpango huo hakuna kitu. Hapo wanatafuta njia ya kupiga hela. Mungu isaidie tz.
 
Hii ni local method, imebuniwa na mtu ambaye hakutaka kuumiza kichwa. Kama ndiyo ubunifu wa viongozi basi hili taifa lina miaka elfu mbele ili liendelee.
 
Kuingia darasani ni kwingine na kufundisha ni kwingine. Cha msingi ni maslahi tu!!
 
Kwanza umeme hakuna vijijini halafu network inasumbua, unaweza kutuma picha ukairudia kuituma mara 100 na isikubali. Wawaunganishe na kifurushi cha internet cha kila wiki
 
Kuna siku watasema waweke computer kila darasa, nchi nzima ifundishwe kwa tehama na walimu wote waachishwe kazi ili kuokoa fedha nyingi zinazopotea kupitia mishahara. Hizi ni dalili na ukumbuke akufukuzaye hakwambii toka.
 
Katika kuhakikisha kuwa walimu wanaingia darasani kumeandaliwa utaratibu wa kuwapa tablet walimu wakuu na wakuu wa shule ili kumpiga picha kila mwalimu pindi anapoingia darasani ili kuthibitisha kuwa amefundisha!

Mara baada ya mwalimu kupigwa picha itatumwa kwenye ofisi za elimu wilaya ili
kuthibitisha kuwa mwalimu fulani ameingia darasani na amefundisha!
Hii taarifa ni kwa mujibu wa rafiki yangu wa karibu mwalimu wa primary mojawapo iliyopo wilayani kongwa dodoma ambapo tayari wao wameshapewa taarifa rasmi kupitia mwalimu mkuu wao kwamba utaratibu huo utaanza hivi karibu hivyo wajiandae kwa hilo!
walimu watakua wanaenda kupigwa picha kwa kupanga foleni ofisini kwa mkuu kabla ya kufundisha, au mkuu ndiye atayekua anawasubiri kwenye milango ya madarasa? mbona madarasa ni mengi na muda wa kuisha kipindi ni mmoja, atawezaje kuwapiga picha wote wanaoingia darasani ukizingatia kua madarasa yapo mengi na kuna umbali kati ya darasa na darasa? huu muda wa kupoteza kusubiri kupigwa picha sjui nani ataulipa!
na kama hatakua anawasubiri mlangoni na kuwapiga picha, bali kuwafuata darasani ili awapige picha; ina maana mkuu kazi yake itakua ni kutembea na ratiba ya vipindi vya shule ili ajue wapi kipindi kimekwisha aende kupiga picha? atakua hana kazi nyingine ya kufanya tofauti na kupiga picha? au shule ataajiri cameraman? huyo cameraman wa kila shule Tanzania nzima atalipwa na nani kipindi hiki cha elimu bure wakati shule haina hata hela ya kuwalipa walimu wa muda wa masomo ya sayansi, badala yake kuwaacha wanafunzi wakiwa hawasomi masomo fulani mpaka mwaka unaisha? pia shule hata kuwalipa walinzi zimeshindwa!
Hii serikali ni ZE.RO kabisa!
 
Katika kuhakikisha kuwa walimu wanaingia darasani kumeandaliwa utaratibu wa kuwapa tablet walimu wakuu na wakuu wa shule ili kumpiga picha kila mwalimu pindi anapoingia darasani ili kuthibitisha kuwa amefundisha!

Mara baada ya mwalimu kupigwa picha itatumwa kwenye ofisi za elimu wilaya ili
kuthibitisha kuwa mwalimu fulani ameingia darasani na amefundisha!
Hii taarifa ni kwa mujibu wa rafiki yangu wa karibu mwalimu wa primary mojawapo iliyopo wilayani kongwa dodoma ambapo tayari wao wameshapewa taarifa rasmi kupitia mwalimu mkuu wao kwamba utaratibu huo utaanza hivi karibu hivyo wajiandae kwa hilo!
Well, to be safe acha ni-assume kuwa huyo rafiki yako alikuwa anatania, nisije nikafanya uchochezi kwa maneno ya urongo.
 
Kwa nini wasiweke utaratibu wa kufunga CCTV kila darasa?
Picha moja ya mnato itasaidia nini?
Kama taarifa ya mkuu wa shule/mwalimu mkuu haiminiki atashindwaje kuwapiga picha tu kama picha hata kama hawafundishi na kuzituma?
 
ataajiriwa mtu kwa kazi hiyo? ujue kila kipindi ni dk 40, habari hii imekaa kizushi..
 
Back
Top Bottom