Waafrika tulimtuma Kolo Muani kuwapiga kibao Wamorocco, leo tunamtumia Kylian Mbappe

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,866
Mfalme wa Morocco alikuwa rafiki mkubwa wa Shujaa Magufuli, kwa sababu ya urafiki wao tumejengewa msikiti wa Kinondoni na tumeahidiwa kujengewa uwanja wa mpira jijini Dodoma. Tunawapongeza sana ndugu zetu Morocco kwa kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza Africa kufika nusu finali ya Kombe la Dunia.

Lakini tuliposikia Wamorocco wakilewa sifa na kusema wao si waafrika, tukamtuma Kolo Muani kuwafunga goli Wamorocco kupitia mizimu ya Babu zake waliolala Congo, na Leo tunamtuma Kylian Mbape akawapige ngumi Argentina kupitia mizimu ya Babu zake waliolala Cameroon kulipa kisasi cha Argentina kuwapoteza Waafrika wote waliopatikana nchini Argentina.

- Kwa nini Argentina haina mchezaji mweusi kwenye timu yao ya Taifa?

Mwaka 1900 bara la Amerika kusini ndilo lilikuwa bara lenye watu weusi wengi zaidi wakikadiriwa kuwa zaidi ya milioni 170 huku Brazil ikiongoza ikiwa na watu weusi takribani milioni 120. Pamoja na hayo yote kitu kimoja cha kushangaza nchi ya Argentina 🇦🇷 ndiyo nchi pekee yenye watu weusi wawili au watatu.

Ni dhahiri kuna kitu kilitokea, watu weusi walikwa mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya Paraguay wakiwa na vifaa duni, vita hivyo vilidumu kwa miaka mitano (1865-70). Pia viongozi wa Argentina wa wakati huo walifanya hivyo pia kwenye vita dhidi ya Brazil iliyodumu kwa miaka mitatu.

Baada ya vita hivyo kuisha ambapo Argentina ilipigika vibya mno, Watu weusi waliosalia waliwekwa kwenye maeneo maalumu ambayo kwa kipindi hicho kulikuwa na ugonjwa wa hatari unaosababishwa na bacteria “Plague”. Watu weusi wengi sana walikufa huku serikali ikiwanyima kwa makusudi matibabu dhidi ya ugonjwa huo.

Nimalizie nanyi Wamorocco, ni kweli kabisa mkiwa Morocco taa za Ulaya usiku mnaziona, sasa hamtakiwi kutukataa sisi kwa kuwa ni weusi na zaidi ya yote kwa kuwa tumezaliwa Afrika basi tayari tumefungwa 1-0, kwa kuwa hatuna elimu ya kutosha basi tumefungwa 2-0, na kwa kuwa tunaomba omba misaada basi tumeshafungwa 3-0.

Niseme tu ninyi ni Waafrika tu kwa sababu kama ninyi Morocco ni Arabs- basi Jamaica ni Afrika na sio America, pia kama ninyi Morocco ni waarabu basi Uturuki nayo ni Waarabu sio wazungu wa Ulaya, kama ni Wamorocco ni waarabu basi Hispania nayo ni Waarabu sio Ulaya, ninyi Morocco mtabaki kuwa Waafrika daima dumu.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
HUYU NI MMOJA KATI YA WATU WEUSI WALIOWAHI KUICHEZEA TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA
WATANZANIA TUSIWE WEPESI WA KUDANGANYWA BILA KUJIONGEZA
FB_IMG_16713792460879516.jpg
 
Penati siku zote hazina mwenyewe. Binafsi nawapongeza kwa kupambana kwa dakika zote za mchezo, mpaka kufikia hatua ya matuta.

Golikipa wa Argentina alionesha umahiri wake kwenye penati, wakati yule wa Ufaransa alikuwa anaruka opposite direction.
Big no, hayo ni maneno ya kukosa, penati zina mwenyewe, na mwenyewe kwa jana alikua Argentina
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom