Waachana siku tatu kabla ya ndoa

Joan S

JF-Expert Member
Oct 26, 2021
2,382
9,503
Wanajukwaa, hii kitu imetokea uku kwetu mtaani, mahusiano yavunjika siku chache kabla ya kufungishwa ndoa... Jamaa na bibie wanafanya Kazi mikoa tofauti, sasa wamerudi Ili wafunge ndoa takatifu Ili wawe rasmi, mke na mume. Sasa ndugu wa mke wakamuuliza bibie, vipi mmeshapima HIV na mumeo mtarajiwa?. ..Binti akajibu hapana.

Itabidi waitwe Mume mtarajiwa na mke mtarajiwa, Ili wapelekwe kupima, maana baba mkwe aligoma mwanae asiolewe mpk wote wajue afya zao. Apo ikumbukwe mahali ilishatolewa ya kutosha, cash. Upande wa mme washanunua kila kítu cha shughuli, washakodi ukumbi, washafanya maandalizi yote, sare ishatembezwa na majirani kualikwa.

Baada ya kufika hospitali, wakachukuliwa vipimo, na majibu yalipotoka....wote mambo ni safiiiiii kbs...familia ikafurahi. Asa Dkt akasema "aah hongera bhana maana umeshaweka kitu tumboni muda si mrefu utaitwa baba, mchumba ana mimba mIEzI ". Jamaa alitoa macho hatari, unasemaje?. Itabd ndugu waulize kwani mzigo sio wako baba?.

Jamaa akasema muulizeni mtoto wenu aseme iyo mimba ni ya nani, maana mimi nna miez nae 6 sijawah shiriki nae tendo, na ata baada ya kurudi apa, mtt wenu alinilazimisha sana twende tukafanye tendo lkn Mimi niligoma katakata nikamwambia tusuburie ndoa ipite bs tutafanya kwa uhuru. Binti akasema ni kweli mimba siyo ya jamaa, akaanza lia aliomba msamaha eti bd anampenda mumewe mtarajiwa.

Yani mpaka sasa binti anatishia kujiua, ndoa jamaa kaikataa, Yani mihela yote ile imepotea. Nimejisikia vby kwa kweli , Dunia hii usiombe likukute jambo kama hili. Ama kweli usaliti mbaya. Ingawa wengine wanamshauri eti amuoe ivyo ivyo atakwenda kulea mimba na mtoto awe wake.
 
Wanajukwaa, hii kitu imetokea uku kwetu mtaani, mahusiano yavunjika siku chache kabla ya kufungishwa ndoa... Jamaa na bibie wanafanya Kazi mikoa tofauti, sasa wamerudi Ili wafunge ndoa takatifu Ili wawe rasmi, mke na mume. Sasa ndugu w
Mwenye mimba amuoe huyo binti kwa maandalizi hayohayo yaliofanyika yaani abadilishe tu bwana harusi vingine vyote vibaki constant.
 
Ndoa ni kamali, anaweza kumuoa huyo na akaishi naye vema japo kila mda akikumbuka lazima roho itaumia, kama anataka kula na appetite yote inakata.

Issue hiyo aliweza Joseph tu na yeye ilibidi Mungu aingilie kati lasivyo alikuwa ameshamkataa Maria. It needs God’s intervention.

Binafsi nisingeweza kufunga ndoa naye maana najifahamu mwenyewe. Namshukuru sana aliyenipatia mke ambaye bado ni bikira.
 
Back
Top Bottom