W J Malecela kwa hili la wizi na kutokuwajibika kwa mawaziri ungekuwa upande gani?

- Again read my lips, hata siku moja siwezi kusaini karatasi ya kumpa Waziri anayetuhumiwa wizi nafasi ya kujiuzulu, ningeshauriana na Mh. Zitto, kwenda ambele zaidi kwa kudai wafikishwe kwenye Sheria,

- Nisingeweza kusaini karatasi ya kuwapa mwanya wa kujiuzulu tu! ni utamaduni mbovu sana kwa the future ya taifa letu!

William.
Gimme a break ! Hivyo walioanzisha utamaduni huo (sheria) wamepotoka ?! Aiseeh ! Ukuliachi !?
 
- Kwanza ningedai FACTS, so far sijaziona zote na very clear of what happened and what did not happen, with FACTS at hand kwanza ningerudi jimboni kwangu kuwafahamisha wananchi FACTS za kilichotokea na kuwauliza nini msimamo wao kwanza, maana ni wao ndio ninaowawakilisha kule Bungeni!

- Unajua unapomtuhumu Waziri wizi ni lazima kuwepo na Legal Facts, kwa sababu muhimu hapo ni historia ya mbele ya safari, unajenga utamaduni wa kujali sheria, kwa hiyo unatakiwa umakini sana kwenye conclusion kwamba kweli ni wezi, siamini kuwa kama FACTS zipo clear, kuna kiongozi yoyote bungeni angeshindwa kusaini!

William.
Hujajibu swali..
 
Ndiye huyo alikuwa anautaka ubunge wa Afrika Mashariki......waliokupiga chini nafikiri walikuwa na sababu. Mwakyembe hakukosea alichokisema juu ya hawa waliokuwa wagombea akiwemo W.J.M

- ha! ha! ha! this is becoming a Classic song! ha! ha! ha! I mean ninaamini sasa mnaona kwamba kuna makosa somewhere na hii ishu nzima sasa hamtaki kukubali, hivi kweli mkuu ungetegemea mimi mtumzima na akili timamu nikaanze kusaini maneno ya kuwapa mawaziri njia ya kujiuzulu bila kufikishwa kwenye Sheria?

- Sheria kwanza!

William.
 
1. For sure nisingesaini kaaratsi ya kuwapa mawaziri kujiuzulu tu, HAPANA NISINGESAINI NO WAY!, NINGEMSHAURI MH. ZITTO, TWENDE MBELE ZAIDI NA KUDAI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE!

2. Hata siku moja siwezi kutetea msimamo wa chama wa kuwalinda mawaziri ambao Sheria imeridhia kuwa ni wezi, unless kama Sheria haijaridhia kama ilivyo sasa!

William.

Mkuu heshima mbele.

Ni jambo la muhimu umejibu swali la mheshimiwa mtoa hoja.

Sasa utaratibu kisiasa ni kwamba kama kuna tuhuma nzito dhidi ya wizara husika na ikathibitishwa na CAG kwa kuweka FACTS zote wazi na Bunge likaona kwamba FACTS zote hazina kasoro, basi inabidi kwa utaratibu wa nchi zote zilizoendelea kwa waziri husika kuwajibika kwa kujiuzuru.

Ni kwa utaratibu huo mbunge husika aliweza kuleta hoja ya kutokuwa na imani na mawaziri wa wizara husika na ikawa ni lazima apate "support" ili hoja iwe na nguvu na hilo likatendeka.

Jambo la pili ambal0o umejibu kwa kusisitiza uwepo wa sheria, sheria ipo na inaweza kutekelezwa endapo mbunge na waziri husika anavuliwa heshima hiyo ya uwaziri kwa kujiuzuru ili kuwapa polisi nafasi ya kuwasiliana na CAG na kupata documents zilizo na FACTS na hapo kumfanya DPP aweze kuamua kama kuna kesi ya kujibu.

Ikifikia hatua hiyo ya waziri na mbunge husika kufunguliwa mashtaka kwamba amehusika na hujuma na ubadhilifu wa mali aya umma basi inabidi ajiuzuru ubunge na awe tayari kujibu mashtaka mahakamani.

Akipatikana na hatia ibidi afungwe jela na uwezo wa kuwa mbunge unakuwa haupo tena kutokana na yeye kuwa "disgraced" kwa jamii na hafai.

Asipopatikana na hatia atabakia kuwa mbunge akiwakilisha bunge lake lakini kwa uangalifu wa rais hataweza kumwamani tena kwamba ataweza kusimamia wizara kikamilifu na mbunge huyo ataendelea kuwa "backbencher".

Huu ni utaratibu wa nchi zote zilizoendelea na zenye kufuata taratibu zote za sheria na ambazo 90% yake umetembelea mkuu.

Kwetu Tanzania Polisi bado hawana meno ya kuanza kufuatilia hiyo kesi mpaka raisi aagize na ndipo DPP atafanya kazi yake jambo ambalo si sahihi.
 
- ha! ha! ha! this is becoming a Classic song! ha! ha! ha! I mean ninaamini sasa mnaona kwamba kuna makosa somewhere na hii ishu nzima sasa hamtaki kukubali, hivi kweli mkuu ungetegemea mimi mtumzima na akili timamu nikaanze kusaini maneno ya kuwapa mawaziri njia ya kujiuzulu bila kufikishwa kwenye Sheria?

- Sheria kwanza!

William.

sasa mtu akishajiuzulu si ndio inakua vzuri kwa sheria kufuata mkondo wake?
 
Willy amekuwa na akili za Nape, anajibu hovyo hovyo kwenye hoja nzito, Nape ndio aliyemwambia Willy rudi Tanganyika tutakupa ubunge wa EAC. Nape amekuchuuza mkuu ni bora ungeendelea kujibebea box zako kuliko kuja kuaibika na kudharaulika. Willy umeshachuja kama Nape
 
Bill nimekuuliza, je ukakuta mtu ana twin tower na mishahara ya mawaziri inajurikana? itakuwaje, yaani utaamua nini? i mean utaamuaje au ndio utasubiri ushahidi?
 
sasa mtu akishajiuzulu si ndio inakua vzuri kwa sheria kufuata mkondo wake?

- Sheria kwanza jamani, otherwise naomba kuwahi mpirani sasa si unajua leo Tanzania tunawakilishwa na Simba, ingawa mimi ni Yanga ngoja nikawashamgilie Simba, I mean ndio Uzalendo wenyewe huo last time nilienda kuona Yanga na Zamaleck, I was shocked kuona washabiki flani uwanjani wanawashangilia sana wageni it broke my heart, sio uzalendo hata kidogo!

- HAYA JAMANI WAKUU LATER KIDOGO NGOJA TUKASHANGILIE WAWAKILISHI WETU KWANZA, TAIFA MBELE SI MNAJUA KAMA KAWAIDA YANGU, TAIFA MBELE!

William.
 
Bill nimekuuliza, je ukakuta mtu ana twin tower na mishahara ya mawaziri inajurikana? itakuwaje, yaani utaamua nini? i mean utaamuaje au ndio utasubiri ushahidi?

- Sheria kwanza jamani sasa ukianza kuvamia wananchi na mali zao bila FACTS itakuwa yale yale mambo ya Azimio la Arusha!

William.
 
- Kaka nchi zote zilizoendelea Duniani, CAG ilitakiwa iwe connected na Sheria, incase imegundua wizi basi Sheria inachukua mkondo wake kwa baraka za kamati ya bunge kwanza, hakuna sababu ya kumsubiri Rais, wala kokus ya CCM, au kusaini saini 72, hapana saa hizi tungekuwa tunajadili mawaziri wakiwa Rumande!

- Gavana wa Ilinois alipotaka rushwa kutoa kiti cha Obama, FBI walifahamishwa mara moja na kamati ya Sheria ya State Assembly wakaanza kumrekodi mpaka kufikishwa kwenye Sheria, CAG ilipogundua wizi ilitakiwa mara moja kuiarifu kama ti ya bunge ambayo nayo haraka sana ingetoa kibali cha DPP kuingia kwenye uchunguzi, by now tungekuwa tunaongea Sheria tu, sio kugombea saini wala kusubiri kamati kuu!

William.

Wewe unazungumzia mfano moja tena mdogo ambao kosa lililofanyika ni la jinai. Lakini nasisitiza tena hata huko Marekani kuna mifano lukuki ya wanasiasa waliojiuzuru kwa mazingira ambayo isingekuwa rahisi kuwashtaki. Ukitaka nitakuletea mifano zaidi ijapokuwa najua unaelewa hilo ila hupo radhi kukubali ukweli.
 
- Kaka nchi zote zilizoendelea Duniani, CAG ilitakiwa iwe connected na Sheria, incase imegundua wizi basi Sheria inachukua mkondo wake kwa baraka za kamati ya bunge kwanza, hakuna sababu ya kumsubiri Rais, wala kokus ya CCM, au kusaini saini 72, hapana saa hizi tungekuwa tunajadili mawaziri wakiwa Rumande!

- Gavana wa Ilinois alipotaka rushwa kutoa kiti cha Obama, FBI walifahamishwa mara moja na kamati ya Sheria ya State Assembly wakaanza kumrekodi mpaka kufikishwa kwenye Sheria, CAG ilipogundua wizi ilitakiwa mara moja kuiarifu kama ti ya bunge ambayo nayo haraka sana ingetoa kibali cha DPP kuingia kwenye uchunguzi, by now tungekuwa tunaongea Sheria tu, sio kugombea saini wala kusubiri kamati kuu!

William.

Idara ya CAG ni wataalamu katika fani yao, baada ya kufanya ukaguzi pamoja na vithibitisho vya uvujaji wa pesa za umma wameambatanisha taarifa hiyo na kuifikisha kwenye mihimili husika. Kwa vyo vyote idara hiyo nyeti iko chini ya ofisi ya rais, hivyo taarifa humfikia mkulu kabla ya kulifikia bunge.

Taarifa za ujuvujaji huo zinawagusa na kuwataja wahusika moja kwa moja, ndio maana baadhi kama atumishi wa wilaya ya kilosa wakuu wao wamewahamishia wilaya nyingine licha ya kuanikwa hadharani uovu uliofanywa.

Wanaowalinda ni viongozi wa juu, yaani wasimamizi wakuu wa wizara na idara za serikali ambazo ziko chini ya viongozi waandamizi Mawaziri.

Mkanganyiko ndio huu, hiyo legal facts zaidi inayohitajika ni ipi wakati CAG ameonyesha kila kitu kwenye ripoti yake? Na kinachopelekwa bungeni ni muhtasari, lakini wahusika wakuu kila wizara hupewa kinaganaga cha taarifa hiyo na hawachukui hatua. Sasa hiyo Legal Fact unayosema Malecela ni ipi? Ni sahihi kabisa wabunge kuwawajibisha Mawaziri wazembe wanaowalinda wavujaji mali ya umma.

Matatizo ya mfumo hayawezi kurekebishika kwa siku moja, ni jambo linalohitaji muda mrefu, na hata katiba mpya ikikamilika, bado kuna amendments zitahitajika kutokana na mikinzano ya utendaji na utekelezaji unaoweza kujitokeza kila leo.

Ndio maana ya kuwa na chombo cha kutunga sheria, vinginevyo sheria ingetungwa mara moja tu na kisha hatungehitaji bunge, ila mhimili wa mahakama tu kutafsiri na kuamua mambo kisheria, lakini kwa vile kila mara kuna mabadiliko au nyongeza ya mambo ya kisheria tunahitaji kuwa na bunge wakati wote, kwa vile dunia inabdilika, watu wanakua na kubadilika, uchumi unakua na kubadilika, na mengineyo. Uwajibikaji ni lazima uchukuliwe mara kabla mambo hayajaharibika.
 
CAG kafanya research na kagundua huwo wizi wa mawaziri,so unataka nini hiyo tayari ni legal (fact)
 
@W J Malecela
Nimesoma comment zako. Nimeona bado kumbe una_akili za kimagamba. Unataka facts gani zaidi ya CAG.

Au unataka Facts za wanasheria, ambao wanaweza kutumia vifungu vya sheria to convice you "this is yellow instead of blue",.....

Mutuz: hamna Facts muhimu kama Facts za kitaalam. CAG anatoa Facts za kitaalam(kimahesabu) na wala sio za kisiasa.
Sasa wewe unataka nini zaidi ya hizo Facts za kimahesabu???

Mutuz hamna siku niliyokudhalau bro kama leo...
 
Mi nakushangaa willy unavyong'ang'ania sheria kwanza wakati hali halisi ya nchi yetu unaiona ni sheria ngapi ambazo zipo hapa tz lakini hazitendi haki kwa wananchi maskini na kufeva tabaka la juu. Alafu ni mara ngapi mahaka zetu zinaingiliwa na viongozi wa juu kama rais sasa wewe unadhani hata ikitungwa sheria kwa ajiri ya mafisadi how sure ure kuwa itatenda haki?
Wakati mwingine usitumie mifano ya 90% ya nchi ulizotembelea wakati hali halisi ya nchi yako unaijua.
 
- Kwanza ningedai FACTS, so far sijaziona zote na very clear of what happened and what did not happen, with FACTS at hand kwanza ningerudi jimboni kwangu kuwafahamisha wananchi FACTS za kilichotokea na kuwauliza nini msimamo wao kwanza, maana ni wao ndio ninaowawakilisha kule Bungeni!

- Unajua unapomtuhumu Waziri wizi ni lazima kuwepo na Legal Facts, kwa sababu muhimu hapo ni historia ya mbele ya safari, unajenga utamaduni wa kujali sheria, kwa hiyo unatakiwa umakini sana kwenye conclusion kwamba kweli ni wezi, siamini kuwa kama FACTS zipo clear, kuna kiongozi yoyote bungeni angeshindwa kusaini!

William.

Kaazi kweli kweli
Kwa hiyo wao wanasaini baada ya hukumu kusomwa au?
 
Mi nakushangaa willy unavyong'ang'ania sheria kwanza wakati hali halisi ya nchi yetu unaiona ni sheria ngapi ambazo zipo hapa tz lakini hazitendi haki kwa wananchi maskini na kufeva tabaka la juu. Alafu ni mara ngapi mahaka zetu zinaingiliwa na viongozi wa juu kama rais sasa wewe unadhani hata ikitungwa sheria kwa ajiri ya mafisadi how sure ure kuwa itatenda haki?
Wakati mwingine usitumie mifano ya 90% ya nchi ulizotembelea wakati hali halisi ya nchi yako unaijua.

Malecela yuko hapa kutetea chama chake.
Nilijua hawa jamaa vijana labda wana maoni tofauti ndani ya CCM. Kumbe wote ni walewale

Usishangae Malecela akiwa mbunge, na yeye anakuwa Fisadi, kama ndugu zake kina Ngeleja, Malima na wengine
 
W.J.Malicela ebu soma post # 124 ya Richard ya uzi huu
Nina imani kuna point za maana ambazo zaweza kubadilisha maono yako juu ya suala hili.
 
Mi nakushangaa willy unavyong'ang'ania sheria kwanza wakati hali halisi ya nchi yetu unaiona ni sheria ngapi ambazo zipo hapa tz lakini hazitendi haki kwa wananchi maskini na kufeva tabaka la juu. Alafu ni mara ngapi mahaka zetu zinaingiliwa na viongozi wa juu kama rais sasa wewe unadhani hata ikitungwa sheria kwa ajiri ya mafisadi how sure ure kuwa itatenda haki?
Wakati mwingine usitumie mifano ya 90% ya nchi ulizotembelea wakati hali halisi ya nchi yako unaijua.

Mkuu QK,
Huyu asingeweza kusign nimesoma post zake nimecheka sana alivyo na utetezi wa kitoto!

Willy unakua mwili tu mkuu, hahahahahahahahaha!
 
- NISINGESAINI BILA KIPENGELE CHA KUWAFIKISHA MAWAZIRI KWENYE SHERIA!

William.

Ulikosea toka mwanzo, hili swali lilikuwa na mitego mingi kwako................Hivyo kama mwanasiasa/mbunge mtarajiwa

unatakiwa kuwa makini sana na vitu vya namana hii, kuanzia sasa hata huko mbeleni..

Bahati yako ni kwamba hawa wanaokuhoji sio wapiga kukura wako watarajiwa la sivyo wangekutilia shaka mapema na

wasingekubali kuja kuongozwa na mtu ambaye anaonekana mba,mba,isha,ji!

Ungeweza kukaa kimya, au ngetafuta jibo lolote ambalo halikaribishi maswali na mashaka kwa watu....

Anagalia, usipokuwa makini utausikia tu ubunge hadi una zeeka!
 
Back
Top Bottom