W J Malecela kwa hili la wizi na kutokuwajibika kwa mawaziri ungekuwa upande gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

W J Malecela kwa hili la wizi na kutokuwajibika kwa mawaziri ungekuwa upande gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasimba G, Apr 29, 2012.

 1. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,487
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Kwa kuwa humu jamvini watu wako wazi saana na W J Malecela watu wamekuelekeza labda ukagombee Jimbo la mtera 2015, je kwa hili la wizi na ukosefu wa uwajibikaji wa serikali ungekuwa upande gani? Ungetia saini form ya Zitto au ungelinda chama chenu kama wenzio akina Kingwa?

  Utakuwa mbunge wa wananchi au wa chama?
   
 2. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,133
  Likes Received: 1,363
  Trophy Points: 280
  - Kwanza ningedai FACTS, so far sijaziona zote na very clear of what happened and what did not happen, with FACTS at hand kwanza ningerudi jimboni kwangu kuwafahamisha wananchi FACTS za kilichotokea na kuwauliza nini msimamo wao kwanza, maana ni wao ndio ninaowawakilisha kule Bungeni!

  - Unajua unapomtuhumu Waziri wizi ni lazima kuwepo na Legal Facts, kwa sababu muhimu hapo ni historia ya mbele ya safari, unajenga utamaduni wa kujali sheria, kwa hiyo unatakiwa umakini sana kwenye conclusion kwamba kweli ni wezi, siamini kuwa kama FACTS zipo clear, kuna kiongozi yoyote bungeni angeshindwa kusaini!


  William.
   
 3. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,487
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  sasa we Bil muda ni finyu saana, hoja is within some fraction of times! si uliiona?
   
 4. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,487
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Facts ilikuwepo report ya CAG, kama labda ulitaka uende kufanya utafiti mwenyewe na ulikuwa huiamini report ya CAG
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 11,829
  Likes Received: 1,281
  Trophy Points: 280
  W.J Malecela Usitudanganye Kurudi jimboni isingewezekana muda ulikuwa mdogo sana kufika jimboni kuwakusanya wapiga kura halafu ukusanye waoni yao uyafanyie analysis mwishoni ndio uconclude.
   
 6. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Sikiliza ukishachaguliwa maana yake tayari wananchi wamaeamua nguvu na maamuzi yao unayo wewe,kurudi kwao kuna maana kuwa hujajua kama nguvu yao unayewwe yaelekea hujui kuitumia nguvu utakayopewa na wana Mtera bora urudi USA
   
 7. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,133
  Likes Received: 1,363
  Trophy Points: 280
  - Mkuu wangu Wabunge wa mabunge yote Duniani huwa wana wasaidizi, hizi ndizo kazi zao wakati Mbunge anaendelea na kikao wao wanakimbia Jimboni kufanya hizi live analysis, kama sisi hatuna wakati ni sasa Wabunge wetu wawe nao, Mbunge huwezi kwenda Bungeni na kuamua tu bila ridhaa za waliokuchagua, sawa kuna ishus ambazo sio lazima sana input ya wananchi wako wa jimbo, lakini ishu serious kama hii ya kufikia kutokwua na imani na Waziri Mkuu, maana yake ni kutokwua na imani na Serikali, huwezi Mbunge peke yako ukajiamulia tu!

  William.
   
 8. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,133
  Likes Received: 1,363
  Trophy Points: 280
  - FACTS za CAG ni za kimahesabu zaidi, muhimu ni Legal Facts katika CAG report, bado sijaziona in full!

  William.
   
 9. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwenye ripoti za CAG hususani kwenye hoja nzito huwa ananukuu kumbukumbu namba ya mkataba, namba ya hati ya malipo, akaunti namba ya benki ambapo malipo yamefanyika nk. Ni legal facts gani unazitaka zaidi ya hizi? Je ina maana kwako wewe ripoti za CAG siyo za kuziamini? Yani wewe una tofauti na Kigwangala aliyeleta uzi humu kujitetea bahati mbaya ule uzi ukageuka kuwa mwiba kwake?
   
 10. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 9,553
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Willy, usituangushe mkuu! CAG aliweka facts wazi ktk ripoti zake, namna wizi ulivyotokea na wahusika ktk wizi huo. Ukisema unataka 'facts' zaidi, kutoka chanzo gn cha kuaminika zaidi ya serikali? (CAG).
   
 11. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,133
  Likes Received: 1,363
  Trophy Points: 280
  - CAG ni wakaguzi wa mhesabu sio wanasheria, ni simply Common Sense wala huhitaji PhD kuelewa hilo!, Crime huwa inakuwa established na DPP! au hata kamati ya Sheria ya bunge, lakini sio CAG!


  William.
   
 12. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,133
  Likes Received: 1,363
  Trophy Points: 280
  - Siwezi kutetea Waziri mwizi hata siku moja au kiongozi yoyote mwizi, lakini ni lazima kuwepo na legal facts kwa mbunge wa jamhuri kufikia kumuita waziri mwizi, kwa sababu sasa unaichokonoa Serikali, CAG imetoa hesabu, kama ilivyokuwa kule Ubalozi wa Italy, walitoa mahesabu ikawa kazi ya DPP kutengeneza LEGAL FACTS, kesi ikaenda kwenye sheria!

  - Unajua sometimes unaweza ukawa emotional na ukaishia kuharibu kila kitu, kama kuna mawaziri wezi na facts zipo, dawa ni kulilia kesi mahakamani kwanza, ama sivyo unawapa nafasi ya kujiuzulu tu na basi, ni utamaduni mbaya sana!


  William.
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Siwezi kuamini lisemwalo linatoka katika kinywa cha William Malecela. Ungeishi Tanzania tu ningeelewa. Lakini uzoefu wa kuishi nchi za nje na ambazo zina upeo wa hali ya juu katika uwajibikaji kwa watumishi wa umma halafu unakuja na utetezi dhaifu kama huu naweza kukuambia labda ulimi wako umeteleza au unajenga hoja ya watu wazidi kukudadafula tu.

  Fact namba moja hapa kwa mawaziri ni uwajibikaji kutokana na ukweli kwamba wao ndio vichwa katika wizara zao, na wanawajibika kusimamia ipasavyo. Sasa kama wameshindwa kusimamia wizara na hivyo kusababisha hasara kubwa serikalini hata kama uzembe huo umesababishwa na walio chini yao ni kosa la msimamizi mkuu katika wizara yake ambaye ni waziri na anapaswa kuwajibika.
   
 14. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  according to CAG report, the evidence is there, ukweli ni kwamba wanachama wa chama either ni ccm or cdm wako pale sio tu kwenye maslahi ya taifa bali pia ya chama...chama ndio kimekuweka pale ukiwakilishe alafu tena uweke sign kuonyesha huna imani na serikali yake...ndio hayo mambo tunasikia wabunge wanapigiwa simu wanatishiwa maisha. Sidhani hata kama mngepata the so called FACTS, full evidence wabunge wa ccm wasingefanya chochote..yule dr kingw..alisema ukweli..watu wamemlalamikia hapa but he was very honest with his answers...kwamba yeye ni ccm na atatatea ccm coz akiiangusha serikali ya ccm kuna uwezekano na yeye akaanguka kwenye jimbo lake...so self interest is and always will be there...
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Uongozi wa umma una taratibu za uongozi kupitia vyombo mbalimbali, unachoongea we ni kumwangalia mtu binafsi bila kujenga taswira ya majukumu ya huyu kiongozi mkuu wa wizara akiwa ndiye msimamizi mkuu wa wizara yake, sasa mkaguzi wa mahesabu wa serikali anapoona uvujaji huo mkubwa na waziri haoni tatizo aendelee kuvujisha wakati tatizo limeshaoekana, maana yake unatetea kulindana siyo?
   
 16. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 2,066
  Trophy Points: 280
  Malecela facts gani zaidi ya report ya CAG.
   
 17. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  willie,unaangalia na situation,its imposibo kwa hayo usemayo,suala la kwenda jimbon na kuanza kuhoj raia kwa maana hata ukitaka kuikataa bajeti itakupasa UKAWAULIZE RAIA
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145

  Kuna dhana ya upeo dhaifu kwa viongozi wetu kuelewa maana ya kuwawakilisha wananchi na kukitumikia chama. Mbunge au waziri hakitumikii chama chake bali wananchi, na anapaswa kuwatetea wananchi, kwa vile chama hakiwakilishi wananchi bali kinawakilisha kundi fulani la wananchi wenye itikadi fulani ambao ni sehemu tu ya wananchi wote. Na vyama vya siasa wanachama wake hawafikii hata theluthi moja ya wapiga kura wote, kwa maana hyo wabunge au mawaziri kutetea tu maslahi ya vyama vyao inajidhihirisha upeo mdogo wa kutoelewa maana ya uwakilishi wao kwa wananchi.
   
 19. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  Duh W.J leo umetoa mpya yaani anyeweza kutoa shutuma za wizi ni DPP tu kwa hiyo CAG aliwekwa wa nini? mbona sijawahi sikia DPP akitoa ripoti yake bungeni? au una maana ripoti ya CAG iende kwanza kwa DPP halafu ndo ijadiliwe bungeni?
   
 20. K

  KVM JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 180
  Sijui kama W. J. Malecela ni mwnasheria au la. Naona inainamia mno upande wa sheria. Katika maisha siyo kila kitu kiwe ni swala la sheria, na kwenye mambo ya siasa ndiyo kabisa. Kuna mambo ambayo mwanasiasa akifanya ambayo kisheria siyo makosa lakini kiutamaduni wa mahali n.k. inabidi awajibike. Hizo zinaitwa kashfa. Kwa mfano, katika nchi nyingine mambo ya uzinzi, ukahaba, kusema uongo, nk. havivumiliki.

  Naona Malecela ameamua kuwa mbanifu kwenye ukweli. Ripoti ya CAG inaheshimika duniani popote duniani. Ukishatajwa huko maana yake unastahili kushtakiwa kisheria. Mara nyingi katika nchi yetu sana sana unafukuzwa kazi.

  Tuchukue mifano miwili. waziri Nungu alisema Waziri mdogo ndiye alitaka kuleta mkataba mbovu. Yeye alikuwa amechukia hilo kwani lingelingarimu taifa. Lakini, badala ya kuagiza kuafanyika kwa upembuzi yakinifu ili kujua kinachotakiwa kufanyika kwa sheria za nchi yetu yeye aliamua kutafuta kampuni ya kwake. Hilo ni sawa? waziri mdogo alisema alienda nchi za nje bila kumuaga waziri wake kwa sababu waziri alikuwa nchi za nje. Je, ni wapi huko alikoenda waziri ambako hakuweza kuwasialian naye hata kwa simu au email? Kwa nini safari yake ilikuwa ni ghafla? Isingeweza kungoja au kujadiliwa kabla ya waziri kwenda nchi za nje.

  Chukua swala la Waziri Mkulo, kwa nini aliingilia maswala ya utendaji wa CHC na kuikwepa Bodi ya CHC, mara mbili?

  Kama bw. Malecela unaona kila kitu lazima kiwe ni swala la mahakama basi wewe hutaweza kutatua matatizo ya wananchi, na kibaya zaidi ukijua wazi wazi kuwa mahakama zetu zenyewe zinatakiwa kushtakiwa - sijui tutazishtaki wapi!
   
Loading...