Asante Pretty kwa mawazo na maneno yako mazuri...
mimi nitaongezea na kusema kuwa.... uwezo wa mtu au kutokuwa nao ni kitu binafsi na siyo cha kiujumlajumla.... haina maana kuwa wanawake wote ni vilaza..au kuwa wanaume wote basi ni vichwa. Sote tumeshashuhudia uwezo tofauti wa hawa viumbe. Nadhani maneno haya ni sehemu ya watu kujifurahisha na kujaribu kujipa moyo kuwa jambo hili linawezekana au haliwezekana ( filosofia zaidi).Kwa wale wenye watoto nadhani watanielewa.... malezi huchangia katika kufunua au kufunika vipaji, akili, maarifa na uwezo wa watoto - wawe wa kike au wa kiume.
Kweli wapo wenye kupenda njia za mkato mkato... huendekeza starehe zaidi ya kilichowapeleka chuoni na huweza kutumia mbinu zozote kuhakikisha wanafaulu. Haijalishi ni wanawake au wanaume. Kuna wanaume/ au vijana wa kiume hutoa hadi rushwa ya pesa ili wanunue mitihani wafaulu. Hatujazungumzia wale wenye kutegemea wasichana wenye uwezo wawatafunie ( kuchambua maswala mazito) ili wao wameze kwa kutayarisha madesa!
Sehemu za kazi utawaona wale wababaishaji waliofaulu kimkandamkanda....hawamudu majukumu yao... ni wepesi kujipendekeza na kutafuta kupendwa na wakubwa ili wapewe nafasi - hii haijalishi mtu ni mwanamke au mwanaume.Hawa wakijikuta hawana kazi utawaonea huruma maana hupata aibu mitaani .... hawajazoea kuogelea bila boya la kuelea lol! KAAAZI KWELI KWELI!
Wenye mawazo muflisi na tegemezi ndo wanaingia chuo na akili hizo. Ila boys sometimes wanatumia gia hiyo kama ndio sehemu ya kupatia yale mambo mengine. Siunajua tena mambo yanaweza kuwa rahisi kama unakuwa karibu na mtu...hata kama hakutaki anaweza kukuonea huruma.
mhhh. wadada wapo vichwa na wanasadia vidume...
Upande wangu mi nadhani tatizo akina dada wakiwa na akili nyingi wanakuwa wachoyo waku share vipaji vyao mara nyingi, labda kwa ma best wao tu.
Whereby akina kaka wengi atuna utamaduni huo, na ukiwa natabia hizo si jambo la ajabu kupewa label, hivyo mara nyingi utakuta makundi ya makaka wakisoma pamoja. Since akina dada wengi ni calculative kushinda akina kaka (again my opinion) huwa hawajali who they look for to get help, lao liende. Na hii mara nyingi hu changia average students (akina dada) kuingia makundi ya makaka kwenye revision not to mention makaka huongeza bidii kwa kuwafuruhisha akina 'hawa' wakiwa na agenda zao nyingine na wao.
Huu msemo kuwa " wasichana/akina dada husaidiwa na akina kaka vyuoni" unatoka wapi?
Nijuavyo mimi kila mmoja awe msichana au mvulana hufuzu kuingia chuo baada ya kupitia mchakato.Hakuna njia ya mkato.Iweje akishafika chuoni basi akili zake hupotea hadi asaidiwe kufaulu?
........Vile vile kuna tabia naona siku hizi inashamiri sana, mwanamke/mdada akiwa close tu na kiongozi wa siasa mwenye jinsia ya kiume basi mengi yanasemwa.......Ohhh anataka kupewa ubunge/uwaziri.
mwanamke huyo huyo akipewa position nzuri kazini basi watu wanaanza kuongea haswa wanaume. Je mwanamke ni mtu wa kubebwa kila mahali? Huyu kiumbe mwanamke hastahili position za juu ofisini hadi apendelewe?
Imefika kipindi inabidi tukubali tu kwamba mwanamke anaweza kufanya kitu kikubwa zaidi kuliko mwanaume. Kuna wanawake wana akili na wanajua kutumia akili zao kuliko wanaume.
Guys What are u talking about? Yaani Mnataka kuniambia bila mtu wa kukusaidia mambo hayataenda kabisa? Suala la kuwa nazo au kuwa kilaza ni suala la individual effort Mtu mpaka anafika chuo kikuu tayari ana potentials, na haitegemei mwanaume au mwanamke! Na kwa bahati nzuri kabisa ni kwamba mtihani wa kidato cha VI hauna cha mjomba wala shangazi! Pumba zooote huenguliwa hapo! Ila tunapofika vyuo vikuu gender huwa ina nafasi yake! Mwanamke akiamua kupita njia ya mkato ni rahisi sana kwake! (Nazungumzia mambo ya nipe nikupe)
Hitimisho
Kwenye academics hakuna cha mwanaume wala mwanamke! Ni suala la jitihada binafsi
Sio kweli Juma Contena. Ukiona mdada anafanya vizuri darasani na hapendi ku-share, tilia mashaka anafaulu vipi. kama anafaulu kwa kupata material kwa njia zisizo halali ni lazima afiche. lakini kama kweli anatumia akili zake huwa wanapenda sana kusaidia.
nakumbuka wakati nasoma chuo fulani tulikuwa na mkaka darasani kwetu ambaye shule ilikuwa haipandi kabisa, nilikuwa namwonea huruma sana. nikaweka mkakati wa kumsaidia yule kaka katika shule. nilichofanya ni kama somo nalifahamu vizuri nahakikisha nakuwa na muda wa kumfundisha na kama silifahamu basi namkamata mtu anayelifahamu vizuri atafute muda wa kumfundisha. Nilikuwa namfuatilia sana kuhakikisha kuwa anafaulu mitihani yote. mpaka sasa yule kaka huwa ananishukuru sana kwa kumsaidia, na hakuwa rafiki yangu na mpaka sasa wala siwezi kumweka kwenye kundi la marafiki zangu.
Haya basi nimekosea hila si nilisema mtazamo wangu tu huu. Lakini hii mimi nime base na life experience yangu. Kuna madada wawili zamani nakumbuka walikuwa noma vichwani hila duuh, kwa kweli walikuwa nuksi.
Huyo mmoja alikuwa anajulikana kwa kutoa toa msaada na kwa kweli akuwa the most popular girl in 'girls building' not that she cared either, though popular with teachers. Na hali akikisha mdada mmoja ambae nilikuwa na bidii sana za kumsaidia akai karibu na mimi matokeo yake nikaamishwa mimi kupelekwa mbele kabisa karibu na mdada mwingine huyo kipanga mwenzake.
Duuh dada akimaliza mtihani anashika tamaa kuniangalia ninavyoandika as if to say tukuone sasa leo uko mbele hapa amna msaada wa nyenzo kaazi kweli kweli nuksi yule. Hila this was primary if im honest.
Kwa vyuoni i do not how utamsaidia mtu apart kumshauri asome sijui how they work over there in bongo.Kumbe unazungumzia primary, sisi tunazungumzia vyuoni. Primary kule huwa ni mashindano, hata wakaka huwa hawawasaidii wadada maana hawataki wapitwe. Primary kila mtu anataka kuwa wa kwanza, sasa unaogopa ukisaidia mtu akakupita itakuwa noma.
Kwa vyuoni i do not how utamsaidia mtu apart kumshauri asome sijui how they work over there in bongo.
Mi nawaonaga engineering students ndio mara nyingi huu concentrate na group discussion na a few students doing bussiness account and things of that nature labda. The rest we just have to hit the books after the lectures usomi ufaulu simple as that na ukisema utumie muda mwingi kumfundisha mtu ambae aelewi utajikuta unaanguka nae.
Reading is very important huku, yaani unasoma unasoma na unasoma na kuna mashine za ku-detect plaigirism sasa kama kazi ina fanana much you have a problem. Hivyo kama ni weupe huwa drop outs no degree for them im sorry there is no help hapo.
My dear, usomaji vyuo vikuu vyote ni ule ule uwe ulaya, africa, bongo, asia, usa, wote tunasoma hivyo hivyo. na kusaidiana kusoma vyuoni ni thru group discussions. unaweza ukang'ang'ania vitabu, ukielewa vizuri ni good for you. lakini sometimes unaweza usome na usielewe ipasavyo, the only way to correct sumu uliyoshindwa kuelewa sawasawa ni thru discussions.
Kwa taarifa yako, kumsaidia mtu kuelewa sio kwamba unaweza ukaanguka naye. the good way kutilia mkazo ulichoelewa kitabuni ni thru practice. ukimfundisha mtu (I am telling you the truth) ni kwamba itakuchukua muda mrefu sana kusahau kile kitu, maana utakuwa ulielewa vizuri kiasi cha kuweza kufundisha mwingine. After all siyo kama utakuwa unamfundisha mtu 24hrs, kuna muda unahitaji kujisomea ili uweze kumfundisha.
Kuhusu swala la plagiarism, usiniambie kuwa kwa kuzama vitabuni unaweza kuliepuka hilo. unaweza ukawa msomi mzuri wa vitabu lakini ukashindwa ku-present issue kwa jinsi ulivyoelewa wewe, ukaishia ku-plagiarise.
Vyuo vikuu huwa tunasaidiana kusoma, maana huwa tunasoma kuelewa sio kushindana. kama upo kwenye position ya kusaidia wenzako fanya hivyo, na kama unahitaji msaada usisite kuomba msaada.
Inategemea huyu dada ameingiaje. Kuna wanaoingia kisiasa zaidi ili ku-equal idadi ya wavulana ktk fani husika.
Nakumbuka kuna mkakat flan nliwahi kuusikia wanafunzi wa kike walimwagma faculty ya engineering kwa fujo. Hawa walijiunga na chuo miezi kadhaa kabla wenzao wa mwaka wa kwanza waliochaguliwa kawaida hawajafungua chuo.
Lengo hapa lilikua kuwapiga msasa wadada hawa kabla ya chuo kufunguliwa.
Hebu mchukulie mdada alieingia ktk mpango huu wa 'ongeza idadi' tena engineering, what do you expect? Kutafuta mvulana (kumbuka hawa ndo wako wengi zaidi) ambaye atakua akimsaidia kimasomo.
Asante
Kwa vyuoni i do not how utamsaidia mtu apart kumshauri asome sijui how they work over there in bongo.
Mi nawaonaga engineering students ndio mara nyingi huu concentrate na group discussion na a few students doing bussiness account and things of that nature labda. The rest we just have to hit the books after the lectures usomi ufaulu simple as that na ukisema utumie muda mwingi kumfundisha mtu ambae aelewi utajikuta unaanguka nae.
Reading is very important huku, yaani unasoma unasoma na unasoma na kuna mashine za ku-detect plaigirism sasa kama kazi ina fanana much you have a problem. Hivyo kama ni weupe huwa drop outs no degree for them im sorry there is no help hapo.
sasa hapo umemsaidia au umemfanyia? na kwanza ilikuwa ya somo gani? na yupo au alikuwa chuo gani?Mkuu wacha hizo mimi nimewahi kumsaidia mtu mmoja kumwandikia thesis nikiwa bongo na yeye yuko UK.....unasemaje hapo?
Not that significant 0.00001%. The system is Transparent and I even know some who were busted out trying to sneak inNani anasema hayo maneno? unaongelea mtihani wa kidato cha 6 wa TZ au? kwa taarifa yako kuna wanafunzi kibao uanaingia vyuo vikuu wakiwa wamefaulu isivyo kihalali kidato cha 6, hii ni kutokana na kupata mitihani kabla n.k. hili halina ubishi. lakini pia kuna wengine wengi ambao wanaingia vyuoni wakiwa hawakufaulu vizuri ila wanapata nafasi sababu ya ndugu zao kuwa na nafasi fulani. hao akina mjomba na shangazi wana-play big role katika vijana kupata nafasi ya kujiunga na vyuo
It may not be completely true, It took me months to write mine! I can imagine with your job, serching for literatures, and articles which by virtual of being in Bongo is even difficult to access some of them! No! you wouldn't waste your precious work time for that, and neither you cant write a sound thesis in your leisure time! What you did, you helped with some proof reading, ideas/opinions/suggestions.Mkuu wacha hizo mimi nimewahi kumsaidia mtu mmoja kumwandikia thesis nikiwa bongo na yeye yuko UK.....unasemaje hapo?
Mkuu wacha hizo mimi nimewahi kumsaidia mtu mmoja kumwandikia thesis nikiwa bongo na yeye yuko UK.....unasemaje hapo?