Vyuoni huko - nani anamsaidia mwenzie?

Asante Pretty kwa mawazo na maneno yako mazuri...
mimi nitaongezea na kusema kuwa.... uwezo wa mtu au kutokuwa nao ni kitu binafsi na siyo cha kiujumlajumla.... haina maana kuwa wanawake wote ni vilaza..au kuwa wanaume wote basi ni vichwa. Sote tumeshashuhudia uwezo tofauti wa hawa viumbe. Nadhani maneno haya ni sehemu ya watu kujifurahisha na kujaribu kujipa moyo kuwa jambo hili linawezekana au haliwezekana ( filosofia zaidi).Kwa wale wenye watoto nadhani watanielewa.... malezi huchangia katika kufunua au kufunika vipaji, akili, maarifa na uwezo wa watoto - wawe wa kike au wa kiume.
Kweli wapo wenye kupenda njia za mkato mkato... huendekeza starehe zaidi ya kilichowapeleka chuoni na huweza kutumia mbinu zozote kuhakikisha wanafaulu. Haijalishi ni wanawake au wanaume. Kuna wanaume/ au vijana wa kiume hutoa hadi rushwa ya pesa ili wanunue mitihani wafaulu. Hatujazungumzia wale wenye kutegemea wasichana wenye uwezo wawatafunie ( kuchambua maswala mazito) ili wao wameze kwa kutayarisha madesa!
Sehemu za kazi utawaona wale wababaishaji waliofaulu kimkandamkanda....hawamudu majukumu yao... ni wepesi kujipendekeza na kutafuta kupendwa na wakubwa ili wapewe nafasi - hii haijalishi mtu ni mwanamke au mwanaume.Hawa wakijikuta hawana kazi utawaonea huruma maana hupata aibu mitaani .... hawajazoea kuogelea bila boya la kuelea lol! KAAAZI KWELI KWELI!

mpendwa hapo umamaliza kila kitu.............. any addition will be a distortion............

but my dear ladies and gentlemen remember that sexual factors are always there.......... and they are always powerful............ clever boyz and girls need to ballance them in the first place..............
 
Wenye mawazo muflisi na tegemezi ndo wanaingia chuo na akili hizo. Ila boys sometimes wanatumia gia hiyo kama ndio sehemu ya kupatia yale mambo mengine. Siunajua tena mambo yanaweza kuwa rahisi kama unakuwa karibu na mtu...hata kama hakutaki anaweza kukuonea huruma.

ha ha haaaaaaaaaaaaa, mnapenda kuonewa huruma?
 
Upande wangu mi nadhani tatizo akina dada wakiwa na akili nyingi wanakuwa wachoyo waku share vipaji vyao mara nyingi, labda kwa ma best wao tu.

Whereby akina kaka wengi atuna utamaduni huo, na ukiwa natabia hizo si jambo la ajabu kupewa label, hivyo mara nyingi utakuta makundi ya makaka wakisoma pamoja. Since akina dada wengi ni calculative kushinda akina kaka (again my opinion) huwa hawajali who they look for to get help, lao liende. Na hii mara nyingi hu changia average students (akina dada) kuingia makundi ya makaka kwenye revision not to mention makaka huongeza bidii kwa kuwafuruhisha akina 'hawa' wakiwa na agenda zao nyingine na wao.

Sio kweli Juma Contena. Ukiona mdada anafanya vizuri darasani na hapendi ku-share, tilia mashaka anafaulu vipi. kama anafaulu kwa kupata material kwa njia zisizo halali ni lazima afiche. lakini kama kweli anatumia akili zake huwa wanapenda sana kusaidia.
nakumbuka wakati nasoma chuo fulani tulikuwa na mkaka darasani kwetu ambaye shule ilikuwa haipandi kabisa, nilikuwa namwonea huruma sana. nikaweka mkakati wa kumsaidia yule kaka katika shule. nilichofanya ni kama somo nalifahamu vizuri nahakikisha nakuwa na muda wa kumfundisha na kama silifahamu basi namkamata mtu anayelifahamu vizuri atafute muda wa kumfundisha. Nilikuwa namfuatilia sana kuhakikisha kuwa anafaulu mitihani yote. mpaka sasa yule kaka huwa ananishukuru sana kwa kumsaidia, na hakuwa rafiki yangu na mpaka sasa wala siwezi kumweka kwenye kundi la marafiki zangu.
 
Huu msemo kuwa " wasichana/akina dada husaidiwa na akina kaka vyuoni" unatoka wapi?
Nijuavyo mimi kila mmoja awe msichana au mvulana hufuzu kuingia chuo baada ya kupitia mchakato.Hakuna njia ya mkato.Iweje akishafika chuoni basi akili zake hupotea hadi asaidiwe kufaulu?

wote wanasaidiana ijapokuwa kwa malengo tofauti
 
........Vile vile kuna tabia naona siku hizi inashamiri sana, mwanamke/mdada akiwa close tu na kiongozi wa siasa mwenye jinsia ya kiume basi mengi yanasemwa.......Ohhh anataka kupewa ubunge/uwaziri.
mwanamke huyo huyo akipewa position nzuri kazini basi watu wanaanza kuongea haswa wanaume. Je mwanamke ni mtu wa kubebwa kila mahali? Huyu kiumbe mwanamke hastahili position za juu ofisini hadi apendelewe?
Imefika kipindi inabidi tukubali tu kwamba mwanamke anaweza kufanya kitu kikubwa zaidi kuliko mwanaume. Kuna wanawake wana akili na wanajua kutumia akili zao kuliko wanaume.

Baadhi ya wanawake wako fiti kuliko wanaume, Mfano Kuna university fulani, Best students Eng dept 2006/2007 alikuwa mwanamke tena na average ya 96%. Tukizungumzia majority hapo ndipo wanaume wanakuwa wako juu kuliko wanawake. Ukiangalia ktk kila sector ya technologia, business, accounting n.k utakuta wanaume wanadominate.

Kusaidiana vyuoni ni kitu cha kawaida bila kujali msaada umetoka kwa mwanamke au mwanaume. Ila sisi wanaume tuna ile ya "You scratch my back and I'll scratch yours " yani kuwezi kusaidia mdada mpaka kuwa kuna pay back.
Uzuri wa dada zetu wakiwa wako fiti academically wala hawana matatizo, hawezi kuanza kukutongoza tongoza.
Tanzania bado hasa hasa ktk sector ya siasa mwanawake hawajaonyesha mwamko wa kutosha. Bunge la TZ linatakiwa liwe na ratio sawa kati ya wanaume na wanawake lkn imeshindikana ndio maana vikawekwa viti maalum vya kina mama ili kuboost lakini bado haijatosha. Mada hii aliizungumzia Msekwa alipokuja ziarani Uk hivi majuzi. Hii inaonyesha kwamba dada zetu wakaze buti kuprove themselves that they can do better than men.
4th president ni mwanaume at least wajitokeze miaka ya mbeleni najua kwamba they can.

Regards
 
Guys What are u talking about? Yaani Mnataka kuniambia bila mtu wa kukusaidia mambo hayataenda kabisa? Suala la kuwa nazo au kuwa kilaza ni suala la individual effort Mtu mpaka anafika chuo kikuu tayari ana potentials, na haitegemei mwanaume au mwanamke! Na kwa bahati nzuri kabisa ni kwamba mtihani wa kidato cha VI hauna cha mjomba wala shangazi! Pumba zooote huenguliwa hapo! Ila tunapofika vyuo vikuu gender huwa ina nafasi yake! Mwanamke akiamua kupita njia ya mkato ni rahisi sana kwake! (Nazungumzia mambo ya nipe nikupe)
Hitimisho
Kwenye academics hakuna cha mwanaume wala mwanamke! Ni suala la jitihada binafsi
 
Nani anasema hayo maneno? unaongelea mtihani wa kidato cha 6 wa TZ au? kwa taarifa yako kuna wanafunzi kibao uanaingia vyuo vikuu wakiwa wamefaulu isivyo kihalali kidato cha 6, hii ni kutokana na kupata mitihani kabla n.k. hili halina ubishi. lakini pia kuna wengine wengi ambao wanaingia vyuoni wakiwa hawakufaulu vizuri ila wanapata nafasi sababu ya ndugu zao kuwa na nafasi fulani. hao akina mjomba na shangazi wana-play big role katika vijana kupata nafasi ya kujiunga na vyuo
 
Sio kweli Juma Contena. Ukiona mdada anafanya vizuri darasani na hapendi ku-share, tilia mashaka anafaulu vipi. kama anafaulu kwa kupata material kwa njia zisizo halali ni lazima afiche. lakini kama kweli anatumia akili zake huwa wanapenda sana kusaidia.
nakumbuka wakati nasoma chuo fulani tulikuwa na mkaka darasani kwetu ambaye shule ilikuwa haipandi kabisa, nilikuwa namwonea huruma sana. nikaweka mkakati wa kumsaidia yule kaka katika shule. nilichofanya ni kama somo nalifahamu vizuri nahakikisha nakuwa na muda wa kumfundisha na kama silifahamu basi namkamata mtu anayelifahamu vizuri atafute muda wa kumfundisha. Nilikuwa namfuatilia sana kuhakikisha kuwa anafaulu mitihani yote. mpaka sasa yule kaka huwa ananishukuru sana kwa kumsaidia, na hakuwa rafiki yangu na mpaka sasa wala siwezi kumweka kwenye kundi la marafiki zangu.

Haya basi nimekosea hila si nilisema mtazamo wangu tu huu. Lakini hii mimi nime base na life experience yangu. Kuna madada wawili zamani nakumbuka walikuwa noma vichwani hila duuh, kwa kweli walikuwa nuksi.

Huyo mmoja alikuwa anajulikana kwa kutoa toa msaada na kwa kweli akuwa the most popular girl in 'girls building' not that she cared either, though popular with teachers. Na hali akikisha mdada mmoja ambae nilikuwa na bidii sana za kumsaidia akai karibu na mimi matokeo yake nikaamishwa mimi kupelekwa mbele kabisa karibu na mdada mwingine huyo kipanga mwenzake.

Duuh dada akimaliza mtihani anashika tamaa kuniangalia ninavyoandika as if to say tukuone sasa leo uko mbele hapa amna msaada wa nyenzo kaazi kweli kweli nuksi yule. Hila this was primary if im honest.
 
Kumbe unazungumzia primary, sisi tunazungumzia vyuoni. Primary kule huwa ni mashindano, hata wakaka huwa hawawasaidii wadada maana hawataki wapitwe. Primary kila mtu anataka kuwa wa kwanza, sasa unaogopa ukisaidia mtu akakupita itakuwa noma.
 
Kwa vyuoni i do not how utamsaidia mtu apart kumshauri asome sijui how they work over there in bongo.

Mi nawaonaga engineering students ndio mara nyingi huu concentrate na group discussion na a few students doing bussiness account and things of that nature labda. The rest we just have to hit the books after the lectures usomi ufaulu simple as that na ukisema utumie muda mwingi kumfundisha mtu ambae aelewi utajikuta unaanguka nae.

Reading is very important huku, yaani unasoma unasoma na unasoma na kuna mashine za ku-detect plaigirism sasa kama kazi ina fanana much you have a problem. Hivyo kama ni weupe huwa drop outs no degree for them im sorry there is no help hapo.
 
My dear, usomaji vyuo vikuu vyote ni ule ule uwe ulaya, africa, bongo, asia, usa, wote tunasoma hivyo hivyo. na kusaidiana kusoma vyuoni ni thru group discussions. unaweza ukang'ang'ania vitabu, ukielewa vizuri ni good for you. lakini sometimes unaweza usome na usielewe ipasavyo, the only way to correct sumu uliyoshindwa kuelewa sawasawa ni thru discussions.
Kwa taarifa yako, kumsaidia mtu kuelewa sio kwamba unaweza ukaanguka naye. the good way kutilia mkazo ulichoelewa kitabuni ni thru practice. ukimfundisha mtu (I am telling you the truth) ni kwamba itakuchukua muda mrefu sana kusahau kile kitu, maana utakuwa ulielewa vizuri kiasi cha kuweza kufundisha mwingine. After all siyo kama utakuwa unamfundisha mtu 24hrs, kuna muda unahitaji kujisomea ili uweze kumfundisha.
Kuhusu swala la plagiarism, usiniambie kuwa kwa kuzama vitabuni unaweza kuliepuka hilo. unaweza ukawa msomi mzuri wa vitabu lakini ukashindwa ku-present issue kwa jinsi ulivyoelewa wewe, ukaishia ku-plagiarise.
Vyuo vikuu huwa tunasaidiana kusoma, maana huwa tunasoma kuelewa sio kushindana. kama upo kwenye position ya kusaidia wenzako fanya hivyo, na kama unahitaji msaada usisite kuomba msaada.
 
Dada sio kukataa kusaidiana hila the nature of the business ndio inakubidi uchukue upande wako, apart from certain fields kama nilivyo kuelezea ambazo nadhani hata wao wanakua encouraged kujaribu ku discuss ili waweze jiinua na vile vile inakua part of employment training kwani in the future watu kama architects watajikuta wanafanya kazi in firms na ku-share ideas au accountants kujikuta wanafanya kazi group kutekeleza majukumu hivyo hapo mara nyingi huwa wanakuwa encouraged to do so.

turudi kwenye biashara yangu mimi ya social sciences mfano swali la essay au hata seen exam paper linaweza kuwa hivi out many option ntakupa matatu?

1. Should equality be a core principle underpinning social policy in a particular area like health, education, social security or housing? if yes what kind(s) of equality should be embedded in your area of a social policy?

Hapa markers wata angalia kitu kama understanding of policies ambazo azitakuwa na marks kubwa. Hila these people know their stuff wanajua kuna money involved therefore your evaluation will be based on the support you give hili waweze kujua wewe ni liberal thinker, left or right thinker.
Na to do so you'll have to hit the books to decide and use your moral guidance as a conclusion to support the argument. kwa hivyo how are you to help mtu hapo awe creative apart of telling him to hit the books. If he dint get it in the lecture or seminar group trust me he is not going to get it from me or you.

2. What do you think might be the right balance between 'rights' and disrection in social welfare? use examples to support your arguments (in terms of housing, income support, health care, education, or social care)

Hili ni swali kama la the great debaters (the movie with Danzel Washington) kama umeiona you cant teach someone to debate on an argument, if he knows nothing about the subject again he needs to refer to his lecture handout and hit the books. You can only discuss (debate) with someone who has read for you to gain; but trust you cant teach someone to be a debater especially kama asomi mwenyewe na ku make up his mind.

Nilisema ntakupa mifano mitatu hila nimechoka kuandika point hapa ni hivi some university programmes require you to hit the books and your marked on understanding and creativity and they do the best to make sure you understand the view point hila they cant teach you to be creative. Its for you to hit the books, ndio maana it doesnt make much difference hata ukipata a seen a exam kwa sababu at the end they look for your original ideas, they know what it means but do you? as a student. Unless huwe m-naigeria ukipata kitu kama essay au seen exam mbio kwenye site za kukusaidia.
 
Inategemea huyu dada ameingiaje. Kuna wanaoingia kisiasa zaidi ili ku-equal idadi ya wavulana ktk fani husika.

Nakumbuka kuna mkakat flan nliwahi kuusikia wanafunzi wa kike walimwagma faculty ya engineering kwa fujo. Hawa walijiunga na chuo miezi kadhaa kabla wenzao wa mwaka wa kwanza waliochaguliwa kawaida hawajafungua chuo.
Lengo hapa lilikua kuwapiga msasa wadada hawa kabla ya chuo kufunguliwa.

Hebu mchukulie mdada alieingia ktk mpango huu wa 'ongeza idadi' tena engineering, what do you expect? Kutafuta mvulana (kumbuka hawa ndo wako wengi zaidi) ambaye atakua akimsaidia kimasomo.

Asante

Tulikuwa tunawaita viwango duni
 
Kwa vyuoni i do not how utamsaidia mtu apart kumshauri asome sijui how they work over there in bongo.

Mi nawaonaga engineering students ndio mara nyingi huu concentrate na group discussion na a few students doing bussiness account and things of that nature labda. The rest we just have to hit the books after the lectures usomi ufaulu simple as that na ukisema utumie muda mwingi kumfundisha mtu ambae aelewi utajikuta unaanguka nae.

Reading is very important huku, yaani unasoma unasoma na unasoma na kuna mashine za ku-detect plaigirism sasa kama kazi ina fanana much you have a problem. Hivyo kama ni weupe huwa drop outs no degree for them im sorry there is no help hapo.

Mkuu wacha hizo mimi nimewahi kumsaidia mtu mmoja kumwandikia thesis nikiwa bongo na yeye yuko UK.....unasemaje hapo?
 
Mkuu wacha hizo mimi nimewahi kumsaidia mtu mmoja kumwandikia thesis nikiwa bongo na yeye yuko UK.....unasemaje hapo?
sasa hapo umemsaidia au umemfanyia? na kwanza ilikuwa ya somo gani? na yupo au alikuwa chuo gani?

Majibu ya ukweli yatasaidia kuweza kukujibu swali lako.
 
Nani anasema hayo maneno? unaongelea mtihani wa kidato cha 6 wa TZ au? kwa taarifa yako kuna wanafunzi kibao uanaingia vyuo vikuu wakiwa wamefaulu isivyo kihalali kidato cha 6, hii ni kutokana na kupata mitihani kabla n.k. hili halina ubishi. lakini pia kuna wengine wengi ambao wanaingia vyuoni wakiwa hawakufaulu vizuri ila wanapata nafasi sababu ya ndugu zao kuwa na nafasi fulani. hao akina mjomba na shangazi wana-play big role katika vijana kupata nafasi ya kujiunga na vyuo
Not that significant 0.00001%. The system is Transparent and I even know some who were busted out trying to sneak in
 
Mkuu wacha hizo mimi nimewahi kumsaidia mtu mmoja kumwandikia thesis nikiwa bongo na yeye yuko UK.....unasemaje hapo?
It may not be completely true, It took me months to write mine! I can imagine with your job, serching for literatures, and articles which by virtual of being in Bongo is even difficult to access some of them! No! you wouldn't waste your precious work time for that, and neither you cant write a sound thesis in your leisure time! What you did, you helped with some proof reading, ideas/opinions/suggestions.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom