Vyuoni huko - nani anamsaidia mwenzie? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyuoni huko - nani anamsaidia mwenzie?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WomanOfSubstance, Mar 19, 2010.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Huu msemo kuwa " wasichana/akina dada husaidiwa na akina kaka vyuoni" unatoka wapi?
  Nijuavyo mimi kila mmoja awe msichana au mvulana hufuzu kuingia chuo baada ya kupitia mchakato.Hakuna njia ya mkato.Iweje akishafika chuoni basi akili zake hupotea hadi asaidiwe kufaulu?
   
 2. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nijuavyo mimi, watu wakiwa vyuoni huwa na vikundi vyao vya kujisomea na kila mmoja huweza kuchangia majadilino (discussion) kwa kadri alivyoelewa "topic" fulani ya somo husika. Na hapa haichagui msichana/mwanamke au mvulana/mwanaume, wote huchangia. Katika darasa langu la Bachelor kuna wasichana wawili walipata "First Class" (UDSM) na walikuwa vipanga kweli na si kwasababu walisaidiwa na wavulana. Kwa kifupi ni kuwa wote husaidiana.
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Wenye mawazo muflisi na tegemezi ndo wanaingia chuo na akili hizo. Ila boys sometimes wanatumia gia hiyo kama ndio sehemu ya kupatia yale mambo mengine. Siunajua tena mambo yanaweza kuwa rahisi kama unakuwa karibu na mtu...hata kama hakutaki anaweza kukuonea huruma.
   
 4. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,170
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Inategemea huyu dada ameingiaje. Kuna wanaoingia kisiasa zaidi ili ku-equal idadi ya wavulana ktk fani husika.

  Nakumbuka kuna mkakat flan nliwahi kuusikia wanafunzi wa kike walimwagma faculty ya engineering kwa fujo. Hawa walijiunga na chuo miezi kadhaa kabla wenzao wa mwaka wa kwanza waliochaguliwa kawaida hawajafungua chuo.
  Lengo hapa lilikua kuwapiga msasa wadada hawa kabla ya chuo kufunguliwa.

  Hebu mchukulie mdada alieingia ktk mpango huu wa 'ongeza idadi' tena engineering, what do you expect? Kutafuta mvulana (kumbuka hawa ndo wako wengi zaidi) ambaye atakua akimsaidia kimasomo.

  Asante
   
 5. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yaani umenjibu swali ninalonikera mara nyingi. Huwa nahuzunishwa sana na dhana ya kuwa mabinti zetu wanapendelewa na wakufunzi wa kiume au kusaidiwa na vijana wa kiume. Tunasahau kabisa kuwa walifaulu darasa la saba, la kumi na mbili na la kumi na nne bila ya mkufunzi yeyote kuwapendelea, na bila mvulana yeyote kuwasaidia; wakienda ulaya huwa wanafaulu tu bila ya upendeleo wowote. Hii tabia ya kuwadhalilisha akina dada kuwa hawajitahidi inakatisha sana tamaa. Ni watoto wetu, ni dada zetu, ni mama zetu, hebu tuwape staha.
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Asante ndugu yangu.... hapo kwenye red hapooo! Kwani hao wasichana wachache ambao ni vichwa hawawezi kuwasaidia wenzao hadi watafute wavulana?...hebu dadavua zaidi...
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kwenye red.... nimekuwa nasikia na kusoma kuhusu hili na likanikera sana.. kitu watu wanasahau... kuna akina dada ambao nao wamejaaliwa kama kina kaka... je, akina kaka dhaifu huwatafuta wawasaidie au huenda kwa wanaume wenzao?

  Kwenye blue...huko kote walibahatisha?
   
 8. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ........Wanaume wanaolalamika kwamba wanawasaidia wadada huko vyuoni ni uzushi mtupu.
  Mtu hadi kufika chuo ni juhudi za mtu mwenyewe binafsi, iweje leo kafika chuoni asubiri msaada wa mwanaume?

  Ninavyojua mimi vyuoni kuna makundi ya discussion na vile vile watu mnaweza kusaidiana kimawazo iwe jinsia moja au tofauti. Ila kuna baadhi ya wanaume kama mlikuwa mnafanya discussion pamoja halafu akakutaka ili uwe mpenzi wake basi ukimtolea nje tu anaanza kuleta story hizi..........ohhh nilikusadia kukupa materials, mara nilikusadia kukufundisha topic hichi mara kile ilimradi tu apate kulalamika.

  Kuna wadada wengi tu vipanga kweli kweli huko vyuoni, wanawasaidia wanaume kimawazo lakini huwezi kuta hata siku moja wanalalamika. Hivyo wanaume ondoeni hii kasumba ya kulalamika hapa kwamba ulimsaidia mdada..........tenda wema uende zako usingoje shukrani.
   
 9. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #9
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 433
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 60
  What is the 'cutoff' point for admission: is it the same for both males and females? Or is there any group that is given 'affirmative action'? Why? Why not?
   
 10. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,170
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  WoS nadhani nature yenyewe inajieleza, like charges repel, unlike charges attract. Hahaha...

  Hivi do u know how welcoming boys are?! Especially to a woman/girl in need!

  Nadhani dada utakua shahidi wangu kua wanawake kwa wanawake bwana kufuatana kwa kwa ajili ya kupeana msaada wenyewe kwa wenyewe ni ngumu sana. Ni rare kwa kweli, sijui labda nyie wenzetu mnaelewa sababu.

  Kwa kweli hii ni experience yangu wakati nasoma.
   
 11. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ........Vile vile kuna tabia naona siku hizi inashamiri sana, mwanamke/mdada akiwa close tu na kiongozi wa siasa mwenye jinsia ya kiume basi mengi yanasemwa.......Ohhh anataka kupewa ubunge/uwaziri.
  mwanamke huyo huyo akipewa position nzuri kazini basi watu wanaanza kuongea haswa wanaume. Je mwanamke ni mtu wa kubebwa kila mahali? Huyu kiumbe mwanamke hastahili position za juu ofisini hadi apendelewe?
  Imefika kipindi inabidi tukubali tu kwamba mwanamke anaweza kufanya kitu kikubwa zaidi kuliko mwanaume. Kuna wanawake wana akili na wanajua kutumia akili zao kuliko wanaume.
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Asante Pretty kwa mawazo na maneno yako mazuri...
  mimi nitaongezea na kusema kuwa.... uwezo wa mtu au kutokuwa nao ni kitu binafsi na siyo cha kiujumlajumla.... haina maana kuwa wanawake wote ni vilaza..au kuwa wanaume wote basi ni vichwa. Sote tumeshashuhudia uwezo tofauti wa hawa viumbe. Nadhani maneno haya ni sehemu ya watu kujifurahisha na kujaribu kujipa moyo kuwa jambo hili linawezekana au haliwezekana ( filosofia zaidi).Kwa wale wenye watoto nadhani watanielewa.... malezi huchangia katika kufunua au kufunika vipaji, akili, maarifa na uwezo wa watoto - wawe wa kike au wa kiume.
  Kweli wapo wenye kupenda njia za mkato mkato... huendekeza starehe zaidi ya kilichowapeleka chuoni na huweza kutumia mbinu zozote kuhakikisha wanafaulu. Haijalishi ni wanawake au wanaume. Kuna wanaume/ au vijana wa kiume hutoa hadi rushwa ya pesa ili wanunue mitihani wafaulu. Hatujazungumzia wale wenye kutegemea wasichana wenye uwezo wawatafunie ( kuchambua maswala mazito) ili wao wameze kwa kutayarisha madesa!
  Sehemu za kazi utawaona wale wababaishaji waliofaulu kimkandamkanda....hawamudu majukumu yao... ni wepesi kujipendekeza na kutafuta kupendwa na wakubwa ili wapewe nafasi - hii haijalishi mtu ni mwanamke au mwanaume.Hawa wakijikuta hawana kazi utawaonea huruma maana hupata aibu mitaani .... hawajazoea kuogelea bila boya la kuelea lol! KAAAZI KWELI KWELI!
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,135
  Trophy Points: 280
  Kulikuwa na akina dada pale FoE ambapo katika jitihada zao za kujiunga katika makundi ya Wanaume ili waweze kushiriki katika discussion mbali mbali ili kufanya vizuri katika assignments na mitihani Wanaume walikuwa wanawapiga chenga kwa kuwaona ni vilaza, basi wakaamua kuwa na kundi lao wenyewe na walikuwa wanafanya vizuri kuliko Wanaume wengi. Hakuna ukweli wowote kwamba kila mwanamke aliyebahatika kufika chuoni ni kilaza wengi wana uwezo mkubwa tu wa kimasomo wa kuweza kushindana na hata Wanaume vipanga na pia kufanya vizuri kuliko Wanaume wengi.
   
 14. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  i studies abroad wote tulikuwa tunasaidiana girls and boys... to be honest men can be more helpful than women sometimes wanawake wanakuwa wanaringa mapozi halafu wivu sasa ndo usiseme...
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Asante kwa mchango wako. Hapo penye red --- huo wivu unatokana na nini au inakuwaje maana kama ni kwenda abroad wote mmekwenda kivyenu vyenu....hakuna alieyembeba mwenzie....
  kusaidia au kutosaidia ni uamuzi wa mtu na kila mtu yuko huru katika hili.. nikikataa kukusaidia utasemaje nina wivu?Hapo juu nadhani BAK kasema kuna wavulana walikuwa wanawakacha wasichana kuwasaidia..ina maana hawa wakaka walikuwa wana wivu?
  ( usikwazike ndugu..nachangamsha mada ndio maana nauliza maswali haya)
   
 16. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ukumbi wenu leo kina Dada ,jifaraguweni mtakavyo yatoweni yaliyomo moyoni mwenu .
   
 17. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Si hivyo tu, wengine tulisikia wakati tukisoma pale mlimani kuwa akina dada wengi wanaishi style ya Mafiga Matatu:

  1. BF wa Chuo anyemsaidia Masomo na Kuhakikisha anafaulu
  2. Sugar Daddy wa Kumpatia Mahitaji yake
  3. BF wa Kweli Chaguo la Moyo wangu.

  Akikosa No. 1: Basi Lecturer ataingiwa kinamna namna . . . Sijui simulizi hizi zilitoka wapi?
   
 18. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Upande wangu mi nadhani tatizo akina dada wakiwa na akili nyingi wanakuwa wachoyo waku share vipaji vyao mara nyingi, labda kwa ma best wao tu.

  Whereby akina kaka wengi atuna utamaduni huo, na ukiwa natabia hizo si jambo la ajabu kupewa label, hivyo mara nyingi utakuta makundi ya makaka wakisoma pamoja. Since akina dada wengi ni calculative kushinda akina kaka (again my opinion) huwa hawajali who they look for to get help, lao liende. Na hii mara nyingi hu changia average students (akina dada) kuingia makundi ya makaka kwenye revision not to mention makaka huongeza bidii kwa kuwafuruhisha akina 'hawa' wakiwa na agenda zao nyingine na wao.
   
 19. shejele

  shejele Senior Member

  #19
  Mar 20, 2010
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yeah nadhani ni ile kasumba ya " give and take" sasa mtu akiona mwenzie ni kupe tu anaachana nae, kama ulivyosema inawezekana wakaka wanakuwa wavumilivu kwa maana anatarget kitu kingine in reward japokuwa sio kwa kesi zote.
  Kwa kuongezea tu mi hadi nafika kidato cha sita discussion groups zangu zilikuwa ni wadada tu na walikuwa capable sanaa.
  Nilipokuwa chuo nikawa nashift wakati mwingine nadiscuss na wakaka wakati mwingine ni wadada tu na hakukuwa na tofauti sana.
   
 20. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ndiyo ukikataa kunisaidia kwenye elimu ntakuona una wive, Unapokataa kumsaidia mwenzio kwenye elimu inakuwa una wivu manake unadhani ukimsaidia mwezio atakuwa better than u... which is not true when u help others by sharing information u only help urself to understand the subject more... .. kama huo sio wivu ndio nini sasa...

  Hata makazini watu wengine hawapendi kuwafundisha wenzao kazi kwa kuogopa watachukuliwa cheo chao... I always tell my colleagues that if you want to grow in ur career then you must teach others, otherwise u will stay in ur place forever...

  na wale wakaka hapo juu walikuwa wanawivu if not intimidated...

  hujanikwaza dada bring it on:)
   
Loading...