hadi kuandika haya yote ni machungu tu ya chuo chako kushushwa,na aliyekishusha hapajui DIT kwa sababu ajasoma hapo,kwann na ww ukaamua kupashusha st.joseph pia haujasoma pale,huwez sema huyo mwny dvs 1.7 alizolewa pale wakati kaenda kujipanga na upya.........ndo tatzo lenu wa bongo hamjui kila kona na machungu yake.Mimi pia nilipita DIT miaka ile ya 1997 division one za Bwiru Boys,Moshi Tech, Iyunga Tech, Tanga Tech, Mtwara Tech, Ifunda Tech nk. Kumbuka hawa ni wadau wa PCM na hakukuwa na combination nyingine. Wengi wa watu wa shule hizo za ufundi ( nadeclare mimi nikiwemo) hesabu zilikuwa timam na kuchagua Tech College ilikuwa ni kwa sababu tuliandaliwa tangu kule Secondary. Wengi wa walimu na au ndugu zetu walitushauri kusomea kazi badala ya kusoma secondary tena. Na kweli faida zake nimeziona. Ijapokuwa mimi division one yangu ilikuwa ni point14 bado nakumbuka tulikuwa na jamaa kutoka Bwiru Boys na point 7 walikuwa watatu tena mmoja alifanya na mtihani wa Advanced Maths na akapata A! Baba yake alikuwa ni Engineer hivyo akamwambia nenda college kama chaguo sahihi.
Kwa kweli wakati naripoti pale DIT tuliambiwa Division One zako zinaishia getini na ukiremba tunakula kichwa na unadisco. Kumbuka hapo tumetoka sekondary ambapo mfumo ni tofauti na college, mambo ya discontinuation yalikuwa mageni na zile supplementary.
Nakumbuka kabisa tulipiga msuli hatari, warembo wa pale CBE unawaangalia tu ukikumbuka masomo kama Mechanics, Engineering Maths( by Gupta, Stroud) nk ilikuwa si mchezo.
Huwez kuamini mmoja wa wale division one ya point 7 matokeo yake hayakuwa mazuri paper la mwisho na hivyo division one iliishia getini kweli. Nasikia kaunga unga hadi kaenda St. Joseph( am sorry to say chuo zoa zoa ili mradi pesa tu)!
Hivyo nahitimisha kusema wengi wa tuliochagua Tech College wakati ule tulikuwa na uwezo wa kwenda F6 lakini option hiyo ilikuwa ni namba mbili. Mwisho wa siku wenzetu waliopitia F6 tumekutana tena UDSM na au makazini kwa level ya Uhandisi. Sema kama unataka ungwini na mambo tofauti na Engineering ni vema upitie F6 kwa maana ya wigo tu mpana wa machaguo ya degree na Siyo vinginevyo nikimaanisha uwezo wa kichwa. Kumbuka Technical Secondary schools zilikuwa ni vipaji maalumu Category Two na wengi ni vipanga wa hesabu.
Napingana na wewe! Si kweli kuwa mzumbe ni matajiri na wenye akili! Mzumbe kuna kujuana kuliko chuo chochote cha Tanzania! Wengi wa wanafunzi wanaoenda pale ni wale 'walioletwa' na mjomba au shangazi! Ni nadra sana kwa UDSM kuchukua mtu mwenye div 3 kwa ajili ya course za Sheria na Utawala!
Lakini ukienda Mzumbe utakuta watu wa namna hiyo! Hao wana akili?
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Umesahau walio ishia la saba wapo jamii forum wanaandika upuuzi kama wakwakoJuzi nilipokea ujumbe kwenye simu yangu kutoka kwenye namba ngeni, ilisomeka hivi:
Hebu cheki sifa za waendao vyuoni.
Matajiri na wenye akili-Mzumbe
Mahandsome na warembo-IFM
Maskini na washamba-SUA
Malaya na wasiojiweza kiakili-CBE Dar
Upeo mdogo na watoto wa mama-Tumaini
Waliokosa vyuo kabisa-MAKUMIRA, MWENGE
Waliokosa nafasi na watoto wa wakulima-UDOM
Wasiojali future zao-USTAWI, MUCOBS, SAUT, MWL NYERERE, TEKU, SEKUCO
Wenye uwezo ila walifeli FIV/FVI-IAA, DIT
Majigambo kibao lakini taaluma hamna kitu-UDSM
Wasiofahamu umuhimu wa elimu, wanategemea chabo ili wafaulu-Magogoni
what matter ni jinsi gani unatumia hiyo degree iwe ya mezani ama ya kitabuni..wewe adm yakwako ya chuo gani?
Kwa Masters Mzumbe ndio habari ya mjini kwa PhD Open ndio penyewe kabisa hila kwa heshima ESAMI,Nelson Mandela na SUA ndio penyewe.Mh! Preta, jamaa walipiga division za ukweli ila Mzumbe ndo wanagawa hizo masters km njugu
Utakuwa na mpuuzi au hujui kinachoendelea nchini, Technical colleges wanaenda watu wenye division one na two wengi tu, hata waliosoma FTC zamani na baadae wakaenda UDSM walitakiwa wawe walifauru vizuri form four, mfano waliopita system hiyo kwa kukusaidia ni Prof Mark Mwandosya DIT, Eng Dr Richard Masika DIT, Eng Stella Manyanya DIT, George Simbachawene ATC,Narudia tena . Ungefaulu vizuri sayansi na comb zinge balance. o level ungeenda a level na hiyo PCM yako then na huko ungefaulu vizuri ungeenda engineering UDSM. Marks zako hazikutosha o level na ndio maana ukapita njia ndefu huko kwenye diploma
kama umefaulu vizuri unaenda DIT kufanya nn achen uongo waliokuwa wanaenda huko ni waliopata marks ndogo
Watu hawataki kukubali kua UDSM ni chuo bora na kikongwe Tanzania, na wengi wao ufaulu wao uliwafanya wakose fursa ya kusoma UDSM wakiwa huko vyuo vingne wanapondaaa mara UD hamna kitu[emoji23]Kitaaluma UDSM hamna kitu alikutumia hyo text ni TEKu