Vyombo vya Habari Tanzania acheni upendeleo kwa chama tawala, Mtaligawa taifa? Hivi hamuelewi?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Nimejaribu kufuatilia jinsi coverage unavyofanywa na hizi local media zetu kuhusu matukio mbali mbali yanayofanywa na chama tawala CCM, hakika inasikitisha. Hakuna balance kabisa kwenye matukio ya kisiasa kati ya chama tawala na Upinzani.

Hivi vyombo vimeamua kua upande wa Chama Tawala hata kwenye urushaji habari na matangazo ya live, hili liko wazi na kila mmoja analijua. Mnataka mpaka mualikwe kwani kazi yenu si kutafuta matukio? Hii kwangu aiona kama ni aibu kubwa.

Hivi taaluma za waandishi wa habari wanazozisema ziko wapi? Tulizoea ITV ilikuwa balanced kwenye taarifa zake lakini kwa sasa ninashangaa sana kwa yanayoendelea. Haya ambayo miaka yote mmekuwa mkiyaripoti leo hii imekua ni uchochezi?

AZAM media na MillardAyo mnalalamikiwa sana na umma kuwa mmefuta taarifa za Mgombea urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu wakati akichukua form toka NEC kwenye mitandao yenu kwa sababu gani?

Toeni notifications kwa Umma ni kwanini mmefanya hivyo kwa wakati mmoja kama ni kweli?

Vyombo vya habari ni muhimu mwingine muhimu sana wa taifa, sasa mkiendelea hivi mtakosa credibility ya kuaminiwa na jamii. Iangalie ni CNN na BBC au DW kunapokuwa na matukio ya kisiasa nchini mwao wanavyokua balanced.
 
Vyama vya upinzani vijipange sana kuhusu media coverage kipindi cha campaign, mainstream media hazipo upande wao.

Wapate wataalamu wawatengenezee strategies hasa online and social media at least wanaweza kutengeneza voters influence.
 
Mkuu, bila ya kutoa mshiko coverage utaikosa. Wenzeni wanatoa eti nauli ya shilingi 100,000. Takukuru wanalijua hilo?
 
Tumekuwa na redio na tv mbao nyingi sana siku hizi, kisa unafiki wa waandishi wa habari kwa magu ili wapate ukuu wa wilaya.
 
Tumekuwa na redio na tv mbao nyingi sana siku hizi, kisa unafiki wa waandishi wa habari kwa magu ili wapate ukuu wa wilaya.
true, kuondokana nazo ni kuzinyima hata habari, wapost za nzi wa kijani, za wapinzani tutazipata BBC
 
Diamond platnumz alipohisi media zimepanga kum sabotage alifungua media yake. Alifanikiwa sana na sasa kwa takwimu za TCRA ndio media pendwa nchini yaani nambari uno.

Nyie chama ki kuu Cha upinzani hata jengo la ofisi hamna achilia mbali ki online TV. Saa nyingine mnaonekana kulalamika ndio sera mama ya chama chenu.
 
Upinzani unatakiwa kujua kwamba vyombo vya habari vinaendeshwa kwa sheria zilizopo hata kama ni mbaya lazima tuzifuate mpaka hapo zitakapobadilishwa.

Hakuna mmiliki Wa chombo chochote ambaye ata risk chombo chake kurusha habari za watu wasiotabirika watafanya nini au wataongea nini. Kwa sheria za sasa ni risk kubwa kwenda kurusha live matukio au hotuba za Chadema.

Media law act 2016 na kanuni zake zina vitanzi juu, chini, mbele na nyuma.
 
Mimi siku hizi sina muda wa kusoma,kusikiliza na wala kutazama media za kibongo zaidi ya kufuatilia habari kupitia mitandao.

Hivi vyombo vipoteze muda wa nini ? waliambiwa watu watajaa Dodoma sasa watu wenyewe hawaonekani ya nini kuendeleza uwongo wa chama cha Mbowe DJ.
 
Diamond platnumz alipohisi media zimepanga kum sabotage alifungua media yake. Alifanikiwa sana na sasa kwa takwimu za TCRA ndio media pendwa nchini yaani nambari uno.

Nyie chama ki kuu Cha upinzani hata jengo la ofisi hamna achilia mbali ki online TV. Saa nyingine mnaonekana kulalamika ndio sera mama ya chama chenu.
TBC ni chombo cha serikali sio Chama
 
Back
Top Bottom