Vyama vya Upinzani vinajiaandaje kwa uchaguzi wa 2025?

Natofautiana na wewe. Binafsi naona wananchi ndiyo wamedoda kama kiporo Cha viazi. Na wapinzani ni sehemu ya wananchi. Hivyo lawama zuende kwa wananchi.
Sio kweli Tanzania hakuna viongozi wa upinzani. Kiongozi halisi lazima afanane na wafuasi wake. Hata Bwana Yesu alikuwa akifanana na wanafunzi wake, ndiyo maana ilikuwa vigumu kumtambua hadi pale msaliti alipomtambulisha kwa kumbusu.

Viongozi wa upinzani hawafanani kabisa na wafuasi wao. Viongozi hawa wana mahoteli, wana forex, wana magari makubwa, wana mashamba ya kisasa, wana magesti house, wana magari makubwamakubwa, wana mabiashara makubwa kuliko wafuasi wao. Viongozi wananenepa na wafuasi wanakonda. Hii inasababisha wananchi waendelee na kazi zao hata kama viongozi wao wakikamatwa na vyombo vya dola
 
Askofu Gwajima hahubiri bali anapiga kampeni dhidi ya mama kwa 2025. Yaani ni heri mbinu ya Gwajima kuliko vyama vya upinzani vinasubiria chorus ya tume mbaya baada ya uchaguzi, sasa hivi wametulia wanakula nyani wala ndizi na jibini
Yeye na boss wake awatorudi tena bungeni hao
 
Back
Top Bottom