Hawa watu wa UK na Asia wanaofungua haya mashina ya CCM wanaboa kweli. I'll put em on blast this coming sunday. I just can't stand them grrrrrrrrrr.
Namna mojawapo ya kushughulikia hawa jamaa wanaofungua matawi kwa ajili ya kulinda status quo ama kama vitega uchumi vyao ama njia ya kujipenyeza kwenye system ni kuwashambulia kama wengine wanavyofanya hapa. Lakini namna nyingine ni kufungua matawi ya vyama mbadala; kuendeleza mapambano ya fikra. Kama wao nafungua matawi ya fikra za kifisadi bila matawi ya fikra nyingine hapawezi kuwa na vitovu organized vya mapambano ya fikra.
Huko tunapoelekea sheria za uchaguzi zitaruhusu watanzania walioko nje kupiga kura; how will political mobilization be done kama hakuna matawi?
Hivi karibuni tulikuwa na mazungumzo na msajili wa vyama vya siasa; na moja ya maeneo ni sheria zetu kueleza bayana kuhusu taratibu za ufunguaji wa matawi nje ya nchi. Kwa sasa sheria iko kimya; kuna mwanya wa matawi kufunguliwa kama affilliates wa vyama vya siasa nje ya nchi.
Pamoja na kujadili jinsi ya kuwapinga wanaofungua matawi kwa nia za kifisadi tujadili pia matawi genuine yafunguliwaje? Kwa nini? Yawe na muundo gani? Malengo gani?
Kikwazo kikubwa ni kuwa kuna matabaka katika watanzania walio nje ya nchi. Wengi ya watu wanaokerwa na yayofanywa na siasa za kifisadi, wengi wao pia wako nje ya nchi kwa njia za mkato- hivyo wakati mwingine wao kujitokeza kufungua matawi na kufanya siasa za upinzani nje ya nchi ni hatari kwa survival yao. Lakini kwa upande mwingine, wengi ya waliokwenda kwa njia iliyonyooka ni hao hao ambao ni wapenzi wa kulinda status quo na baadhi yao ni wanufaika wa ufisadi.
Lakini bado naamini kwamba wako watanzania wengi tu wenye uwezo wa kufungua matawi ya upinzani nje ya nchi, ambao wametimiza taratibu zote za kuwa nje; ambao hawahitaji kujipendekeza kwa Balozi za Tanzania nje ya nchi. Ni wakati wa kusimama na kuhesabiwa.
Nitafurahi siku moja- kukawa na mabalozi mbadala katika nchi mbalimbali; watakaoweza kuzikosoa hata balozi zetu nje ya nchi kama zikishindwa kutimiza wajibu wake kwa raia wa Tanzania walioko nchi hizo na hata kwa malengo ya kitaifa yaliyowapeleka huko. Nitafurahi siku hiyo! Nitafurahi kwa kuwa tutakuwa na mifumo mbadala ya kutoa hata sera mbadala za mambo ya nje kuhusiana na mahusiano yetu na nchi hizo. Lakini ili hili litokee, linahitaji wewe uliyeko huko; sio sisi viongozi wa kisiasa tulioko huku nyumbani.
Natambua kwamba kuna vyama vya watanzania walioko nchi hizo- wakati mwingine zinafanya malengo yanafanana kidogo na hayo- lakini hizi ni non partisan civil society; bado political activism inahitajika ili mradi tumeamua ku-organize vyama vyetu katika model ya matawi.
Otherwise; kwa wale ambao dhana ya matawi inawachefua; bado wananafasi ya kufanya siasa mbadala, siasa za upinzani nje ya nchi- kwa mtindo wa vuguvugu(movement). Chama cha siasa si lazima muundo pekee; hata mawazo tu yanayoratibiwa chini chini kwa vuguvugu yanaweza kuleta mabadiliko. Hayakamatiki; hayaonekani- lakini yana nguvu kubwa ya kuushinda mfumo wa kifisadi; madikteta kote duniani wanajua jinsi vuguvugu linavyoweza kuangusha tawala zinazominya demokrasia. Tujaribu, tutaweza!
JJ