(1). Uhalali wa mume wa balozi kuwa mwenyekiti wa tawi la ccm ambalo limeanzishwa na wananchi wachache wa-Tanzania, waishio London, je huu uhalali unakuwa in question kwa sheria zipi za bongo au za UK?
I mean ninaamini mume wa balozi ni mwananchi wa Tanzania aliyeko huko UK kwa sheria za kidiplomasia, ambazo ni makubaliano kati ya Tanzania na UK, kwenye kila ofisi yetu ya ubalozi nje kuna ofisa wa sheria, na wa usalama, kabla mume wa balozi kuwa mwenyekiti wa ccm au chama chochote huko nje, ni lazima mke wake ambaye ni balozi wetu awasiliane na hawa watu wawili ubalozini na kumpa okay mumewe kushiika hiyo nafasi, ni suala la wazi na very clear kwa mwananchi wa nchi yoyote duniani anayehusika na diplomasia, na kuhusu kibali cha kazi inategemea juu ya makubaliano kati yetu na serikali ya UK, ila ninaamini kuwa tunayo makubaliano ya namna hiyo yanyowaruhusu spouses wa maofisa wa ubalozi wao kwetu na sisi kwao kufanya kazi, otherwise binafsi sioni what is an ishu hapa, unless I am missing something?
au hili swali huenda linatakiwa kuelekezwa kwa serikali ya UK, badala ya wa-Tanzania!
(2). Anaweza ku-influence mambo ubalozini yakawa ki-ccm, you might have a point on this, lakini still, balozi wetu huko ni wa kuteuliwa na rais wetu ambaye ni mwenyekiti wa ccm taifa, au chama tawala, sasa nani anaweza kuwa na influence zaidi over balozi wetu huko, mwenyekiti wa taifa wa ccm au mume wa balozi ambaye mwenyekiti wa tawi dogo huko London? Serikali inaendeshwa na sera za ccm, ambazo moja ya kazi za balozi wetu huko nje ni kuzisimamia kwa nguvu zake zote kama alivyoapa mbele ya rais, sasa huyu mume ataongeza nini kwani msimamo wa ccm upo tayari ndani ya huyo balozi?
Uless Tanzania tunahitaji kuwa na sheria inayomkataza mume au mke wa kiongozi yoyote wa siasa, kujihusisha na siasa, ndani au nje ya nchi yetu, manake Anna Abdallah akiwa mwenyekiti wa UWT, na mumewe akiwa Spika wa bunge letu, si nayo ingekuwa a conflict of interest au? Waziri wa elimu na mke wa Spika, hiyo nayo vipi? Hatuwezi kisheria kuwalazimisha mke na mume kuwa na msimamo mmoja wa kisiasa, au kuwa na msimamo tofauti, nafikiri inapofikia hilo siasa comes to an end, the only problem ni pale tu hiyo influence inapokuwa inavunja any of our sheria au za huko UK, unless tena kama nina-miss something?
(3). Uhalali wa tawi la ccm London kutumia pesa zetu kuleta bendera na kulipia jengo, ninataka kuamini kuwa jengo hilo linalipiwa na either ccm tawi la huko huko London, au zinatoka makao makuu ya ccm, unless kuna ushahidi kwamba pesa zinazolipiwa ni za ubalozi ambazo zinatumwa na serikali yetu kwa ajili ya matumizi ya ubalozi, hapo kweli kutakuwa na ishu, lakini kama hatuna huo ushahidi basi haya yatakuwa ni majungu!
Otherwise, sioni tatizo lolote lile chama cha siasa chochote kile bongo kuwa na tawi lake huko majuu, mbona tunajua kuwa Dc kuna tawi la cuf, ingawa la siri lakini lipo, na hata Boston lipo tawi la cuf, tatizo ni nini?
Unajua huenda kuna something ninaki-miss na hii ishu, ama sivyo so far sioni tatizo ni nini? Kama kuna hela za serikali zimetumika kwenye shughuli za hili tawi la ccm, basi ushaidi uwekwe hapa au wazi lili wahusika waulizwe, ili kulinda hadhi ya hii forum!