Vyama vya siasa si ajira kwamba ni mahali pa kwenda kujipatia riziki.
Vyama vya siasa vina wajibu. Wajibu wake si mdogo.
Siasa ni kama mchezo wa mpira kuchukua na kuzitumia lose balls zote Ili kujipatia magoli.
Kumekuja kukapita mambo ya tozo. Kumekuja panya road. Kunafukuta ya bima ya afya. Kuna katiba mpya ambayo mbele na nyuma yake wala hakujulikani tena. Mauaji ya kiholela yanaendelea, nk nk.
Vyama vyetu viko kimya. Zaidi sana tunasikia pongezi eti kuwa mwendo sasa uwe huo unaoitwa wa kususa, ati hadi akili ziwakae watu sawa!
Mbatia ndiyo hivyo tayari yamemfika, alipo maji ya shingo. Hata pa kusemea tu amekosa kwa maelekezo pendwa kutoka juu.
Enyi vyama vya siasa, agenda zenu ni za kusubiri kupewa ushindi mezani na walio washindani wetu?
Hatupaswi kuchezeshwa ngoma na washindani wetu. Hawa tuna haki ya kuwachezesha yetu.
NInakazia: Aluta continua, mikutano ya siasa ni haki yetu. Twende kazi. Mengine tutayaona mbele kwa mbele.