Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,620
- 46,264
Hii mikutano kama ya Kituo cha demokrasia Tanzania(TCD), ya vyama vya siasa, sijui ya kamati za amani na maridhiano ni upotezaji muda tu, ni matumizi mabaya ya rasilimali fedha na muda na pia ni kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa.
Nchi ya miaka zaidi ya 60 haitakiwi kupoteza muda kupiga gumzo na kusogoa kwa mambo ambayo yako wazi kabisa kikatiba, kisheria na hata kwa common sense. Majadiliano yanayofanyika katika mikutano na vikao vya namna hii ilipaswa kufanyika katika shule za sekondari na vyuo vikuu.
Nimekuwa nikiona hata "mabeberu" wako na ushiriki mkubwa sana katika matukio ya aina hii wakati huko kwao hakuna mambo kama haya kabisa. Balozi wa Marekani atuambie ni lini Democrats na Republicans waliwahi kukaa tofauti na vikao rasmi vya bunge au na Rais Ikulu kupanga namna ya kutekeleza katiba ya Marekani katika masuala ya uchaguzi au mambo mengine yoyote ambayo katiba yao imekwisha weka muongozo.
Kwa nini huko Marekani Democrats na Republicans hawakai chini kukubaliana jinsi ya kwanyang'anya raia silaha?
Kwa nini hakuna mijadala nje ya bunge ya Democrats na Republicans kukubaliana kama Trump alishindwa au Biden alishinda 2020?
Tukue sasa tuheshimu katiba ya nchi, vyombo vya dola na mamlaka nyingine zote vitende wajibu wao kwa haki kwa kuzingatia katiba na pia tuheshimu uhuru wa kila mtu na kila kundi, tuachane na tabia za hovyo za binadamu wasiostaaribika.