The Legacy
JF-Expert Member
- Jun 1, 2022
- 8,217
- 16,089
Kuna SSH Sahani mapupu?
Chakula ni tamaduni.Jamaa wanajali sana AFYA.
Wanakula mbwa na viumbe vingine vizuri tu na hakuna shida.
ILA MHEHE AKILA MBWA anasemwa kila Kona. Tafadhari watuache kuanzia sasa
Hii inaitwa GWajimix food
hadi fisi wanakula?Hawaachi kitu
👊Wachina ni mojawapo wa mbari inayosifika duniani kwa ubunifu wa vyakula na mapishi.. Lakini pia ni watu wanaokula chochote chenye uhai kinachoonekana kwa macho
Kiwe aridhini
Kiwe angani
Kiwe majini
Walipitia kipindi cha msoto mkali wa baa la njaa na hii ikawafanya waweze kula chochote chenye uhai.. Lakini pia kuwa na uwezo wa kupika ladha anuwai kwa chakula kilekile
Mchina kila pishi anshakikisha linatiwa kiungo ambacho ni tiba mbadala mwilini na ni watu wanaokiheshimu sana chakula..
Muda wao rasmi wa kula ni saa 12-1 asubuhi
5-6 mchana
12-1 jioni
Chakula kikuu ubwabwa usio na kiungo chochote hata chumvi
Mboga ni lazima zisipungue 3 au4
Nyama/samaki 1
Mboga za majani 2
Supu/mchuzi
Pishi la mchina ufundi uko kwenye mboga
Formula ya kula
Asubuhi kula vizuri
Mchana kula ushibe
Jioni kula kidogo
Vyakula vyao huendana na majira..
Kuna vya majira ya joto
Kuna vyakula vya kiangazi
Kuna vyakula kipindi cha baridi
Nyama inayopendwa sana ni kitimoto na umbwa hii inajoto sana...
Nitaendelea kwenye maswali.. Mapicha pia kama yote😋😋😋View attachment 3357157
Duh, ila hawa jamaa hapana, kuna sehemu walikuwa wanajenga barabara mbwa walibaki wachache sana mtaani, vijana walijilipa sana kwa mbwa wa watu.Kama anapumua ni ndafu hiyo