Ukisikia wali jaa na mchuzi juu, jua tayari ushalishwa kiporo...Heshima kwenu wakuu.
Kama kichwa kinavojieleza hapo juu, naomba kujua vile vyakula vinavyobaki baada ya mauzo ya siku kule kwenye mahoteli, migahawa na mama lishe huwa vinaenda wapi?
Msaada kwa anaejua maana nina wasiwasi huwa tunalishwa viporo.
Wali/ ugali JAA maana yake wa jana...Hahaha hii terminology nilikuwa siielewi kumbe ndo maana yake.
Wali wa maji ukibaki, kesho utatiwa viungo na kuwa pilau. Maharage ya Leo, kesho yanatiwa tui la Nazi. Nyama iliyolala, kesho inakaangwa rost. Wali, ulioliwa na kubakizwa kwenye sahani, unaenguliwa na kurudishwa sufuriani. Maji ya kunywa wanachemsha ndoo moja ya Lita 20,wanachanganya na maji ambayo hayajachemshwa Lita 30,ili yanuke moshi, mnywaji ajue yamechemshwa, kumbe hola. Vijiko vinatumbukizwa na kutolewa kwenye maji na kurudiswa kwenye Huduma. Upo hapo brother?
Hmm... hatuna namna, ingawa mimi hupenda kwenda kwa watu niliowazoea, nikikosa bora nile hata chipsi dume au matunda...Tufanyeje mkuu ili tusilishwe viporo, au sisi wateja ndo tunahitaji viporo
Kiporo cha nyumbani ni tofauti na cha hotelini, kwa sababu hotelini unatoa pesa, wangekuwa wanatoa bure sidhani kama kuna mtu angelalamika humu...Mkuu ina maana nyumbani hamjawahi kuhifadhi chakula mkala kesho yake?
Heshima kwenu wakuu.
Kama kichwa kinavojieleza hapo juu, naomba kujua vile vyakula vinavyobaki baada ya mauzo ya siku kule kwenye mahoteli, migahawa na mama lishe huwa vinaenda wapi?
Msaada kwa anaejua maana nina wasiwasi huwa tunalishwa viporo.
Tatizo sio kuhifadhiwa vizuri, tatizo ni kwamba kwanini wasiweke wazi kwamba hiki ni kiporo ili mtu unaponunua unajua kabisa kuwa nanunua kiporo. Kwanini ununue kiporo kwa bei ya chakula cha leo?Kama kimehifadhiwa vizuri bila kuharibika hamna tofauti mkuu. Kama umeshakula hotelini jua umeshakula kiporo mara nyingi tu.
Duuh kiporo kiwe kitamu zaidi, mathalani ugali wa jana uwe mtamu kuliko wa leo?!!Si unauziwa tena siku zinazofata.
Ina maana wewe kwenu hujawahi kula kiporo cha jana kikawa kitamu zaidi ya chakula cha leo leo?
Uhifadhi wa vyakula ni kitu cha kawaida sana wala si kitu cha kushangaza.
Kariakoo ukisikia wali jaa mboga juu sio kwamba wanakujazia, kakuona wakuja na hautagundua wali wa jana na mboga ya juzi.Heshima kwenu wakuu.
Kama kichwa kinavojieleza hapo juu, naomba kujua vile vyakula vinavyobaki baada ya mauzo ya siku kule kwenye mahoteli, migahawa na mama lishe huwa vinaenda wapi?
Msaada kwa anaejua maana nina wasiwasi huwa tunalishwa viporo.
Hapo nakubaliana na wewe...Wafanyabiashara kitu cha kwanza wanachoangalia ni faida, vingine vitafuata. Usitegemee kila mfanyabiashara atasema ukweli ktk kila jambo.
Duuh kiporo kiwe kitamu zaidi, mathalani ugali wa jana uwe mtamu kuliko wa leo?!!