Ni muhimu Sana kupata mwanamke anayekusikiliza nafikiri kusikilizwa inatakiwa ndio iwe sifa kuu

Paul dybala

JF-Expert Member
Jul 30, 2023
304
1,096
Wakuu,

Yaani hapa nilipo nimejikuta Niko down Sana na Sio kwa sababu eti Nina shauku ya kutaka kumla manzi wangu...hapana ni just mzuka umekata tu na hiki kibaridi Cha dar sielewielewi.

Iko hivi wakuu, mimi tena nikileta mada humu kuhusu demu wangu yaani sijui hata mnifanyaje..

Huyu demu wangu huko msibani alikokuwa ameenda yapata wiki Sasa hivi kwa sababu aliondoka jumatano ilioyopita na yeye alisema atakaa siku tatu tu..kosa la kwanza Hilo

Sasa tokea juzi amekuwa akilalamika Sana kuwa simjali Mara anaumwa nimnunulie dawa kule Moshi baridi kifua kinabana. Mara huku msibani wanapika tu makande yeye hapendi bhasi kiroho safi Mimi huwa namzingatia..ili asijisikie vibaya


Sasa Jana baada ya yeye kunihakikishia kwa kusema leo lazima atakuja endapo nitamtumia nauli ...nikaona isiwe kesi mi nikamwambia ninakutumia nauli kwa masharti ya kuwa Mimi ndio nitakupokea magufuli terminal na tutaenda kwangu utakaa siku mbili ndio Kisha aende kwa dada yake kwa kuwa alienda msibani na dada yake kwa hio dada yake ye amebaki huko...akasema sawa

Ilivyofika sa sita mchana ya leo nikamtumia 40000 ikiwa mchanganuo wake apate ya kutolea na ya kula njiani kwa kuwa alisema nauli ni 33k.

Sasa wakuu baada ya kumtumia akaniambia hapo anaenda tu kuoga anasepa Hamna kilichobakia Kila kitu kipo sawa kwa kuwa na Mimi mtu wa mishe Sana nikaona nisilete genye kama za kijana anae balehe Kila dakika kumpigia kumuulizia kafika wapi. Cha msingi nilichoamini anakuja akifika karibu atanijulisha nikampokee na kwa kuwa niliuliza wadau mda wa kutoka Moshi Hadi dar kwa masaa niliopiga nikajua atafika sa nane au tisa usiku sikuwa na wasiwasi

Sasa mda huu Niko ghetto nimejupumzisha ili nisiwe na uchovu ,,si ndio ikabidi nimcheki kumjulia hali na kujua hatua zake za safari kuwa amefika wapi? Hapo ndio nikajikuta mood inakata baada ya kunijibu eti hajatoka Bado..

Mmmkee nimemfokea balaa...nikamwambia acha habari za kingese..nikamwambia iweje ameshindwa kusema mapema Kama haji Leo na kwanini siku nzima asubiri mpka nimempigia simu ndio aje na excuse za kipumbavu...nikamwambia hizo ni tabia za kishamba na kiswahili...Sasa Mimi sihangaiki na yeye tena..Kisha nikakata simu

Sasa wakuu nimekosea au na Mimi namuacha rasmi saivi maana huku nakoelekea nitakufa afu nikitaka kumuacha mwanamke Kama huyu nifanyaje? Mbona akilini Huwa nawaza jinsi navyomfanyaga na mwanaume mwingine atafanya vile Yani nikifumba tu macho picha hio inakuja moyo unalipuka.

Nisaidieni msinitikane Mimi napitia kwenye tanuli la moto mkali sana.
 
Uko sahihi, maelewano yanaanza kwenye kusikilizana, ni muhimu sana kuwa na mtu anaekusikiliza, mkisikilizana hakuna kitu kinaharibika kwakua mnakua tayari ku sort out. Sema uwe mkali kwa mke wako ulohalalishiwa
 
Hakuna mwanamke saivi ambaye mwanaume atamwambia amuoe aseme asubiri...

Huenda anamwanaume mwingine, au wewe unatudanganya...
Hizi generalization hizi...how can you be so sure? Unajua ni sababu zipi zimemfanya amwambie asubiri mwakani? Wanawake wote tunatumia ubongo mmoja, tuna malengo sawa na circumstances zinazofanana?

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom