Kenya 2022 Vurugu zanukia Kenya, mawakala wa Odinga waishtumu tume kufanya uhalifu

Kenya 2022 General Election

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,837
Mzee Odinga sijui kanusa kushindwa sijui
Mawakala wake wamekuwa wakilalamikiwa na Tume kuzua vurugu kila mara kwenye ukumbi wa kuhesabia kura Bomas

Wakala Mkuu wa odinga anasema Bomas imekuwa chumba cha uhalifu akimaanisha haamini mchakato wa uhakiki
 
Wanaosema kuna utulivu,uchaguzi wa Kenya,wameziba macho na masikio,matukio mengi,yameshatokea,mpaka ya kupigana risasi na kufariki msaidizi wa Mbunge.Msimamizi wa uchaguzi,hajulikani alipo.Wapo maofisa waliokimbia kituo cha kura.Ruto apunguziwa kura 10,000,Magari kukamatwa na karatasi zimeshapigwa kura,mashine za kura kuwa mbovu,sehemu nyingi.Malori kuwa na wapiga kura kutoka Uganda,Yupo aliyetoa form nne kwa mpiga kura, nk.
 
Ni suala la muda tu Kenya lazima kipigwe...utasikia Mtu anahojiwa anasema "Watangaze matokeo watu waendelee na shughuli zao".

Hao tume ya uchaguzi wenyewe wanajiandaa kisaikolojia kwanza maana wakitangaza matokeo ya uraisi ndio wamepiga filimbi "anzeni".

Hakuna wa kukubali mwenzake ashinde, sio Ruto wala Baba...tuwaombee sana jirani zetu hawa.
 
Sio mchezo hizi story za kweli au za kupika?
 
Kuna baadhi ya maeneo kwenye ngome ya mgombea wa urais kura za urais zimekuwa nyingi kuliko kura zilizopigwa kwa wagombea wengine kama gavana, seneta, mbunge nk. Ni kama watu walikuwa wanaenda kumpigia kura rais tu na kuondoka!
Tuwaombeeni jirani zetu.
 
Wewe utakuwa ni fisiemu ukidhani wote mnafanana kwa mipango mibovu ya maandalizi ya kupiga kura
 
Huyu Mzee Chebukati naye ni shida tupu.

Miaka zaidi ya tano yote yeye na tume yake hawakuweza kujipanga kuondoa makosa ya hovyo hovyo katika muundo wa uchaguzi?

Matatizo yanaweza kuanzia kwa hawa wajumbe wa tume ya uchaguzi.
Wakati huu ilitakiwa kila kitu kiwe kimekamilika, wao wanajivutavuta na kutia wasiwasi katika uchaguzi mzima.
 
Huko huko Kenya, miaka siyo mingi iliyopita kulikuwa na mtu anaitwa Kivuitu, hakuwa na tofauti yoyote na Jecha wetu hapa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…