Vurugu kubwa zatokea Kariakoo, Dar

Vurugu kubwa zatokea Kariakoo, Dar

ni vurugu kati ya machinga na askari swala kupanga vitu chini...mabomu yamepigwa hatari,wezi wamejipatia vitu,na inasemekana baadhi ya bidhaa za wamachinga zimechukuliwa na polisi muda si mrefu wamachinga wameandamana wanaenda msimbazi kituo cha polisi kufata bidhaa zao..lakini hii ni nchi gani ambayo raia akiwa mwizi anachomwa moto akitafuta kwa jasho lake anakamatwa anapigwa na mali zake zinachukuliwa wakati mafisadi wamekaa huko ofisini tu wanakula kodi za watanganyika bila kuchukuliwa hatua..sio haki kwa kweli..uamuzi upo juu ya kila mtanzania kuchagua chaguo sahihi..muda ni sasa.
 
Mmh! Ndio maana kule ndani ya bunge yule waziri alipokuwa anaelezea jinsi bomu la kienyeji lilivyo na linavyotengenezwa wabunge waliomba muongozo fasta kwa kujua athari yake raia wengine watajifunza!

Hiyo simple techonolgy wangekuwa wanaijua hao wamachinga leo mizinga ya konyagi,tambi za majiko na kituo cha mafuta big bon hapo kariakoo wangeuza sana!

Ingekuwa mkuki juu ya mkuki mpaka kielewekee

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
nimepita hapo nimekuta shughuli imeisha ila kuna majivu ya matairi yaliyochomwa na vipande vya matofali
 
Watu wamefunga maduka na biashara zingine baada ya kutokea askari wakifanya fujo, mabomu/risasi hakika sijajua anayeharibu amani nchi hii ni nani kati ya wananchi au serikali ya CCM?

Watu ndani ya nchi yao wakifanya shughuli zao za kihalali na mchana kweupe anapigwa mabomu, anatishiwa maisha, wakati huo huo yeye ndie mlipa kodi kwa maana kodi yake inamgeuka kumtishia maisha yake...

Ngojea aje Mbowe kama ataruhusu wamachinga kujiuzia tu bidhaa kila wanapoona panafaa bila utaratibu eti kwa kuwa wako huru katika nchi yao. Nenda hapo jirani Rwanda tu uone kama kuna wamachinga! acheni akili za matope.
 
Wakazi wa mtwara tunapanda magar tunakuja kuwasaidia komaa nao mpaka jion tutakuwa tmefka.musichokee tatzo leo nyie watu wa dar ni waoga sana...tukifka ngoma mpaka magogoni
 
BREAKING NEWS--NI VITA KARIAKOO, RISASI ZA ZARINDIMA NJENJE,MAGARI SOMA HAPA KUJUA

HABARI zilizotufikia Mda huu zinasema Vurugu kubwa imetokea mda huu maeneo ya kariakoo Jijini Dar Es Salaam na kupelekea Jeshi la polisi kurusha Risasi hovyo ili kuwatawanya Wamachinga walioanzisha Fujo hizo huku barabara za kuingia na kutoka kariakoo zikiwa zimefungwa kutokana na Matairi ya Gari yaliyochomwa moto barabarani.

Kwa Mujibu wa Shudhuda wetu aliyoko Maeneo hayo ya Kaliakoo anasema Chanzo cha vurugu hizo zinatokana na Wafanyabiashara Wadogodogo Maarufu Wamachinga kudai mfanya Biashara mwenzao kuuliwa na Mgambo wa jiji.

Shuhuda huyo alizidi kusema Mfanya Biashara huyo aliuliwa na Mgambo kwa kupigwa kipigo kikali na kumpelekea mauti, Wafanyabiashara hao wanadai hali hiyo ni ishara ya kuchoshwa na Manyanyaso hayo wanayofanyiwa na Mgambo hao na kuanzisha hali hiyo ya Fujo ambayo wanadai ni njia ya kupeleka ujumbe kwa Serikali.
Machinga wao wameshindwa kuua hata mgambo wawili? Huu ukondoo sijui mpaka lini!
 
Jiji lolote lile duniani lahitaji usafi na mipango, hatuwezi kubali watu wafanya biashara kiholela eti sababu ya kura. Hapana twahitaji endelea hivyo hatuna budi hata wachache waumie ili wengi wanufaike baadae
 
Walisubiri uchaguzi wa serikali za mitaa uishe, afu ndio muone makucha yao.
 
nasema wapigwe tu!!
si ndo hao wameipa ccm ushindi wa 70% daslamu?
kama wangekuwa vidume wangepaswa waambulie 40% tu!
_
 
hao wamachinga waende hadi lumumba wakawabane magambaaa
 
nasema wapigwe tu!!
si ndo hao wameipa ccm ushindi wa 70% daslamu?
kama wangekuwa vidume wangepaswa waambulie 40% tu!
_
wanatabikaaa lakn bado tu wanaipigia kura ccm....mkuu mtu akijifanya ccm sanaaa alafu huku anaumiaaa na shida wala hatakiwi kupewa msaada...maana hawakomi achaa wataabike tu
 
acha mshituliwe mmezidi umburura na kudekadeka huko bongo
 
Wanaume wa dar ni waoga sana hawana tofauti na mabinti
 
Back
Top Bottom