Tuchagua mazungumzo badala ya vurugu

Tuchagua mazungumzo badala ya vurugu

Best home tutor

Senior Member
Joined
May 8, 2026
Posts
194
Reaction score
265
TAFAKURI.

Saba Saba ni Sherehe ya Kitaifa, Sio Siku ya Vurugu na Maandamano Haramu
Tarehe Saba mwezi wa Saba ni siku takatifu katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ni siku ya Siku kuu ya Biashara ya Kimataifa ya NchiniTanzania, yenye chimbuko kubwa la kihistoria tangu kuundwa kwa chama cha TANU mnamo tarehe 7 Julai 1954 chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Ni siku ya mapumziko kitaifa iliyotengwa kwa ajili ya kusherehekea hatua za kiuchumi, kubadilishana fursa za kibiashara duniani, na kutafakari umoja wetu.

sio siku ya kufanya fujo, chokochoko, wala maandamano yasiyo na kibali.
Kuandamana bila kibali chini ya mgongo wa sikukuu ya kitaifa ni uhalifu, ni usaliti kwa nchi, na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya uzalendo.

Wale wote wanaojaribu kushawishi vijana kuingia barabarani bila kufuata sheria na taratibu za nchi, wanapaswa kukataliwa kwa nguvu zote.

Maandamano yasiyo na kibali sio haki, bali ni fujo na vurugu zinazolenga kuharibu miundombinu, kurudisha nyuma uchumi wetu, na kuhatarisha maisha ya wananchi wasio na hatia.

TuJifunzeni Kutokana na Somo la Oktoba 29.

Yeyote anayefikiri vurugu zinaweza kujenga nchi anapaswa kujifunza na kukumbuka vyema yaliyotokea Oktoba 29.

Tukio lile lilibeba funzo kubwa na la uchungu kwa taifa letu.

Vurugu Hazina Macho.
Hakuna maendeleo yanayozaliwa katikati ya moshi wa mabomu ya machozi, mawe, na uharibifu wa mali.

Siku ile ilitufundisha kuwa uvunjifu wa amani unawaumiza zaidi wananchi wa kawaida mama ntilie, wafanyabiashara wadogo, na vijana wanaotafuta riziki ya kila siku.

Amani Haina Badala.

Kupoteza amani ni kazi ya dakika moja, lakini kuirejesha ni gharama ya vizazi na vizazi. Kamwe tusiruhusu mawakala wa vurugu watupitishe tena katika njia hiyo ya giza.

Umuhimu wa Kuilinda Amani ya Nchi Yetu
Amani ndio mtaji mkuu na wa pekee ambao Tanzania tunauringia duniani kote.

Bila amani, hakuna biashara ya Saba Saba, hakuna shule, hakuna kilimo, wala hakuna maendeleo ya kiuchumi. Ulinzi wa amani hii sio kazi ya vyombo vya dola pekee, ni wajibu wa kila raia mwenye akili timamu na uzalendo wa dhati moyoni mwake.

Kujifanya mwanaharakati kwa kuvunja sheria za nchi ni upofu wa fikra.

Kama una hoja, ziko njia za kisheria na kistaarabu za kueleza changamoto zako, lakini sio kwa kuvuruga utaratibu na amani ya nchi.

Wito kwa Vijana wa Kitanzania,
Ndugu zangu, tusikubali kutumiwa kama chambo cha kisiasa au kiuchumi na watu wanaoshinda kwenye viyoyozi huku wakitaka ninyi mwingie barabarani kupambana na vyombo vya dola.

Tuwakatae kwa maneno na kwa vitendo. Siku ya Saba Saba iwe siku ya mapumziko, tafakari, na kujenga uchumi wetu, na sio siku ya kubomoa kile tulichokijenga kwa miaka mingi.

Mzalendo wa kweli anajenga, habomoi. Kataa maandamano yasiyo na kibali, linda amani ya Tanzania yetu.

Samia Suluhu Hassan
Ofisi ya Makamu wa Rais
Ofisi ya Waziri Mkuu

Balozi wa amani,,,,!!!!!.....
Bado naendelea kusoma nje ya darasa
 
Unatafuta uteuzi?
Kama mshauri kweli kwa waleta vurugu why uweke tag ya samia.. lengi lako aone nawe ufikiriwe kwenye uteuzi?

Hizi siasa majitaka, siasa za kujipendekeza uteuliwe, zimeharibu sana akili za watanzania wengi wenye uroho na uchu.
Yuko radhi awe mnafiki wa nafsi yake mwenyewe, mbele ya watu anajichekesha ila naamini akijifungia bafuni analia na kulaani yanayoendelea nchini

We unajitoa akili tu, hakuna kijana anaeshawishiwa, vijana wamechoka, tuna madini, rasilimali chungu nzima, lakini havina impact na uchumi wetu.
Viongozi wanaishi kishua wakati raia hali tete, kodi na tozo chungu mzima lakini hakuna maendeleo ya maana, utafungua kabiadhara kako, mamlaka zitabaki kukusumbua ww mpaka ujute kianzisha biashara.

Nchi ambayo afya tabu, umeme shida, elimi changamoto, miundo mbini tatizo.. bado viongozi wanatembelea magari ya milioni 500, kwa mwaka matumizi ya bilioni 500 kununia magari ya kifahari tu.

Ufisadi kila kona, na wanachekeana tu,
Viongozi wetu wangekuwa serious nadhani tungekuwa tunakimbizana hata na kina singapore huko.. tizama mataifa ambayo mwaka 60,70 tulikuwa sawa kiuchumi, wao leo wako wapi sisi tuko wapi?
Tunafelishwa na nani kama sio viongozi wetu?

Mshahara wa mtumishi wa umma, hapo hapo anajitafutia makazi, malzi, mavazi, usafiri, chakula n.ka

Kuna wapuuzi wanalipwa mamilioni ya hela, na bado wanaiba, ila gari bure, mafuta bure, umeme hawalipi, maji ni juu ya mtanzania, matibabu etc..

Mna hubiri amani bila haki.. ndio nyie ambao mwanamke akishika mimba mnampongeza kwa kumshika tumbo, bila kukumbuka UB40 uliotia hiyo mimba 😂🤣🤣,

Matumizi ya serikali ni ya hovyo wabunge karibia 300+ sijui, billions of money zinachezewa, viti maalum karibia 100, wana kazi ya kupiga piga makofi tu... waziri anakuja anaomba bajeti yenye karibu trilioni 1 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, mijtu pwa, pwa, pwah..

Siungi mkono vurugu, je nyie mshawahi kukaa chini na kujiuliza chanzo cha vurugu, mmechukua hatua gani?

Madaraka matamu mko radhi mmalize watz wenzenu ili nyie mkae madarakani.
 
Tujifunze watoto wetu kuuwawa kinyama
au wajifunze wao kuheshimu na kuthamini uhai wa raia wao?

Kama kutakuwa na maandamano 7/7 kikatiba ipo poa wacha raia wafurahie katiba yao mbovu!
 
Back
Top Bottom