James.L.Laiser
Member
- Feb 20, 2014
- 87
- 35
Taarifa kupitia ITV sa 2 leo tarehe 8/1 mtendaji wa serikali ya kijiji kapewa kipigo kikali kwa kosa la kubandika matokeo yanayoonyesha mgombea wa ccm kuwa mshindi badala ya wa NCCR.
alipata kichapo baada ya hapo wananchi wakamshurutisha amtangaze mgombea wa NCCR. Naomba kama kuna aliye na nyongeza aongezee au kurekebisha hapa. Ila kiukweli nimeipenda hii, juzi na jana maeneo kadhaa ya dsm viongozi wa ccm wamepewa kichapo kwa kosa hilo hilo la kuwatangaza washindi feki,
Naomba adhabu iwe kali zaidi
Ni kweli hata mm niliona habari hiyo saa 2 usiku huu kupitia kituo bora kabisa cha Television cha ITV.
Kwa wale ambao hawajafanikiwa kuiona habari hiyo itaonyeshwa tena saa 5:00 usiku huu.
Kilichotokea ni kwamba wagombea ktk uchaguzi waliopigiwa kura ni watatu. TLP kura 9 CCM kura 258 na NCCR 263. Ajabu eti Mtendaji akataka kumtangaza na kumwapisha mgombea wa Ccm kua ndie mshindi hivyo ndio anaestahili kua Mwenyekiti wa Kijiji.
Baada ya UKAWA kumtembezea kipigo huyo Mtendaji alikubali kumtangaza mgombea wa NCCR kwamba ndie mshindi na mwenyekiti wa kijiji. Aliomba msamaha kwa kudai kwamba alishinikizwa na viongozi wa Serikali kumtangaza mgombea wa Ccm alieshindwa kwamba ndie mwenyekiti.
Kwa uhakika kipigo alichopewa mtendaji kilisaidia kutenda haki na kuacha kuchakachua!