Vurugu Kilimanjaro Serikali za Mitaa,mtendaji apata kipondo

Vurugu Kilimanjaro Serikali za Mitaa,mtendaji apata kipondo

Kiongozi wa kutoa hicho kichapo yuko wapi??

Anitafute tafadhari ninaround zake tatu za biere hapa, duuuuuh ninausiku mwanana leo acha kabisa... Weita ongeza Kinana nyingine tafadhari

BACK TANGANYIKA
 
Huu ni mwaka wa maamuzi magumu, mtu yeyote atakayehujumu maamuzi ya wananchi atakua nihalali yetu na tutamfanya vile tunavyotaka, vyombo vya dola ni mali ya ccm vijiandae kisaikolojia
 
Kwanini watendaji wa kata na wakurugenzi wanatumia madaraka yao kupokonya haki ya wengi?je hawakujiandaa na vyama vingi vya siasa nchini?navyoona mimi hawa watendaji hawajui nafasi waliyonayo na wajibu wao kazini.wamekuwa wakitumiwa na chama cha magamba kupokonya haki ya wengi kidemokrasia,hii ni hatari sana maana wanahamasisha vurugu na kutoweka kwa amani nchini.ccm siamini kama wataachia madaraka kwa amani,maana wamekuwa mabingwa wa kujitangaza hata kama wameshindwa.mfano,kilichotokea moshi na dar es salaam iwe fundisho kwa wenye tabia kama hiyo.
 
Naona style ya kuwatwanga mangumi wanaochezea maamuzi ya wananchi imechukua kasi ya ajabu. Nimeona mtendaji yule kule Moshi akila makofi kama mtoto mtukutu. Jana nayo Makongoro Mahanga Mbunge kaponea chupuchupu kuzabwa heri yake ilikuwa uwapo wa Polisi tuu.
Jee ndivyo watakavyo CCM kuwa mpaka washughulikiwe ndio wakubali kushindwa?
 
Hao watendaji wajipime na hata hao wanaokubali kwenda kuapishwa wakijua kuwa hawakustahili nao pia wajipime. Serekali yetu hii sikivu imeshajua kuwa watz wa leo sio wa kujaribu kama maji ya mto kujaribu kuyavuka.
Kama kule Kirua Vunjo kijijini yamekuwa hayo basi hata huko kwingine, kama ulisimikwa ukijua hujashinda haya yaweza kukutokea. Nasikia jamaa kalazwa hospitali, ya nini yoote hayo wakati waliokutuma hakuna hata mmoja tu aliyekuja kukupa hata pole tu?
 
Bado kule tarime ambako ccm waliahilisha kuwaapisha wenyeviti na wajumbe ktk halmashauri ya mji kwa zoezi hilo lilikwama trh30.12.2014 likasogezwa baada ya maccm kutaka kuapishwa kwa mitaa miwili kwa nguvu wakapewa kichapo kisha hakimu akaishia njiani wakapanga trh6 ya juzi nayo imeshindikana sababu kubwa wanasema usalama haupo hadi sasa haijulikani ni lini wataapishwa
 
Ni kweli hicho kijiji kipo jimbo la Vunjo,ni aibu sana huwezi amini jambo kama hilo kutokea!lkn sasa wananchi washajua dawa yao maana hata Mh Pinda asharuhusu Wapigwe maana tushachoka.
 
Back
Top Bottom