Vodacom yahonga Wabunge Blackberry

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
430
Katika hatua ambayo imeibua mjadala mzito katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti, Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom imemwaga Blackberry kila moja ikiwa na thamani ya Shilingi laki 7 na muda wa maongezi wa Shilingi 100, 000 ka wabunge 23 wa kamati ya Miundombinu akiwemo Spika wa Bunge Anna Simamba Makinda.

Baadhi ya Wabunge wameripotiwa kukataa simu hizo huku Mwenyekiti wa Kamati hiyo Peter Serukamba na Spika Anna Makinda wakidaka ofa hiyo kiulaini.

Source; Gazeti la MWANAHABARI la leo

My Take:
Si kwamba huu ni mkakati wa Vpdacom kuzima kelele za Wabunge ambao wamekuwa wakidai kuwa makampuni ya simu yamekuwa yakiwakamua wananchi vya kutosha na yamekuwa yakilipa kodi kiduchu?
 
Hii ni rushwa, nchi nyingine hao waliopokea wote wangekuwa ndani. Takukuru vipi. Kama hizi kodi zinawawasha wapeleke mahospitalini na mashuleni.
 
Hii ni rushwa ya wazi wazi kabisa sijui kwa nini wabunge siku hizi wananunulika kwa bei rahisi sana
 
Kama hii ni kweli basi bunge letu litakuwa linanuka rushwa na Spika atatakiwa awajibike. Hivi Spika hana uwezo wa kununua blackberry? Safari zote anazofanya hizi per diem anashindwa kununua blackberry?

Na vodacom wametoa blackberry kwa wabunge kwa sababu gani? wabunge ndio watu maskini hivyo wanahitaji msaada?
 
Na hapo ndipo utaona wakichangia bungeni full usanii bla bla kwamba makampuni ya simu hayalipi kodi na nini mwisho wanaunga hoja mkono 100/...yaani wameshatuona sisi Wananchi kama mazuzu.
 
ni kile kinachotafsiriwa na wengi kama kuwaziba midomo wabunge wa j.k.kwa kuwapa simu aina ya blackbery laki 7.ili wabweteke kulikemea kampuni hilo nyonyaji lisilo lipa kodi.kila baada ya miaka 5.wamo spika wa mjengoni yule mama wa njombe.wengine wastukia mchezo.wagoma.

Source-mwananchi jumatatu.
 
Last edited by a moderator:
Basically Hawa Voda through M pesa Wamepora Kabisa Kazi za mabenk ambao wengi ni walipa Kodi!! Mbaya zaidi hawa mabwana Hawalipi Kabisa Kodi Kwenye Hiyo Biashara!! Hawa Watunga Budget wamekaa tu hawaoni hata Hiyo ni big source ya Mapato / Kodi!! Tangu lini mlipakodi halali anakwenda Bungeni Kuwapooza Wabunge?? Hapa Ujue Kuna Wizi mkubwa sana!! Mbona sijawaona Airtel wala TBL Wakijipendekeza Bungeni ili hali ni walipakodi Wakubwa!! Shame on this people!! Wanatoa Vinawati Hamsini na kukwepa kodi ya Mabilioni!!
 
Hii ni ukuzaji wa mambo. hata wewe hapo ulipo inawezekana kabisa unatumia simu uliyopewa bure na hizi kampuni za simu, na hii utasema ni rushwa au kuzibwa mdomo?
 
mhuu!!! Ya kweli hii.?

Kuna gazeti la Mwanahabari la leo limeripoti hili.Nimejaribu kulitafuta online silipati.Ni habari ya kweli maana hata Rukia Mtingwa wa Vodacom amehojiwa
 
ni kile kinachotafsiriwa na wengi kama kuwaziba midomo wabunge wa j.k.kwa kuwapa simu aina ya blackbery laki 7.ili wabweteke kulikemea kampuni hilo nyonyaji lisilo lipa kodi.kila baada ya miaka 5.wamo spika wa mjengoni yule mama wa njombe.wengine wastukia mchezo.wagoma.

Source-mwananchi jumatatu.

Kwanini wasiwape Polisi ziwasaidie mawasiliano na kuchukua ushahidi wa picha kwenye matukio mbalimbali?
 
Vodacom hata mimi wananipa simu mpya kila mwaka mwaka wa nne huu, kwa sasa ni BB ya tatu na kila wakinipa simu mpya wananipa na maongezi ya bure. Kwa kuwa ni mteja wao mzuri na hawataki nihame.

Dunia zingine sasa hivi simu ni bure bora utumie mtandao wao tu, kwa sasa hapa kwetu zinakwenda kwa "targeted market" lakini itafika huko kwa bure kwa wote ushindani ukizidi. Biashara ni matangazo, ujuwe hizo zinatoka kwenye bajeti yao ya matangazo, hiyo inaitwa "directional promotion" na si hongo hilo.
 
Basically Hawa Voda through M pesa Wamepora Kabisa Kazi za mabenk ambao wengi ni walipa Kodi!! Mbaya zaidi hawa mabwana Hawalipi Kabisa Kodi Kwenye Hiyo Biashara!! Hawa Watunga Budget wamekaa tu hawaoni hata Hiyo ni big source ya Mapato / Kodi!! Tangu lini mlipakodi halali anakwenda Bungeni Kuwapooza Wabunge?? Hapa Ujue Kuna Wizi mkubwa sana!! Mbona sijawaona Airtel wala TBL Wakijipendekeza Bungeni ili hali ni walipakodi Wakubwa!! Shame on this people!! Wanatoa Vinawati Hamsini na kukwepa kodi ya Mabilioni!!

I side with you. Niliwahi kusema hapa! Ila kuna watu ukigusia hii kitu ni wanakuona kichaa. Taasisi yoyote inayojishughulisha na kuweka, kutoa ama kubadilisha fedha lazima wasajiliwe na Benki Kuu ya Tanzania. Hebu benki kuu watuambie ni kwenye category gani MPESA, TIGO PESA nk wamesajiliwa kwa sheria ipi na wapi?
 
Vodacom hata mimi wananipa simu mpya kila mwaka mwaka wa nne huu, kwa sasa ni BB ya tatu na kila wakinipa simu mpya wananipa na maongezi ya bure. Kwa kuwa ni mteja wao mzuri na hawataki nihame.

Dunia zingine sasa hivi simu ni bure bora utumie mtandao wao tu, kwa sasa hapa kwetu zinakwenda kwa "targeted market" lakini itafika huko kwa bure kwa wote ushindani ukizidi. Biashara ni matangazo, ujuwe hizo zinatoka kwenye bajeti yao ya matangazo, hiyo inaitwa "directional promotion" na si hongo hilo.

zombe kwa ku-justify upo juu,,,,,,
 
Back
Top Bottom